Alhamisi, 06 Dhu al-Qi'dah 1447 | 2026/04/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Marekani Yaanzisha Mashambulizi ya Kikatili kwa Yemen Huku Majeshi Yetu Yakitulia tuli, Yakishindwa Kuinusuru Yemen na Gaza!

Kwa siku nyingi sasa, Amerika imekuwa ikianzisha mashambulizi ya kikatili kwa watu wetu nchini Yemen, kwa kutumia kile Rais wa Marekani Trump alichoeleza kuwa "nguvu kuu mbaya." Alikuwa amewatisha hapo awali, akichapisha, “JAHANAM ITANYESHA JUU YENU KWA NAMNA AMBAYO KWAME HAMJAWAHI KUONA KABLA!!”

Wakati wa Ziara yake nchini India, Tulsi Gabbard katika Taarifa yake Alieleza Kujitolea kwa Ushirikiano wa Marekani na India na Mapambano dhidi ya Uislamu na Waislamu

Ingawa maoni ya chuki yaliyotolewa na Mkuu wa Ujasusi wa Kitaifa wa Kruseda Amerika, Tulsi Gabbard wakati wa ziara yake nchini India juu ya mateso ya watu walio wachache nchini Bangladesh na 'Khilafah ya Kiislamu' hayakuwashtua watu wanaozingatia siasa na wapenda Uislamu wa nchi hii, yaliondoa aibu ya mwisho ya vibaraka wa Amerika nchini Bangladesh. Kwa sababu vibaraka hawa walikuuza kukubalika kusiko epukika kwa Amerika kama rafiki wa Bangladesh ili kukabiliana na India na kuwahakikishia watu wapenda Uislamu wa nchi hii kwamba Amerika ilikuwa imeacha sera ya "vita dhidi ya Uislamu". Ingawa ukweli ni kwamba, hata kama uongozi wa Amerika utabadilika, 'sera yao ya kigeni' haibadilika. Badala yake, Trump shupavu au utawala wake hupenda kuwatusi vibaraka wake na kufichua nia za ‘sera zao za kigeni’. Kwa hili ametaka uwajibikaji wa dolari milioni 29 ambazo zililipwa kwa vibaraka ili kubadilisha mazingira ya kisiasa ya Bangladesh, huku kutumia pesa kama hizo kudhibiti siasa za nchi huru ni uhalifu mkubwa na ni sawa na kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine.

Enyi Majeshi: Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache

Enyi Majeshi katika ardhi za Waislamu, hasa zile zinazoizunguka Palestina: Je, kuna udhuru wowote uliobaki kwa wanaoomba msamaha? Je, kuna hoja yoyote iliyobaki kwa wanaolaani? Vipi mnaweza kuona na kusikia uvamizi na mauaji ya Mayahudi hali mmekaa katika sehemu zenu, bila kutikisika, badala ya kuelekea katika ardhi ya Al-Ribat, Palestine Ardhi Iliyobarikiwa, ili kurudisha uvamizi wa Mayahudi na kuliondoa umbile lao?

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu