Jumamosi, 21 Sha'aban 1445 | 2024/03/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  20 Jumada II 1440 Na: 1440/019
M.  Jumatatu, 25 Februari 2019

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mohammad Bin Salman Anawakabidhi Waislamu wa Uyghur kwa Madhalimu Wao

«إِنَّ شَرَّ الرِّعَاءِ الْحُطَمَةُ»
“Watawala waovu zaidi ni wale wanaoamiliana na raia wao kwa ukali."
(Imetafsiriwa)

Mohammad Bin Salman anatafuta njia kadha wa kadha za kubakia mamlakani kwa gharama yoyote hata ikiwa inahitaji kumkhini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na waumini. Baada ya kuanikwa hadharani juu ya mauwaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi na kukua kwa idadi ya miito ya kuhisabiwa kwake na kuondolewa afisini, alichukua hatua kadhaa ili kuthibitisha utiifu wake kwa wakoloni Wamagharibi. Ndani ya Saudi Arabia, alifungua wazi mlango kwa kampeni kabambe ya kueneza uchafu na uovu, chini ya pazia ya kuimarisha utalii na burudani, na kuwaleta waimbaji na wasanii wa uchafu miongoni mwa Waarabu na wasiokuwa Waarabu ili kufanya matamasha machafu, na wakati huo huo, kuwaweka kizuizini mamia, bali maelfu ya Waislamu katika magereza.

Bin Salman anafanya bidii kuinua sura yake mbele ya rai jumla ya kimataifa, hii ni kupitia kutia saini mikataba na nchi nyingi katika hatua ya kueneza ujumbe kuwa kazi inaendelea ili kunali mradi unaoitwa “Ruwaza ya 2030”. Baada ya mauwaji ya Khashoggi kuchafua sura ya Kongamano la Saudi la Uwekezaji (mnamo 23/10/2018, lililopewa lakabu ya mji wa Davos Jangwani, lilipoteza nuru yake kutokana na kujiondoa kwa wageni wengi mashuhuri wa kimataifa na wafanyi biashara), alikwenda katika ziara ya Pakistan, India, China na Indonesia, iliyo shuhudiwa kutiwa saini kwa mikataba mingi yenye thamani ya mabilioni ya dolari.    

Katika ziara yake nchini China, Bin Salman hakutia tu saini mikataba bali alizipa mamlaka za China idhini katika kampeni zao za kinyama dhidi ya Waislamu wa Uyghur eneo la Turkestan Mashariki (Xinjiang). Gazeti la The New York Times lilinukuu stesheni ya runinga ya China (CCTV) ikisema kuwa Bin Salman alisema wakati wa mkutano wake pamoja na Raisi wa China Xi Jinping: “China ina haki ya kuchukua hatua dhidi ya ugaidi na misimamo mikali ili kulinda usalama wa taifa.”   

Huku vyombo vya habari vya kimataifa vikishutumu msako wa China kwa Waislamu wa Turkestan Mashariki, taarifa ya Ibn Salman ili halalisha uovu huu wa kinyama, na kutoa ushahidi dhidi yake binafsi kuwa yeye ni miongoni mwa Masafihi (Sufaha) ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ameonya kuwahusu. Imehadithiwa kuwa Jaber bin Abdullah alisema: Mtume (saw) alimwambia Ka’b ibn Ajra:

«أَعَاذَكَ اللهُ مِنْ إِمَارَةِ السُّفَهَاءِ». قال: وَمَا إِمَارَةُ السُّفَهَاءِ؟ قال: «أُمَرَاءُ يَكُونُونَ بَعْدِي، لَا يَقْتَدُونَ بِهَدْيِي، وَلَا يَسْتَنُّونَ بِسُنَّتِي، فَمَنْ صَدَّقَهُمْ بِكَذِبِهِمْ، وَأَعَانَهُمْ عَلَى ظُلْمِهِمْ، فَأُولَئِكَ لَيْسُوا مِنِّي وَلَسْتُ مِنْهُمْ، وَلَا يَرِدُوا عَلَيَّ حَوْضِي، وَمَنْ لَمْ يُصَدِّقْهُمْ بِكَذِبِهِمْ، وَلَمْ يُعِنْهُمْ عَلَى ظُلْمِهِمْ،    فَأُولَئِكَ مِنِّي وَأَنَا مِنْهُمْ، وَسَيَرِدُوا عَلَيَّ حَوْضِي...»

Mwnyezi Mungu akulinde kutokana na uongozi wa masafihi” akasema: ni upi uongozi wa masafihi? Akasema: "Ni viongozi watakao kuwa baada yangu, hawafuati uongofu wangu, na hawashikamani na Sunnah zangu, basi yeyote atakaye wasadikisha urongo wao, na kuwasaidia katika dhuluma zao, basi hao si katika mimi na mimi si katika wao, na hawatakuja katika birika langu (Hawdh). Na yeyote ambaye hata wasadikisha urongo wao, na wala hata wasaidia katika dhuluma zao, basi hao ni katika mimi na mimi ni katika wao, na watakuja katika birika langu …”

Enyi Watu wetu katika Ardhi ya Wahyi:

Ufafanuzi katika Hadith hii unamlekea mtu huyu safihi:

: «إِنَّ شَرَّ الرِّعَاءِ (أي الأمراء) الْحُطَمَةُ»

“Watawala waovu zaidi ni wale wanaoamiliana na raia wao kwa ukali."

Ni dhahiri kwenu sasa ambapo munamuona Bin Salman, kwa idhini kutoka kwa babake, aliyemteua juu yenu na mshirika wake katika uhalifu, akiharakisha katika kuonyesha utiifu wake kwa Wamagharibi, na kutumia utajiri wa Ummah ili kuwaridhisha viongozi wa kikafiri wanao wadhulumu na kuwatesa ndugu zenu katika Dini. Hamupaswi kukaa kimya kuhusu uhalifu wake na uvunjaji moyo wake dhidi ya ndugu zenu eneo la Turkestan (Xinjiang). Bali Uislamu una wawajibisha kumpinga na kufanya kazi kumng’oa, na kuitwahirisha ardhi hii ya wahyi kutokana na najisi yake na magenge yake. Shari'ah ina wawajibisha kuwasaidia ndugu zenu katika Dini eneo la Turkestan Mashariki kama vile wale walioko Palestina, Kashmir na biladi nyenginezo za Waislamu. Tunawakumbusha maneno yake (saw):

«سَيِّدُ الشُّهَدَاءِ حَمْزَةُ بْنُ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، وَرَجُلٌ قَامَ إِلَى إِمَامٍ جَائِرٍ فَأَمَرَهُ وَنَهَاهُ فَقَتَلَهُ»

“Bwana wa mashahidi wote ni Hamza Bin Abdul Muttwalib, na mtu anaye simama mbele ya kiongozi jeuri akamuamrisha (mema) na akamkataza (maovu) kisha akamuuwa kwa hilo.”

Kwa hivyo tekelezeni wajibu wenu na amana zenu katika Dini hii, utukufu wenu ni kwa kuwa Ummah bora ulioletwa kwa wanadamu unao walingania watu mema na kuwakataza maovu, katika hili ndio mafanikio yenu na izza yenu hapa duniani na kesho Akhera.

Dkt. Osman Bakhach
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu