Jumapili, 05 Dhu al-Hijjah 1446 | 2025/06/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

“Unachokitafuta Kinakutafuta wewe”

(Imetafsiriwa)

Habari:

Islamabad, Pakistan – Baraza la mawaziri la Pakistan mnamo Jumanne lilimpandisha cheo Jenerali Syed Asim Munir, mkuu wa jeshi la nchi hiyo, hadi cheo cha field marshal, kufuatia mzozo wa hivi majuzi wa kijeshi kati ya nchi hiyo na India. (Aljazeera.com)

Maoni:

Tokeo muhimu sana na lisilotarajiwa la mzozo wa hivi majuzi wa siku nne kati ya India na Pakistan limekuwa dori yake kulazimisha watu kugundua maana. Watafutaji ukweli walipata uwazi katika njia yao, huku wafadhili na wanafiki wakifichuliwa walipokuwa wakitafuta vyeo na malipo. Kwa watu walioelewa wajibu wao, mzozo huu ulitoa fursa wazi ya kuunusuru Umma wa Muhammad (saw), ambao unaendelea kuteseka na ukatili mkubwa kiasi kwamba unashindana hata na ule waliotekelezwa na Wamongolia. Vita hivyo havikuonyesha tu uwezo na nguvu ya jeshi la Pakistan linazomiliki lakini pia viliwafanya watu washuhudie kusita kwa mamlaka katika kulitumia kwa kiwango chake kikamilifu. Watu pia walishuhudia kuongezeka kwa malipo na vyeo. Mfano wa upandishwaji cheo kama huo ni kile mkuu wa jeshi la Pakistan alipokea kwa njia ya tangazo la Jenerali Asim Munir kuwa Field Marshal. Field Marshal ni cheo cha juu zaidi katika jeshi, nafasi inayotolewa kwa watu binafsi kwa ajili ya huduma bora, ambayo mara nyingi ni ya ishara na inatolewa kwa ajili ya uongozi wa kipekee wa kijeshi, iliotengwa kwa ajili ya viongozi wa ajabu ambao sio tu wameamuru majeshi lakini pia kuunda hatima ya mataifa yao.

Vita katika historia vilipata majina yao baada ya kuhitimishwa, mara nyingi vilipewa jina la 'maeneo' au matukio muhimu au mikakati iliyotumiwa wakati wa vita. Ulimwengu wa kisasa wa kibepari umebadilisha vita kuwa operesheni, ambapo maamuzi huchukuliwa siri na vitendo vinatekelezwa kwa watu wa kawaida, kama tulivyoona katika matukio ya kimataifa ya miaka 25-30 iliyopita. "Vita dhidi ya Ugaidi", ilimaanisha tu kwamba vita vimeanzishwa kwa Waislamu kana kwamba wao ndio magaidi na walikua kama uyoga na lazima kuondolewa kama magugu. Hivyo vita ambavyo vilipewa jina mwaka 2001 na Rais wa Marekani George W Bush na kuungwa mkono na Mkuu wa Jeshi la Pakistan wakati huo, Pervez Musharraf, vinaendelea hadi leo.

Iwapo watalii wa Kibaniani watauawa nchini India basi operesheni lazima ifanyike kwenye misikiti na madrasa. Iwapo misikiti na madrasa hizi zingekuwa ndani ya India basi Pakistan isingekuwa na pingamizi, kwani India ina haki ya kukabiliana na magaidi wake kama vile Pakistan ina haki ya kuua watu wake wenyewe, na hivi majuzi tangu Machi 2025 jeshi la Pakistan linatumia nguvu kubwa kuwamaliza watu wake wenyewe. Lakini India ilipovuka mipaka ya kitaifa ya Pakistan, Pakistan iliamua kulipiza kisasi na kuipa operesheni hii jina la Bunyan al Marsoos. Jina hili limechukuliwa kutoka katika aya ya Surah al-Saff, ambapo Allah (swt) asema:

[إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِهِ صَفًّا كَأَنَّهُم بُنْيَانٌ مَّرْصُوصٌ]

“Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao pigana katika Njia yake kwa safu kama jengo lilio kamatana.” [As-Saff: 4]

Ibn ‘Abbas alito maoni yake juu ya maana ya Ayah, “kana kwamba walikuwa ni jengo lilio kamatana.” kwa kusema, "Wako kama jengo thabiti lisilosonga, kwa sababu sehemu zake zimeunganishwa pamoja."

Katika Sura hiyo hiyo kauli yake Mwenyezi Mungu,

[يأَيُّهَا الَّذِينَ ءَامَنُواْ لِمَ تَقُولُونَ مَا لاَ تَفْعَلُونَ]

“Enyi mlio amini! Kwa nini mnasema msiyo yatenda?” [As-Saff: 2] inakanusha wale wanaopuuza kutimiza ahadi zao.

Qatadah na Ad-Dahhak walisema kwamba Aya hii iliteremshwa ili kuwaonya baadhi ya watu waliokuwa wakisema kwamba waliua, wakapigana, wakadunga visu, na wakafanya hivi na hivi wakati wa vita, ingawa hawakufanya lolote katika hayo.

Said bin Jubayr amesema kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu:

[إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الَّذِينَ يُقَـتِلُونَ فِى سَبِيلِهِ صَفّاً]

“Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao pigana katika Njia yake kwa safu” [As-Saff: 4] “Kabla ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) hajaanza vita dhidi ya adui, alikuwa akipenda kupanga vikosi vyake katika safu; katika Sura hii, Mwenyezi Mungu anawafundisha waumini kufanya vivyo hivyo.” Pia amesema kuwa kauli yake Mwenyezi Mungu,

[كَأَنَّهُم بُنْيَـنٌ مَّرْصُوصٌ]

“kama jengo lilio kamatana.” [As-Saff: 4] inamaanisha kuwa sehemu zake zimeunganishwa pamoja katika safu kwa ajili ya vita.

Kutoka katika Sunnah, kwa Hadith iliyoandikwa ndani ya Sahih Mbili ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «آيَةُ الْمُنَافِقِ ثَلَاثٌ: إِذَا وَعَدَ أَخْلَفَ، وَإِذَا حَدَّثَ كَذَبَ، وَإِذَا اؤْتُمِنَ خَان»  “Alama za mnafiki ni tatu: anapoahidi huvunja ahadi, anaposema husema uongo, na anapoaminiwa hufanya khiyana.

Ummah ni walinzi wa jeshi la Pakistan kwa sababu Mwenyezi Mungu amedhihirisha nguvu na uwezo wao kwa ulimwengu. Wameegemea kwenye aya za Quran ili kuhalalisha nguvu zao kwa sababu wanatambua uhalisia kwamba hawana neno au ibara ambayo inaweza hata kukaribia yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu ndani ya Quran tukufu. Kuzitumia vibaya Aya hizi kwa manufaa ya kibinafsi huleta vitendo vyao kwenye unafiki na alama za mnafiki zimeelezwa wazi na Mtume Mtukufu (saw).

Kupata vyeo na malipo huku masuala yakiwa bado hayajatatuliwa na Uislamu ungali hautumiki hakutokani na kipimo cha Kiislamu. Rasuli wetu alitoa uamuzi akiwa amekaa kwenye kiwanja cha udongo cha msikiti wa Mtume. Aliongoza ghazwat, alifanya mikakati, alifundisha na kupigana bega kwa bega na ulimwengu ukashuhudia upanuzi wa aina yake. Ushindi na upanuzi wote huu umeahidiwa kwa Waislamu kwa sharti la utiifu wa asilimia mia moja tu na unaweza kupatikana kwa kamanda ambaye hatamani kuishi milele kwa ajili yake au jina lake bali anayefanya kazi kwa cheo chake cha milele katika Jannah. Vita vinavyopelekea kuasisiwa Khilafah vinasubiriwa sana na historia itavipa jina linalostahiki kwalo na jina la amiri wa jeshi hilo litang’ara machoni na nyoyoni mwa vizazi vya Ummah huu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ikhlaq Jehan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu