Jumatatu, 10 Dhu al-Qi'dah 1447 | 2026/04/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Urusi Yajaribu Kubandika Shtaka la Ugaidi kwa Chama Kinachoheshimika zaidi cha Kisiasa ili Kuhalalisha Ukandamizaji na Kufilisika kwake!

Chini ya kichwa cha habari: "Huduma ya Usalama ya Urusi yakamata seli ya kigaidi yenye uhusiano na Hizb ut Tahrir," Russia Today ilichapisha ripoti mnamo 5 Februari 2025, ikisema kwamba "Huduma ya Usalama ya Shirikisho la Urusi ilisambaratisha seli ya kigaidi yenye uhusiano na Hizb ut Tahrir huko Crimea na kuwakamata watu watano ambao walikuwa wakisajili wafuasi wa chama hicho, ambacho kimepigwa marufuku nchini Urusi." Video ilionyeshwa inayoonyesha operesheni ya ukamataji na uvamizi wa nyumba.

Maamuzi ya Mikutano ya Mawaziri wa Kiarabu ni Matupu na Hayatapita zaidi ya Maandishi kwenye Karatasi

Mkutano wa Mawaziri wa Pande Sita wa Kiarabu jijini Cairo mnamo Jumamosi, 1 Februari 2025, kuhusu Gaza na Kadhia ya Palestina ambayo ni pamoja na Jordan, Imarati, Saudi Arabia, Qatar, na Misri, pamoja na Katibu wa Kamati ya Utendaji ya Jumuiya ya Ukombozi wa Palestina na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu - walithibitisha katika taarifa yao kile walichokiita "uungaji mkono wao kamili wa watu wa Palestina juu ya ardhi yao na kuzingatia haki zao halali kwa mujibu wa sheria ya kimataifa."

Kuanguka kwa Khilafah Kunaashiria Wito wa Kuhuishwa Kwake

Mnamo tarehe 3 Machi 1924, sawia na 28 Rajab 1342 H, kikundi kidogo cha wasaliti wa Kituruki, wakiongozwa na Mustafa Kemal, walivunja urithi wa zaidi ya karne 13 za umoja wa Waislamu. Kuanzia wakati huo na kuendelea, Waislamu walipoteza paa lao juu ya vichwa vyao na wakawa mayatima. Leo, miaka 104 ya hijria imepita tangu tukio hili la kusikitisha. Baada ya kuanguka kwa Khilafah, makafiri waligawanya ulimwengu wa Kiislamu katika maeneo madogo yaliyojitenga. Waliweka vikwazo vya usafiri kati ya maeneo haya, yakihitaji pasipoti na visa, na kuharibu majeshi yetu, silaha, rasilimali, ardhi, uwezo wa binadamu, na teknolojia-kila kitu.

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu