Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 598
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Vichwa Vikuu vya Toleo 598
Vichwa Vikuu vya Toleo 598
Kwa kuzingatia mamlaka ya Lebanon kushiriki katika mazungumzo ya moja kwa moja ambayo hakika yatapelekea katika amani na uhalalishaji mahusiano na umbile nyakuzi na halifu la Kiyahudi, na kama sehemu ya kampeni ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon kuwatembelea wanasiasa, mamufti, wasomi, nyanja ya kisiasa, na watu mashuhuri, wajumbe kutoka Kamati Kuu ya Mawasiliano na kamati za shughuli za kikanda walifanya ziara. Hizi zilianza katika mji wa Sidon kusini mwa Lebanon kwa ziara ya Mbunge Dkt. Osama Saad, Katibu Mkuu wa Shirika Maarufu la Wananasseristi, na ziara ya Mufti wa Sidon na wilaya zake, Sheikh Salim Sousan. Hii ilifuatiwa na ziara katika mji mkuu, Beirut, kwa Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Shia, msomi Sheikh Ali Al-Khatib.
Mnamo Jumatano tarehe 12 Dhu al-Qa‘dah 1447 H sawia na tarehe 28 Aprili 2026 M, dada mwema, mbebaji da’wah aliyefanya kazi kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashidah ya pili kwa njia ya Utume, mwanachama katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Yemen, Dada Lamya bint Bashar alifariki.
Je, ni nini maana ya kauli za Trump zenye kusitasita—kutoa Iran masaa 48, kisha siku 5, kisha siku 10—na pendekezo lake la mpango wenye nukta 15? Namna gani ujanja wa kauli, nyingi kutoka kwa Trump na chache kutoka kwa Iran, na tangazo la televisheni ya Iran kukataa pendekezo la Trump? Matokeo ya hayo yote ni nini?