Ijumaa, 12 Dhu al-Hijjah 1447 | 2026/05/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Silsila ya Maswali Yaliyowasilishwa kwa

Amiri wa Hizb ut Tahrir

Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah katika Ukurasa Wake wa Kifikra wa Facebook
Jibu la Swali

Kazi ya Hizb ut Tahrir Baada ya Kusimama Khilafah Rashidah

Kwa: Yusuf Habashi

(Imetafsiriwa)

Swali:

Asslamu Alaikum wa Rahmat Allah wa Barakatuhu, Sheikh wetu muheshimiwa, Mwenyezi Mungu akuhifadhi na akupe ushindi mikononi mwako.

Yusuf Habashi kutoka ardhi ya az-Zaitouneh (Tunisia).

Ili kuendelea: Ningependa kuuliza kuhusiana na kuendelea kwa kazi ya Hizb ut Tahrir baada ya kusimama Khilafah Rashida:

Kazi yake itakuwa ni nini baada ya kusimama kwake? Kubakia kwake kutakuwa kwa lengo gani? Na dalili ya hilo ni ipi?

Jibu:

Wa Alaikum Assalam Wa Rahmatullahi Wa Barakatahu,

1- Ndiyo, Hizb itabakia baada ya kusimamishwa Khilafah, kwa sababu kuasisishwa kwa Hizb ni faradhi kabla ya Khilafah na baada yake. Imekuja katika kitabu, Hizb ut Tahrir Sura ya: “Sababu za Kuasisiwa kwa Hizb ut Tahrir”.

“Hizb ut Tahrir iliasisiwa kwa kuitikia Maneno ya Mwenyezi Mungu ﷻ,ِ

[وَلْتَكُنْ مِنْكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ]

“Na kuwe kutokana na nyinyi kundi (makundi) linalo lingania kheri na linalo amrisha mema na kukataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.” [Surah Aali Imran 3:104]. Hii ni kwa ajili ya kuuamsha Ummah wa Kiislamu kutokana na mporomoko mkubwa uliofikia, na kwa ajili ya ukombozi (tahrir) wa Ummah kutokana na fikra, mifumo na hukmu za ukafiri, na kutokana na udhibiti na ushawishi wa dola za kikafiri. Hii ni kwa ajili ya kufanya kazi ya kuirudisha dola ya Khilafah ya Kiislamu, ili hukmu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ﷻ irudi.”

Faradhi ya Shariah ya Kuanzisha Vyama vya Kisiasa

Kwanza, kuanzishwa kwa Hizb ni kuitikia Kauli ya Mwenyezi Mungu ﷻ.

[وَلْتَكُنْ مِنْكُمْ أُمَّةٌ]

“Na kuwe kutokana na nyinyi kundi (makundi).” Hii ni kwa sababu Mwenyezi Mungu amewaamuru Waislamu, katika aya hii, kwamba lazima kuwe na kundi lenye muundo (jamaa'ah), ambalo lazima litekeleze amri mbili:

Kwanza, kulingania kheri (khair), ambayo ni Dawah kwenye Uislamu.

Pili, kuamrisha yote yaliyo ma’ruf (mema) na kukataza yote yaliyo munkar (maovu).

Amri (amr) ya kuanzisha kundi lenye muundo ni talab (ombi). Hata hivyo, kuna muktadha (qarina) unaofanya kuwa ombi la lazima (talab jazim). Kazi ya kundi lenye muundo, kama ilivyoelezwa katika aya hapo juu- ya kuwalingania kwenye Uislamu, na kuamrisha yote yaliyo mema na kukataza yote yaliyo maovu- ni wajibu (faradhi) kwa Waislamu, ambao lazima wausimamishe. Hili linathibitishwa katika aya nyingi na hadith zinazotoa dalili ya ufaradhi huo. Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) amesema, ,«وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَتَأْمُرُنَّ بِالْمَعْرُوفِ وَلَتَنْهَوُنَّ عَنِ الْمُنْكَرِ أَوْ لَيُوشِكَنَّ اللَّهُ أَنْ يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عِقَابًا مِنْ عِنْدِهِ ثُمَّ لَتَدْعُنَّهُ فَلَا يَسْتَجِيبُ لَكُمْ» “Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake. Lazima muamrishe yote yaliyo mema na lazima mukataze yote yaliyo maovu. Vyenginevyo, Mwenyezi Mungu atakuteremshieni adhabu yake. Kisha mutamuomba, na asikujibuni.” [Imesimuliwa na Ahmad]. Hiyo ni qareenah (muktadha) kwamba ombi (talab) ni ombi la lazima (talab jaazim). Kwa hivyo amri ndani ya ombi hilo ni wujoob (faradhi).

Kundi lenye muundo lazima liwe chama cha kisiasa. Hii inatokana na mtazamo kwamba ayah inaomba Waislamu kuanzisha kikundi kutoka miongoni mwao, na kutokana na mtazamo wa kufafanua kazi ya kundi hili kama Dawah kwa Uislamu, na kuamuru yote yaliyo mema, na kukataza yote yaliyo maovu.

Kitendo cha kuamrisha yote yaliyo mema, na kukataza yote yaliyo maovu, ni pamoja na kuwaamurisha watawala yote yaliyo mema, na kuwakataza yote yaliyo maovu. Hakika, kazi muhimu zaidi ya kuamrisha yote yaliyo mema, na kukataza yote yaliyo maovu, ni kumhisabu (muhaasabah) mtawala, na kuwapa ushauri. Kitendo hiki ni cha kisiasa. Zaidi ya hayo, ni miongoni mwa vitendo muhimu zaidi vya kisiasa, na ni mojawapo ya vitendo maarufu zaidi vya vyama vya kisiasa. Kwa hivyo, aya inatoa dalili ya wajibu (wujoob) wa kuanzisha vyama vya kisiasa.

Hata hivyo, aya inaweka kizuizi kwamba miundo hii lazima iwe vyama vya Kiislamu, kwa sababu kazi ambazo aya imezifafanua, ambazo ni Dawah kwa Uislamu, kuamrisha yote yaliyo mema na kukataza yote yaliyo maovu - kwa mujibu wa hukmu za Sharia za Uislamu - haziwezi kufanywa, isipokuwa na miundo na vyama ambavyo ni vya Kiislamu.”

2- Kwa hivyo, Hizb itaendelea baada ya kuanzishwa kwa Khilafah, lakini kazi itakayofanya inapofikia mamlakani inatofautiana na kazi iliyofanya kabla ya kuanzishwa kwake, kulingana na hukmu husika za Kiislamu.

Tulifafanua hili katika Swali la Jibu la tarehe 30/12/2014, ambapo ilisemwa:

“Hizb inatekeleza vitendo vinne: kutoa thaqafa (ya umakini na jumla), na mvutano wa kifikra katika suala la kufafanua fikra sahihi kutoka kwa fikra batili na fisadifu. Vitendo hivi viwili si mada ya uwajibishaji, bali ni kazi ya kithaqafa na kifikra ya hizb. Kazi ya hizb kufanya yote mawili inaendelea, kabla na baada ya hukmu, kwani haiathiriwi na kuchukua madaraka kwa hizb.

Ama kazi ya tatu (kufichua mipango), si kazi ya hizb tena kwa sababu uwepo wa hizb madarakani umeondoa suala la hizb kufichua mipango ya kikoloni. Badala yake, inafanywa na vyombo vya serikali, na kuwahisabu watawala kwa kutabanni maslahi, kama ilivyokuwa kabla ya utawala, inabakia na inafanywa na Kamati za Wilaya.

Kamati za Wilaya, kama ilivyo kabla ya utawala, zina mamlaka ya kuuhisabu uongozi wa hizb (Amiri na afisi yake), kwa hivyo zinaendelea kuwa na mamlaka haya ya kuuwajibisha uongozi wa hizb wakati ukiwa madarakani, na katika kutabanni maslahi ya Ummah kwa mujibu wa Shariah na kuwaangalia kwa wema na uhodari.”

Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Zaidi na Mwingi wa Hekima.

Ndugu yenu,

Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah

5 Dhul Hijjah 1447 H

Sawia na 22/05/2026 M

Link ya jibu hili kutoka ukurasa wa Amiri wa Facebook.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu