Hakuna Udhuru kwa Muislamu au Asiyekuwa Muislamu Baada ya Leo, Kuhusiana na Vita Vipya vya Msalaba vinavyoitwa Uzayuni
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hakuna aliyesalia kwenye uso wa dunia hii ambaye hajui jinai zinazofanywa dhidi ya watu wasio na hatia wa Gaza. Kila mtu anajua jinsi dola jeuri ya Mayahudi inavyolipua majumba, na kuzibomoa juu ya vichwa vya wakaazi wake. Umbile la Mayahudi linawashambulia raia wasio na silaha, na kuwaua shahidi barabarani mchana kweupe.