Jumatatu, 28 Sha'aban 1444 | 2023/03/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Serikali "Imevalia" Janga la Ugonjwa wa Korona na Kutekeleza Amri ya Kutotoka nje ili Ipitishe Maagizo ya Shirika la Fedha la Kimataifa na Watu Kuponda Masikini waliobakia

(Imetafsiriwa)

Kamati Kuu ya Dharura za Kiafya imeamua kutekeleza amri ya kutotoka nje katika jimbo la Khartoum, kuanzia Jumamosi ijayo kwa mda wa wiki tatu. Maamuzi haya yanajiri kinyume na taaswira ya Wizara ya Afya iliyo sajili mnamo Jumatatu, 13/4/2020, visa kumi vipya vya virusi vya Korona, kufikisha idadi ya maambukizi hadi 29. Uamuzi umekuja kinyume na taaswira kwa tofauti mbili: kuenea kwa maandamano dhidi ya serikali ya mpito na ongezeko la hali ngumu ya kiuchumi, kunako wakilishwa na uhaba wa mafuta; gesi, petrol na upungufu wa mkate hata baada ya serikali kuongeza bei maradufu, na zaidi ya ongezeko la bei za bidhaa ni kuanguka kwa pauni dhidi ya sarafu zingine.

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan tunataka kubainisha ukeli ufuatao:

Kwanza: Serikali imecheza dori kubwa katika kusambaza Janga hili nchini, kwa faida yake binafsi. Kama kuanzia mwanzo wa ugonjwa huu duniani, ingekaza mkono wake katika mipaka ya nchi, kuwatenga wote wanao fika kwa wiki mbili katika vituo maalumu kisha kuwaachilia walio wazima, na kutibu walio athirika, janga hili halingeingia nchini, lakini haikufanya hivyo! Badala yake waliwaruhusu walio athirika kuingia, na ugonjwa ulipo onekana unasambaa, ikaanza kuongea kutowezeka kwake kuwafikia asilimia 40 ya wale waliovuka mipaka, na hivyo ugonjwa umefikia hatua ya maambukizi ya kijamii!!

Pili: Matibabu ya janga la virusi vya Korona yameegemezwa katika mbinu ya serikali iliyo ng'atuka; nayo ni kuchukua masuluhisho kutoka kwa mfumo wa kirasilimali, na mfumo wa kimaisha wa Wamagharibi, kwa njia ya matumizi na kuwaiga, kwa kuchua wazo la kinga kwa wengi kuwa ndio msingi, kuchanganya wagonjwa na wazima na kutatiza maisha ya walio wazima bila kuangalia mambo yao, bila kuwapatia hali nzuri ya maisha. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema; «لاَ تُورِدُوا المُمْرِضَ عَلَى المُصِحِّ» “Msiwachanganye walio wagonjwa na wazima pamoja”.

Yote haya yanaashiria kufeli na uzembe wa viongozi katika kushughulikia mambo ya watu.

Tatu: Suluhu ya sawa kwa janga hili ni kuwa Uislamu umeleta; kwamba serikali ifuate ugonjwa kutoka uliko anzia, na ifanye kazi ya kuzuilia kusambaa kwake; na walio wazima waendelee katika maeneo mengine kufanya kazi na kuzalisha. Katika mapokezi ya Osama bin Zaid kutoka Mtume (saw) amesema:

«إِذَا سَمِعْتُمْ بِالطَّاعُونِ بِأَرْضٍ فَلَا تَدْخُلُوهَا وَإِذَا وَقَعَ بِأَرْضٍ وَأَنْتُمْ بِهَا فَلَا تَخْرُجُوا مِنْهَا»

Mtakapo sikia mkurupuko wa tauni katika ardhi fulani, msiingie humo; na mkurupuko huo unapotokea katika ardhi mliopo basi msitoke humo.”

Karantini mfano huu ni katika taifa ambalo liko mbele ya dola zote. Serikali ya Kiislamu lazima izuilie ugonjwa tatika sehemu yake, na wakaazi wake na wengine wasiingie katika hilo eneo. Serikali inabeba majukumu yake kwa sababu ni serikali inayojali (mambo ya watu wake) na inatekeleza amana.

Nne: Serikali yataka "kuvalia" janga la virusi vya Korona ili kupitisha mradi wa jinai wa kikoloni; kutabikisha maagizo ya Shirika la Fedha la Kimataifa, ambayo inaungwa mkono na viongozi wengi wa Qahta, kupitia kuongeza bei ya mafuta, mkate na stima, ambayo imeleta janga la mfumko wa bei,ambalo watu nchini hawawezi kuuhimili na wao ndio wanaoteseka kwa bei ya bidhaa iliyo ongezeka maradufu wakati huu wa serikali ya mpito! Pia bei za bidha mnamo Aprili zilikuwa kama ifuatavyo: [kilo moja ya sukari kwa pauni 21, kilo moja ya unga kwa pauni 35, lita moja ya mafuta kwa pauni 80 na bakuli la ngano kwa pauni 360] huku hivi leo bei za bidhaa hizi zikiwa ni: [kilo moja ya sukari kwa pauni 90, kilo moja ya unga kwa pauni 95, lita moja ya mafuta kwa pauni 190 na bakuli moja la ngano kwa pauni 1100]!

Tano: Kile kinacho ashiria kuwa serikali inataka kutumia janga hili kuondoa wanachokiita  bidhaa za ruzuku ni kwamba, ilijipanga tayari kwa kuzuka visa hivi kumi vipya kwa kutoa amri nambari (1) ya mwaka 2020 siku ya Jumapili 12/04/2020, na maamuzi haya yakijumuisha adhabu pamoja na faini ya pesa ya kati ya pauni elfu tano na elfu ishirini kwa yule atakaye kiuka marufuku hii! Serikali pia inaongelea kuhusu kurekebisha bajeti ili kujumuisha kuondolewa kwa ruzuku!

Sita: Waziri wa habari ametaja kwamba amri ya kutotoka nje itasimamishwa kwa saa moja, ili kuwezesha watu kununua vitu wanavyo hitaji, bila shaka anaongelea kuhusu wale wanao weza kumudu kununua, lakini familia nyingi zinamtegemea mchumaji mmoja na huyo mchumaji anapata kipato cha siku hadi siku. Hivyo, ikiwa siku moja tu mchumaji huyo hatafanya kazi, basi hii inamaanisha hakuna pesa za kununua bidhaa msingi, hivyo vipi serikali inataka kuwafunga watu?! Haiwalisha, wala haiwaruhusu kufanya biashara zao! Hili limeharamishwa kwa mujibu wa na kauli ya Mtume (saw)

«عُذِّبَتِ امْرَأَةٌ فِي هِرَّةٍ سَجَنَتْهَا حَتَّى مَاتَتْ فَدَخَلَتْ فِيهَا النَّارَ، لَا هِيَ أَطْعَمَتْهَا وَسَقَتْهَا، إِذْ حَبَسَتْهَا، وَلَا هِيَ تَرَكَتْهَا تَأْكُلُ مِنْ خَشَاشِ الْأَرْضِ»

“Mwanamke aliadhibiwa kwa sababu ya paka aliyemfungia mpaka akafa, basi kwa hilo akaingia Motoni, hakumpa chakula wala maji pindi alipomfungia, wala hakumwachilia akale chakula kilicho dondoka ardhini”

Na kwa maneno yake (saw) «الْإِمَامُ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» “Kiongozi (Imam) ni mchungaji na ataulizwa kuhusu raia wake.”

Hakuna faraja katika uongo wa serikali; kusema imejipanga kupeana pensheni kwa maskini wakati wa marufuku hii kamili ya kutotoka nje! Mpaka kufikia nukta hii, haija tatua tatizo la wale walio athirika na marufuku ya kusafiri kuanzia madereva wa magari ya usafiri na wafanyikazi katika sekta hii!

Enyi Watu Wetu Wa Sudan: Al-Haq (swt) anasema:

(أَوَلَا يَرَوْنَ أَنَّهُمْ يُفْتَنُونَ فِي كُلِّ عَامٍ مَّرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ لَا يَتُوبُونَ وَلَا هُمْ يَذَّكَّرُونَ)

 “Je Hawaoni ya kwamba wanatiwa mtihani kila mwaka mara moja au mara mbili? Kisha hawatubu, wala hawakumbuki” [At-Tawba: 126].

Ni bora kwetu kutubia kwa Mwenyezi Mungu na tumkumbuke. Tutubie dhambi zetu za kupuuzilia jukumu letu kubwa; la kurudisha mfumo wa maisha wa Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na tukumbuke na kujifunze kutoka katika miaka 99 ya kutawaliwa na yasiyo kuwa Uislamu,tangu Khilafah ilipovunjwa. Na tumerithi nini kutoka kwa mtawala huyu dhalimu isipokuwa idhilali, umasikini, na unyonge. Na tunawakaribisha katika kazi ya kusimamisha Khilafah kabla hatujafikia miaka 100,hivyo muonesheni Mwenyezi Mungu kheri iliyomo ndani ya nafsi zenu, na kunjeni mashati yenu kwa kazi adhimu.(لِمِثْلِ هَذَا فَلْيَعْمَلِ الْعَامِلُونَ) “Kwa mfano wa haya na watende watendao.”

#Covid19    #Korona    كورونا#

H. 21 Sha'aban 1441
M. : Jumanne, 14 Aprili 2020

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu