Jumamosi, 24 Shawwal 1447 | 2026/04/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi Salih bin Muhammad al-Shafrah

Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia inaomboleza mmoja wa Mashababu wake, ndugu Salih bin Muhammad al-Shafrah, aliyefariki mnamo Jumamosi, tarehe ishirini na moja ya Rabi’ al-Awwal 1447 H sawia na 13/09/2025 M. Alikuwa miongoni mwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika eneo la al-Qayrawān, ambaye alifanya kazi katika safu zake wakati wa zama zenye giza kuu za ukandamizaji na dhulma. Hakika alikuwa ameshikilia imara da‘wah yake, akijitolea katika kuibeba, akilingania Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, mwenye kuiamini ahadi ya Mola wake Mlezi na bishara njema ya Mtume wake Mtukufu (saw), mpaka alipofariki dunia. Hivyo ndivyo tunavyomhisabu, na wala hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu.

Mayahudi Wanachimba Makaburi kwa Mikono Yao Wenyewe Huku Watawala wa Waarabu na Waislamu Wakiuzuia Ummah wa Kiislamu Usiwazike

Katikati ya milipuko ya mabomu na makombora ya umbile la Mayahudi, ikinyesha moto juu ya vichwa vya watu wetu mjini Gaza, ambapo wanalenga ghorofa za makaazi, vyuo vikuu, shule, hospitali na misikiti, hata kuangusha mahema chini, kiasi kwamba mifupa ya watoto na nyama zao inachanganyika na vifusi, “mkutano wa aibu na waovu” ulikusanyika na kufanywa. Ilikuwa ni mkutano wa kilele wa watawala Ruwaibidha duni, waovu kutoka miongoni mwa Waarabu na wasio Waarabu.

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan: Kisimamo cha Port Sudan kwa ajili ya Kufelisha Mpango wa Kuitenganisha Darfur

Kisimamo kilichofanywa na Hizb ut Tahrir/Wilayat Sudan ili kufelisha mpango wa kuitenganisha Darfur kilipokelewa kwa maingiliano makubwa, ikiwemo takbir, tahlil, na kuungwa mkono, pamoja na uhamasishaji wa vyombo vya habari na wa kisiasa mbele ya msikiti mkuu katika mji wa Port Sudan. Waumini walikusanyika baada ya swala ya Ijumaa mnamo 20 Rabi' al-Awwal 1447 H 12 Septemba 2025 M kwenye Msikiti Mkuu wa Port Sudan katika kisimamo kilichofanywa na Hizb ut Tahrir/Wilayat Sudan mbele ya Msikiti huo Mkuu kama sehemu ya kampeni ya Hizb kukwamisha mpango wa kuitenganisha Darfur.

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu