Ijumaa, 10 Shawwal 1445 | 2024/04/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hotuba katika Msikiti wa Al-Aqsa Uliobarikiwa
Ummah wa Kiislamu na Wanadamu Wote Wanahitaji Pakubwa Macheo ya Dola ya Khilafah
(Imetafsiriwa)

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu (swt) aliyesema:

[إِنَّا لَنَنْصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ]

“Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi” [Ghafir: 51].

Na rehema na amani zimshukie yule ambaye Mwenyezi Mungu amemtuma katika safari ya Israa kutoka Msikiti wa Al-Haram hadi Al-Aqsa iliyobarikiwa.

Enyi Waislamu... Enyi watu wetu katika viunga vya Msikiti wa Al-Aqsa na Ardhi Iliyobarikiwa... Enyi Ummah wetu kipenzi katika sehemu zote za dunia:

Tunasimama mbele yenu leo ​​katika Masra ya Mtume wenu Mtukufu, katika kumbukumbu ya mwaka wa 101 wa kuvunjwa kwa Dola ya Kiislamu ya Khilafah. Tunasimama kwa mara nyingine tena huku kila mmoja akikabiliwa na maafa yaliyoupata Umma wa Kiislamu kwa sababu ya kuvunjwa Khilafah... janga lililowapata watu wa Palestina hasa huku wakiendelea kugeuza makaa ya moto kutokana na athari za kukosekana kwa Khalifa, ngao ambayo Waislamu hupigana nyuma yake, na hujihami kwayo. Wakafukuzwa katika ardhi yao baada ya kunyakuliwa. Tunawatazama wakiua asubuhi na jioni kwenye televisheni, wakitishiwa na walowezi katika vitongoji na miji, wanaochafua Msikiti wa Al-Aqsa ili kutekeleza ibada zao humo. Watu wa Ghaza bado wanateseka chini ya mzingiro mkali wa dhulma, yote haya yakiwa kwa ushirikiano wa watawala wa Kiislamu, ambao wanakimbia kuelekea kwenye uratibu, usawazishaji mahusiano na usaliti kwa namna ya wazi bila ya kumuogopa Mwenyezi Mungu au kuwaonea haya waja Wake.

Enyi Waislamu: Ummah mzima unaishi katika maafa ya kuvunjwa Khilafah... Unaishi katika maafa hayo huko Ash-Sham, ambapo watoto na wanawake wake waliuawa mbele ya wanaume wake, miji yake ikavunjwa na watu wake kuwa wakimbizi. Watu wa Iraq na Afghanistan wanaishi ndani yake, wanateseka kutokana na matokeo ya vita vilivyopiganwa dhidi yao na wakoloni, ambao waliteketeza kila kitu na kuharibu maeneo ya mijini katika vita vilivyotangazwa dhidi ya Umma wa Kiislamu. Athari za kuvunjwa kwa Khilafah ziliwaathiri watoto wa Kiislamu waliotawanywa kote ulimwenguni kutokana na dhulma na ukandamizaji. Watoto wa Kiislamu wanatekwa nyara kutoka kwa familia zao nchini Uswidi na kwingineko ili kuwekwa pamoja na familia za Kikristo zitakazowatenga na dini yao!

Waabudu ng'ombe walitushambulia, na wakavua hijab kutoka kwa vichwa vya wanawake wetu, ambao ni wanyonge na wasio na msaada na hakuna wa kukemea hili! China inaendelea kuwaua Waislamu wa Uyghur, kuwakandamiza na kuwazuia kufanya ibada, kama ilivyo kwa Myanmar.

Enyi Waislamu: Tawala za vibaraka alizoziunda mkoloni katika nchi yetu baada ya kuvunjwa Khilafah yetu na kugawanywa kwa Ardhi yetu ndio vinara katika vita vyake dhidi ya Umma wa Kiislamu. Wanakandamiza watu, wanarusha makombora vichwani mwa watu, wanawatupa wanazuoni wanyofu gerezani, na wanawasilisha utajiri wa nchi kwenye sahani ya fedha kwa wakoloni wa Magharibi. Wanapigana vita dhidi ya Dini, thaqafa na imani ya Ummah katika vyombo vya habari na mitaala ya kielimu, wakiondoa kile kilichosalia cha harufu nzuri ya Uislamu kwenye mitaala na kutia saini mikataba ya kimataifa kama vile CEDAW iliyolaaniwa ili kuyatekeleza kwa Waislamu ili kuwatenganisha zaidi na Dini yao.

Hii ndiyo hali yenu baada ya miaka mia moja na moja baada ya kuvunjwa Khilafah mithili ya mayatima kwenye karamu za waovu, damu yenu, heshima yenu, mali yenu na matukufu yenu vinajuzishwa kukiukwa.

Enyi Watu: Leo tumesimama katika Msikiti wa Al-Aqsa na dunia nzima inateseka kwa sababu ya kutokuwepo Uislamu. Kwa sababu ya kukosekana kwa Khilafah kama dola ya kimataifa, watu walikoloniwa na utajiri wa nchi dhaifu ukaporwa, na dunia nzima imekuwa mateka wa maamuzi ya kihalifu ya Marekani na Urusi. Kwa sababu ya kutokuwepo Khilafah kama dola ya kimataifa, ulimwengu ulishuhudia vita viwili angamivu vya dunia, na hivi sasa wako ukingoni mwa vita vya tatu vya dunia, na ikiwa Ummah wa Kiislamu hautachukua hatua ya kuokoa wanadamu, ulimwengu huu utabaki kutawaliwa na matamanio ya marais wajinga na mizozo haribifu ya kimataifa.

Enyi Watu: Kutoka Msikiti wa Al-Aqsa, tunauhutubia Ummah wa Kiislamu hasa na watu wa dunia nzima kwa jumla, na tunawaambia Waislamu: Nyinyi ndio mnaoweza kuunusuru ulimwengu na wanadamu kutokana na dhulma ya mabepari na uhalifu wao. Nyinyi ndio wabebaji wa rehma na uongofu. Nyinyi ni mashahidi wa Mwenyezi Mungu kwa watu, basi je, mtatikisa vumbi kutoka mabegani mwenu na kuinuka pamoja utukufu wa Uislamu?

Tunawaambia majeshi ya Kiislamu: Nyinyi ni nguvu na ulinzi wa Waislamu, na kwa mikono yenu ufunguzi na ushindi hutokea. Mpaka lini mtabaki kuwa mateka wa tawala hizi vibaraka, zilizoua ndani yenu msukumo wa Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt)? Ni lini mtaghadhibika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) na kuwapindua wasaliti hawa wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake (saw)? Je! wakati haujawadia kwa nyoyo zenu kujisalimisha kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na yale yaliyoteremshwa kwa haki, na kumnusuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kutoa Nusra kwa Hizb ut-Tahrir na Amiri wake, na kutoa ahadi ya utiifu (bay'ah) kwake mithili ahadi ya utiifu ya Answar, ambayo kwayo mnasimamisha Dini na kuibeba kama ujumbe wa kheri na mwongozo kwa walimwengu?

Ama kwa watu wa dunia tunawaambia: Urasilimali umevipofusha vyama na marais wenu, na moja ya uhalifu wao mkubwa ni kuchochea uadui dhidi ya Uislamu, licha ya kuwa ni rehema itakayokuokoeni, na kwa sababu ya kiburi chao na ubinafsi wao, hatma yenu imetishiwa na kutoweka. Yanayotokea Ukraine leo ni onyo ambalo linakutishieni endapo hamtawakomesha wahalifu hawa. Mabepari na viongozi wa nchi kuu hawapatii uzito isipokuwa kwa maslahi yao, nao ni uovu unaowasibu wanadamu. Na msipokimbilia kurekebisha mambo yenu, mtaathirika na zaidi ya yale yaliyokupateni katika vita viwili vya dunia.

Enyi Watu: Dunia nzima inahitaji nguvu mpya ya kimataifa ili kuupindua mfumo huu wa kihalifu, inahitaji Uislamu na Dola ya Khilafah, ili kuinusuru na jinai za nchi kubwa - Marekani, Urusi, Uingereza, Ufaransa na China - kwani jinai zao dhidi wanadamu ni za aibu. Dola ya Khilafah ni mwokozi wa wanadamu na itabadilisha mahusiano ya kimataifa na kuyaunda tena, ni kimbilio la wanyonge katika ulimwengu mzima.

Ni Dola kwa njia ya Utume, inatawala kwa sheria ya Mwingi wa Rehma, ambamo uadilifu huthibitika na wema huenea, wanaodhulumiwa wanatendewa uadilifu, dhalimu anahisabiwa, na anasukumwa juu ya haki.

Ni Khilafah kwa njia ya Utume ambapo watu wote humiminika kwake, kwa sababu ndio wokovu wao, ngome yao, ngao yao. Twamuomba Mwenyezi Mungu (swt) ayafanye macheo yake yawe karibu, ni wakati sasa wa Dini yetu kudhihiri na bendera ya Mtume wetu kunyanyuliwa. Huu ndio wito wetu kwenu, ndani yake kuna uhai na wokovu wenu.

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa” [Al-Anfal: 24]

Ewe Mwenyezi Mungu, tunakuomba Khilafah Rashida kwa njia ya Utume ambayo kwayo tunamridhisha Mola wetu Mlezi na kuregesha utukufu na heshima yetu, kwayo tunaikomboa ardhi yetu na njia ya Mtume wetu.

Ewe Mwenyezi Mungu zifungue nyoyo za watu wenye nguvu na ulinzi ili wainusuru Dini yako na kuisimamisha kama Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Ewe Mwenyezi Mungu, inyanyue bendera ya Uislamu ipepee juu ya kuta za Bayt Al-Maqdis, na uzifanye sauti za Takbira za majeshi ya Khilafah zisikike kwenye pembe zake kwa Rehma Zako, Neema Zako, na Fadhili Zako Adhimu. Na rehma na amani zimshukie yule aliye tumwa kama rehma kwa watu, na sifa njema ni za Mola wa walimwengu wote.

H. 1 Sha'aban 1443
M. : Ijumaa, 04 Machi 2022

Hizb-ut-Tahrir
Ardhi ya Baraka-Palestina

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu