Alhamisi, 01 Ramadan 1444 | 2023/03/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Enyi Waislamu! Zuieni Mateso ya Serikali kwa wale Wanaolingania Kuregeshwa kwa Utawala wa Haki na Uadilifu - Khilafah

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir ina kazi ya kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kwa kuzikomboa nchi za Kiislamu, ikiwemo Bangladesh, kutoka katika makucha ya Wakoloni makafiri na kusimamisha tena Khilafah Rashida; na Wakoloni wa makafiri wanajaribu kuzuia kurudi kwa Khilafah kupitia vibaraka wao - watawala masekula wa Waislamu. Serikali ya Hasina ni moja ya watawala hao vibaraka ambayo inajaribu kinidhamu kuwakandamiza viongozi na wanaharakati wa Hizb ut Tahrir wanaoongoza harakati za kusimamisha tena Khilafah katika nchi hii. Licha ya kuwa ni chama cha kisiasa na kimfumo kisicho na vurugu, inawakamata na kuwafungulia mashitaka viongozi na wanaharakati wa Hizb ut Tahrir chini ya sheria mashuhuri ya kupambana na ugaidi, kuwaweka kizuizini katika korokoro za siri bila kuwafikisha mahakamani kwa wakati, kuwanyima dhamana mara kwa mara na kuwaweka kifungoni pasipo haki, kuwatishia wanafamilia, kwa kujaribu kimakosa kuchukua "taarifa ya kukiri" chini ya Kifungu cha 164 kwa njia ya udanganyifu, mateso ya kimwili na kiakili ni baadhi tu ya mifano michache ya ukandamizaji wa kawaida wa serikali hii. Kwa kuiga CIA ya Amerika, serikali hii dhalimu pia imeweka mifano kwa kutia shoti za umeme kwenye rumande na kutumia njia ovu za mateso, kama vile kuzamisha kwenye maji. Enyi Waislamu, katika kuangamiza ulinganizi wa Uislamu, serikali ya Hasina inafuata nyayo za Abu Lahab ambaye hakuacha fursa yoyote impite kuzuia kuanzishwa kwa dola ya Kiislamu na Mtume (saw), iliyomfanya astahiki kuangamizwa na Mwenyezi Mungu Al-Qawwi Al-Aziz:

[تَبَّتْ يَدَا أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ]

“Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia!” [Surah Al-Masad: 1].

Enyi Waislamu, mnajua kwamba Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa ambacho mfumo wake ni Uislamu na mbinu zake zimetabanniwa kwa mujibu wa Quran na Sunnah;

[لَقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِمَنْ كَانَ يَرْجُو اللَّهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّهَ كَثِيراً]

“Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana.” [Al-Ahzab: 21]. Hizb ut Tahrir inajenga ufahamu mkubwa na rai jumla kuegemea upande wa Khilafah kupitia amali zake za kifikra na kisiasa kama vile vipeperushi-mabango, maandamano-mikutano, mikusanyiko, semina-makongamano, mawasiliano ya umma katika mitandao ya kijamii, nk. Hizb ut Tahrir haiamini kubadilisha utawala kwa njia ya ghasia za kisiasa au mapambano ya kisilaha, lakini badala yake inatoa wito kwa maafisa wenye ikhlasi wa jeshi kuondoa utawala unaotawala na kutoa msaada wa kimada (nusrah) kwa Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah.

Kama mnavyofahamu, Hizb ut Tahrir imekuwa ikiwasilisha kwa watu dosari za mfumo wa kisekula na ukandamizaji wa mfumo wa Kibepari, na kufichua uingiliaji wa wazi wa Wakoloni wa makafiri wa Amerika na Uingereza na washirika wao wa kieneo katika siasa na uchumi wa nchi na mipango na njama zao ovu dhidi ya mamlaka na nguvu za kijeshi za nchi, na imekuwa akipinga ufisadi na utawala mbaya wa watawala wa kisekula. Munaweza kukumbuka kwamba Hizb ut Tahrir ilipinga makubaliano mbalimbali ya kijeshi, na pia dhidi ya mikataba ya kutoa njia hadi India, na pia ilifichua njama ya India ya kudhoofisha jeshi katika mauaji ya Pilkhana. Vile vile imepinga mazoezi mbalimbali ya kijeshi ya pamoja na Marekani, ikiwemo ‘Tiger Shark’ na makubaliano kama vile TICFA, ACSA, ambayo yalifanywa ili kuanzisha utawala wao juu ya rasilimali zetu za kimkakati na kijeshi. Hizb ut Tahrir imeeleza jinsi mfumo wa Khilafah utakavyoibuka kuwa Dola inayojitegemea na inayoongoza dhidi ya mfumo dhalimu wa Kibepari uliolazimishwa na Wakoloni wa makafiri. Imeeleza kwa kina jinsi Uislamu unavyohakikisha mahitaji msingi ya raia wote, bila kujali dini au rangi, na kuhakikisha ugavi wa haki wa mali miongoni mwa watu, bila kuilimbikiza mikononi mwa wachache. Kupitia makongamano mengi ya mtandaoni, Hizb ut Tahrir iliwasilisha kwa wananchi rasimu ya katiba ya Dola ya Khilafah, muundo wa idara wa Dola ya Khilafah, pamoja na sera zinazohusu uchumi, mahusiano ya mwanamume na mwanamke (mfumo wa kijamii) na sera ya kigeni. Hii imesababisha uungaji mkono mkubwa wa Khilafah katika nyanja zote za maisha.

Enyi Waislamu, kwa nini inachukuliwa kuwa ni uhalifu kudai utawala wa Uislamu, yaani mfumo wa Khilafah, katika ardhi za Kiislamu? Ambapo, Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala anasema:

[إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ]

“Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu.”?! [Surah Yusuf: 40]. Kwa nini amali zisizo za vurugu na za kifikra za kusimamisha Khilafah zinalinganishwa na misimamo mikali na uanamgambo? Kwa hakika, kanuni mojawapo ya wakoloni wa makafiri ni kuzuia mwamko wa Uislamu kwa kisingizio cha ugaidi au uanamgambo, ambao katika utekelezaji wake utawala kibaraka unashirikiana. Serikali ya Hasina inadai kwamba Dola za Kikafiri-Kishirikina zinatoa usaidizi wao kwa serikali yake kwa ajili ya mafanikio yake katika "Vita dhidi ya Ugaidi" ambavyo kwa hakika ni "Vita dhidi ya Uislamu". Enyi Waislamu, tunawaomba museme waziwazi dhidi ya vita hivi vinavyoendelea dhidi ya Dini yetu, muipeleke mbele zaidi kazi ya kusimamisha Khilafah na kupinga ukandamizaji wa serikali dhidi ya wale wanaotaka kusimamishwa tena kwa Khilafah.

Enyi Waandishi wa Habari Wenye Ikhlasi! Tumeshangazwa kuona kwamba baadhi ya vyombo vya habari vinaishutumu Hizb ut Tahrir kuwa ni muundo wa wanamgambo au wenye msimamo mkali, na matoleo yaliyochapishwa na Hizb ut Tahrir na machapisho kuhusu katiba, muundo wa idara, uchumi na sera ya kigeni za Dola ya Khilafah kuwa ni "misimamo mikali". Je, hizi porojo na propaganda hazitilii shaka uandishi wenu wa habari? Kwa kuwa Hizb ut Tahrir imejengeka vyema katika jamii inayosifika kama chama cha kisiasa na kinachojulikana sana na tabaka zote za watu, je, hizi kashfa na propaganda hazichafui uaminifu na sifa yenu? Kumbukeni, waongo wamelaaniwa na Mwenyezi Mungu (swt).

[لَعْنَتَ اللَّهِ عَلَى الْكَاذِبِينَ]

“… laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake ikiwa ni miongoni mwa waongo.” [Surah An-Noor: 7]. Ni jukumu lenu kuthibitisha Habari mmnayopewa na serikali hii dhalimu kuhusu Hizb ut Tahrir:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَنْ تُصِيبُوا قَوْماً بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَى مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ]

“Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda…” [Surah Hujurat: 6]. Wito wetu kwenu ni kukataa uvumi wa kirongo kuhusu Hizb ut Tahrir na mujitokeze kusimamisha haki na uadilifu.

Enyi Mahakimu! Kumbukeni kwamba Mwenyezi Mungu Subhanahu Wa Taala ndiye Hakimu wa mahakimu wote, na siku moja mutalazimika kusimama kizimbani kwa ajili ya Hukumu yake. Yeye (swt) amekuamrisheni msihukumu kwa sheria yoyote isiyokuwa ile aliyoiteremsha Yeye (swt), na lazima msimamishe uadilifu wakati wa kuhukumu.

[وَإِذَا حَكَمْتُمْ بَيْنَ النَّاسِ أَنْ تَحْكُمُوا بِالْعَدْلِ]

“Na mnapo hukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu...” [Surah An-Nisa: 58]. Ni wazi kama ulivyo mchana mweupe kwenu kwamba ile inayoitwa sheria ya kupambana na ugaidi iliyotungwa na serikali kibaraka katika vita dhidi ya Uislamu imetolewa chini ya maelekezo ya Marekani na washirika wake ili kuwakandamiza Waislamu. Sheria hii haina uhusiano wowote na haki. Si haki kuwahukumu viongozi na wanaharakati wa Hizb ut Tahrir chini ya sheria hii mashuhuri. Zaidi ya hayo, ni dhulma kubwa kuwakabidhi kwa vyombo vya usalama ili wateswe kwa kukariri kuwaweka rumande, au kuwaweka jela kwa miezi kadhaa kwa kuwanyima dhamana mara kwa mara. Mtume (saw) amesema:

«الْقُضَاةُ ثَلَاثَةٌ وَاحِدٌ فِي الْجَنَّةِ وَاثْنَانِ فِي النَّارِ فَأَمَّا الَّذِي فِي الْجَنَّةِ فَرَجُلٌ عَرَفَ الْحَقَّ فَقَضَى بِهِ وَرَجُلٌ عَرَفَ الْحَقَّ فَجَارَ فِي الْحُكْمِ فَهُوَ فِي النَّارِ وَرَجُلٌ قَضَى لِلنَّاسِ عَلَى جَهْلٍ فَهُوَ فِي النَّارِ»

Mahakimu ni aina tatu, mmoja atakwenda Peponi na wawili watakwenda Motoni. Ima yule aliyeko Peponi ni  mtu aliyeijua haki na akahukumu kwayo. Ama mtu aliyeijua haki kisha akahukumu kwa jeuri atakuwa Motoni na mtu aliyewahukumu watu kwa ujinga atakuwa Motoni. [Imesimuliwa na Abu Daud]. Matakwa na matarajio yetu kutoka kwenu ni kwamba mutafanya maamuzi sahihi. Enyi Mahakimu, mnapotoa hukumu yenu, kuweni watiifu kwa Mwenyezi Mungu (swt), watendeeni uadilifu wale wanaobeba ulinganizi wa Uislamu na wanaharakati wa kisiasa wa Khilafah, na waacheni huru kwa kupuuza maagizo ya serikali ya kuwaweka kizuizini kwa dhulma.

Enyi Wanachama wa Utekeleza Sheria! RasulAllah (saw) amesema, «لَا طَاعَةَ لِمَخْلُوقٍ فِي مَعْصِيَةِ الْخَالِقِ» Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba. [Imesimuliwa na Ahmad], matakwa ya Uislamu kwenu ni kutotii amri ya serikali ya kuwahangaisha, kuwakamata, kuwateka nyara, kuwaweka kizuizini na kuwatesa wanaharakati wa kisiasa wa Uislamu na Khilafah. Wengi wenu mnadai kwamba mnawajibika kutii amri za serikali kwa sababu ya kazi yenu lakini kisingizio hiki hakina thamani yoyote kwa Mwenyezi Mungu (swt) kwa sababu kutii amri za dhulma za serikali ni haramu. Tunakukumbusheni kwamba Mwenyezi Mungu (swt) atakuhisabuni kwa matendo yenu; Yeye (swt) amesema:

[إِنَّ الَّذِينَ فَتَنُوا الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَتُوبُوا فَلَهُمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمْ عَذَابُ الْحَرِيقِ]

“Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua.” [Surah Al-Buruj: 10] na RasulAllah (saw) amesema, «لَا يَحِلُّ لِمُسْلِمٍ أَنْ يُرَوِّعَ مُسْلِماً» “Si halali kwa Muislamu kumtishia Muislamu mwengine.” [Kanz al-Ummal]. Tunazidi kuwambusha kwamba msipoacha, hamtakuwa tu miongoni mwa wenye hasara kesho Akhera, bali pia mtapata hasara kubwa hapa duniani baada ya kuregea Khilafah iliyo karibu sana, insha’Allah. Wahusika watafikishwa mahakamani kwa uhali wote uliotendwa dhidi ya watoto wenye ikhlasi wa Kiislamu na Ummah.

Enyi Maafisa Wenye Ikhlasi katika Jeshi! Mtume (saw) amesema, «مَنْ رَأَى مِنْكُمْ مُنْكَراً فَلْيُغَيِّرْهُ بِيَدِهِ فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِلِسَانِهِ فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِقَلْبِهِ وَذَلِكَ أَضْعَفُ الْإِيمَانِ» Yeyote anayeuona uovu, basi na aubadilishe kwa mkono wake; na akiwa hawezi basi kwa ulimi wake; na akiwa hawezi basi (achukie) kwa moyo wake – na hiyo ni Imani dhaifu Zaidi.” [Imesimuliwa na Muslim]. Kwa mujibu wa Hadith hii iliyosimuliwa na Mtume (saw), munaangukia katika kundi la kwanza kwa sababu muna nguvu za kijeshi mikononi mwenu ambazo kwazo munaweza kuondoa dhulma yoyote. Kwa hiyo, ni wajibu wenu kuchukua hatua ya dhati ya kuondoa dhulma za serikali kwa walinganizi wa Khilafah. Waagizeni wenzenu katika upande wa idara, waache kuwadhulumu wale wanaolingania Khilafah. Hatimaye, kwa ajili ya Uislamu na Waislamu, iondoeni serikali hii dhalimu kutoka madarakani na mukabidhi mamlaka (toeni nusrah) kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha tena Khilafah.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ]

“Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kuweni pamoja na wakweli.” [Surah At-Taubah:119]

H. 18 Dhu al-Hijjah 1444
M. : Jumapili, 17 Julai 2022

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Bangladesh

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu