Kamandi Kuu ya Ulinzi ya Marekani (CENTCOM) ilitangaza kwamba jioni ya Jumamosi, 15 Machi 2025, ilianzisha msururu wa mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo lengwa ya Mahouthi nchini Yemen. Ilidai kuwa ilifanya mashambulizi sahihi dhidi ya maeneo lengwa ya kundi hilo kote Yemen, ikihalalisha mashambulizi hayo kama utetezi wa maslahi ya Marekani, kuzuia dhidi ya maadui, na kuregesha uhuru wa bahari, kulingana na taarifa yake. Kufikia Alhamisi jioni, Machi 20, makumi ya mashambulizi ya anga ya Marekani dhidi ya Yemen yalikuwa yameripotiwa, na kusababisha vifo vya watu 53 na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa, wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Kuna matarajio kwamba operesheni zitaendelea kwa wiki kadhaa. Haya ni mashambulizi ya kwanza dhidi ya Yemen tangu makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya umbile la Kiyahudi na Hamas mjini Gaza Januari iliyopita, kufuatia kiapo cha Trump cha "kuwamaliza kabisa."