Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
| H. 28 Jumada II 1447 | Na: H 1447 / 037 |
| M. Ijumaa, 19 Disemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Watawala wa Waislamu Wameshikana Mkono kwa Mkono na Marekani na Mayahudi Kupitisha Mipango Yao, Na kwa Kauli na Shutma Tupu Pamoja na Waislamu
(Imetafsiriwa)
Umbile la Kiyahudi linaendelea kutekeleza jinai zake dhidi ya Gaza, Ukingo wa Magharibi, Lebanon na Syria; kumuua limtakaye, kupiga mabomu popote lipendapo, kubomoa nyumba na vituo, kujenga makaazi, na kuwaandama watu katika nyumba na ardhi zao, huku watawala wa Waislamu wakiendelea na misimamo yao ya fedheha ya kula njama na kurahisisha mambo kwa ajili yake, wakicheza dori ya mwangalizi na mwandishi wa habari anayeripoti habari na kutoa maoni yake kwa misemo isiyozuia wala kutibua njama.
Kwa hivyo, Qatar iliandaa mnamo Jumanne, 16/12/2025, kongamano pana la kimataifa linaloongozwa na Kamandi Kuu ya Amerika (CENTCOM), kwa kushirikisha wawakilishi kutoka zaidi ya nchi 25, kwa lengo la kupanga uanzishwaji wa jeshi la kimataifa ambalo litafafanuliwa kama jeshi la kuleta utulivu kwa Gaza, ambalo linakusudiwa kuwa uvamizi wa kimataifa ambao utahifadhi usalama wa Mayahudi na kuhakikisha kupita kwa mpango wa Marekani, huku, kwa upande mwengine, ikitosheka kwa taarifa ya kulaani uidhinishaji wa serikali ya Kiyahudi wa kuanzishwa kwa sehemu za makaazi 19 katika Ukingi wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, ikizingatiwa kuwa ni “ukiukwaji wa wazi wa maazimio ya kimataifa”!
Ama kuhusu rais Erdoğan wa Uturuki, anaendelea na juhudi zake za kuwaruhusu Mayahudi na Trump kumruhusu kutuma majeshi ya Uturuki ndani ya vikosi hivyo vya kimataifa, aliridhika na maneno ya uandishi wa habari kuhusu uhalifu wa Mayahudi huko Gaza na Syria, ambapo alisema: “Vitendo vya uchokozi vya Israel dhidi ya Syria hivi sasa ni kikwazo kikubwa kwa usalama na utulivu wa nchi hii kwa muda mrefu.” Na kuhusu uhalifu wa Mayahudi katika Gaza, alisema: “Waliiharibu Gaza kwa mabomu makubwa mara kumi na nne kuliko yale yaliyoangushwa juu ya Hiroshima, hivyo tunawezaje kuzungumzia mfumo wa kimataifa unaofanya kazi na kuzuia ukosefu wa haki?”
Kuhusu Misri, inashughulishwa na kujadili hali na Poland, ambayo haina uzito na dori yoyote, kama Waziri wake wa Mambo ya Nje Badr Abdel Aaty alivyojadili na mwenzake wa Poland Radosław Sikorski juhudi za kuimarisha usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza na kuhakikisha kuingia kwa misaada ya kibinadamu, pembeni mwa Jukwaa la Wizara ya Mambo ya Nje la Sir Bani nchini Imarati, kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri.
Ama kuhusu Jordan, Waziri wake wa Mambo ya Nje Ayman Safadi aliridhika na kulaani na kukataa kile kinachotokea na kutoa wito wa kuwepo kwa suluhisho la dola mbili; mradi wa kuachiliwa kwa ardhi, kama alivyothibitisha mnamo Jumatatu ulazima wa kukomesha ongezeko hatari la vurugu na hatua haramu za uvamizi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu na ukiukaji unaoendelea wa hadhi ya kihistoria na uhalisia wa kisheria katika Jerusalem na maeneo yake matakatifu, na kuunganisha kufikiwa kwa utulivu na upeo wa wazi wa kisiasa unaojumuisha dola huru, yenye ubwana ya Palestina huru, kwenye mipaka ya 4 Juni 1967, huku Jerusalem Mashariki ikiwa mji mkuu wake, kwa mujibu wa maazimio ya uhalali wa kimataifa na Mpango wa Amani wa Kiarabu.
Wakati huo huo, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Kamisheni ya Muungano wa Afrika zimetoa taarifa ya pamoja kufuatia kikao cha mashauriano kilichofanyika mnamo Jumanne kwenye makao makuu ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu katika mji wa Jeddah, kuhusu jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua zote zinazohitajika ili kuhakikisha kuwa inawajibisha uvamizi huo kwa ukiukaji na jinai zake zote, na kuhakikisha kuwa unafunguliwa mashtaka, mbele ya mahakama za kitaifa, kikanda, na za kimataifa, na hasa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, na Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ili kukomesha hali ya kutojali sheria, na kutoa ulinzi wa kimataifa kwa watu wa Palestina.
Hivyo tunaona jinsi watawala wa Waislamu wanavyosimama kidete na Mayahudi na Trump ili kupitisha mipango yao na kuficha jinai zao, huku wakitosheka na kulaani na maelezo ya uandishi wa habari juu ya jinai za Mayahudi, kana kwamba ni sindano za ganzi kwa rai jumla ya umma, kwa kuhofia kwamba akili zinaweza kutafakari juu ya hali hiyo na kuongozwa kwenye njia ya wokovu.
Kukabiliana na uchokozi wa Mayahudi na mipango ya Trump hakupatikani kwa kupitisha miradi ya uvamizi na kujaribu kusuluhisha mzozo huo kupitia taasisi na uhalali wa kimataifa, ambazo zimekuwa na zinaendelea kuwa uungaji mkono na msaada wa uvamizi huo. Wala kulaani, kushutumu, na misemo ya maelezo ya uandishi wa habari haifai kwa uvamizi na kiburi cha Mayahudi. Badala yake, ni muhimu kuhamasisha majeshi kuikomboa Palestina na kuikomboa Lebanon, Syria, na maeneo mengine ya kanda hiyo kutokana na maovu ya Mayahudi. Vyenginevyo, damu ya Ummah itaendelea kumwagika, na kiburi cha Mayahudi na Trump kitaendelea kuongezeka. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللّهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُّؤْمِنِينَ]
“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini.” [Surat At-Tawbah: 14].
Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |



