Alhamisi, 13 Dhu al-Qi'dah 1447 | 2026/04/30
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Katika Kumbukumbu ya Kila Mwaka ya Kuvunjwa Khilafah na ukingoni mwa kuregea kwake, Tunaulingania Umma wa Kiislamu Uharakishe Kuisimamisha

Tangu Khilafah ilipovunjwa mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H, sawia na 3 Machi 1924 M, Ummah umekuwa ukipitia majanga na kushindwa mfululizo; kuanzia mgawanyiko wa ardhi yake, mpaka kunyang'anywa mali yake, na kuwaua wanawe, na kudhihakiwa matukufu yake na mashambulizi dhidi ya Sharia yake. Hata hivyo, leo Khilafah iko karibu zaidi kuliko wakati mwingine wowote kurudi, Rayah (bendera) yake iko tayari kupeperushwa kwa mara nyengine tena juu ya ardhi za Waislamu. Kwa hakika, tunaishi katika wakati unaokumbusha usiku ule watu wa Madina walipokuwa wakishauriana, wakikubaliana kwamba wakati umefika wa kumpa Bay'ah bwana wetu Muhammad (saw) kama kiongozi wao wa kisiasa na mkuu wa dola.

Watawala Vibaraka Wana Hofu juu ya Tishio kwa Viti vyao vya Utawala lakini Hawana Wasiwasi juu ya Vita vya Mauaji ya Halaiki!

Mnamo Jumanne na Jumatano, wizara za mambo ya nje za Jordan, Saudia, Imarati, Mamlaka ya Palestina na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu zililaani uchapishaji wa akaunti rasmi unaohusiana na umbile la Kiyahudi wa ramani za kanda hiyo ambazo ni pamoja na maeneo ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, Jordan, Lebanon na Syria, wakidai kwamba hayo ni ramani ya kihistoria ya umbile la Kiyahudi. Walionyesha wasiwasi wao kuhusu masuala mawili.

Unafiki wa Kisiasa katika Demokrasia Kamwe Hautaisha Mpaka Tuubadilishe kwa Siasa za Kiislamu

Mnamo tarehe 06/01/2025, rufaa ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Malaysia, Datuk Seri Najib Tun Razak kuhusu kuwepo kwa amri ya nyongeza ya Mfalme, inayomruhusu kutumikia kifungo chake kilichosalia chini ya kifungo cha nyumbani, imekubaliwa na mahakama kwa wingi wa 2-1. Majaji wa Mahakama ya Rufaa kisha wakaamuru kesi hiyo irudishwe katika Mahakama Kuu ili ombi la Najib la uhakiki wa mahakama lisikizwe na jaji mpya. Amri hii ya nyongeza, ambayo ni sehemu ya mchakato wa msamaha wa kifalme, imekuwa jambo la kawaida, ambalo halijawahi kutokea katika asili yake. Sambamba na hilo, kulikuwa na jambo jengine - mkusanyiko mkubwa wa kuonyesha mshikamano uliokusanyika nje ya mahakama, ulioandaliwa na vyama ambavyo hapo awali vilikuwa wapinzani wa kisiasa wa Waziri Mkuu huyo wa zamani.

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu