Alhamisi, 22 Shawwal 1447 | 2026/04/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Kuitelekeza Gaza ni Doa katika vipaji vya Nyuso Zenu Enyi Wanajeshi wa Kinana na muhimu zaidi, ni Swali kutoka kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama

Kila siku, mtoto mjini Gaza hufa kwa njaa, au mzee hupumua pumzi yake ya mwisho bila dawa, au mwanamke hufunga macho yake kwa mara ya mwisho kwa maumivu yasiyoweza kuvumilika kutokana na kiu au njaa. Kila saa mbingu hutokwa na machozi, mawe yanapiga kelele, na ardhi inawalaani wale waliowaacha peke yao. Hii ndiyo Gaza... Gaza, ambayo imezingirwa si tu kwa mipaka na vifaru, bali na uzio wa usaliti uliosukwa na viongozi wa majeshi, watawala wa khiyana, na kimya cha Umma wao.

Kuhamishwa kwa Watu wa Arish ni Uhalifu wa Kisiasa Uliojificha kama Maendeleo

Wakati serikali ya Misri ikizungumzia "kuimarisha bandari ya Arish," kuigeuza kuwa bandari ya kimataifa na kuiunganisha na mradi mpya wa ukanda wa kiuchumi, uhalifu wa halisi unafanywa dhidi ya wakaazi wa kitongoji cha Al-Raisa huko Arish. Watu wanalazimishwa kuondoka majumbani mwao chini ya athari ya matingatinga, na nyumba zao zinabomolewa kinyume na matakwa yao kwa kisingizio cha manufaa ya umma. Wanakabiliwa na shinikizo la kisaikolojia na mazungumzo ambayo hayaendani na hadhi ya kibinadamu na yanakiuka kanuni za Kiislamu.

Vyombo vya Ukandamizaji vya Serikali ya Jordan Vyamkamata Sheikh Saeed Radwan kutoka Hizb ut Tahrir

Katika wakati ambapo watu wa Jordan kutoka kaskazini hadi kusini na kutoka matabaka yote ya maisha wanaongeza hasira na uungaji mkono kwa Gaza, ambayo inaangamizwa, watu wake wanakabiliwa na njaa ya kikatili inayolazimishwa na umbile halifu la Kiyahudi kwa njama za fedheha kutoka kwa serikali ya Jordan, na huku vyombo vya ukandamizaji vya serikali hii vikisimama kupinga uasi huu kupitia ukandamizaji na ukamataji wa wana na watu waheshimiwa wa Umma huu.

Hasira ya Watu wa Gaza kutoka Ng'ambo za Bahari Inataka Mzingiro Uvunjwe... Watu wa Misri na Jeshi lake Watakasirika Lini? Lini Hasira yao Itakuwa Moto wenye Kuteketeza Umbile la Kiyahudi na Tawala za Mamluki Zinazolilinda?

Wakati Gaza ikiwa inakufa kwa njaa, ikizingirwa kwa kimya cha aibu cha Waarabu na njama ya wazi ya kimataifa, kijana mmoja wa Kimisri kutoka ng'ambo, Anas Habib, alifunga milango ya ubalozi wa Misri nchini Uholanzi na kumwaga unga kwenye kizingiti chake. Alipiga kelele kwa jina la watu waliozingirwa wa Gaza na kuliita jeshi lake nchini Misri kuvunja mzingiro, kufungua kivuko, na kumaliza njaa ya kupangwa... Kilio kutoka nchi ya mbali kilisikika ndani ya nyoyo huru. Je, kuna yeyote kati ya watu wa Misri atakayejibu? Je, kuna ulinzi wowote katika nyoyo za watu wa jeshi la Kinana? Au kufuli zilizowekwa kwenye ubalozi wa Misri jijini The Hague ni za kikatili kidogo kuliko kufuli zilizowekwa kwenye utashi na silaha zao?!

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu