Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
| H. 1 Sha'aban 1447 | Na: H 1447 / 046 |
| M. Jumanne, 20 Januari 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hitimisho la Kampeni “Khilafah sio Ndoto… Bali, ni Kilio cha Ulimwengu Unaowaka Moto!”
(Imetafsiriwa)
Leo, kwa Msaada Wake, tunahitimisha kampeni ya kimataifa iliyozinduliwa na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, kwa maelekezo ya Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, katika kumbukumbu ya miaka 105 ya kuvunjwa kwa Khilafah, ambayo iliamshwa na wanaume na wanawake wa Hizb ut Tahrir kote ulimwenguni. Kampeni hii ilijumuisha amali zifuatazo:
Kampeni ilianza na hotuba ya Amiri wa Hizb ut Tahrir, ambayo ilitangazwa kwa sauti kupitia majukwaa mbalimbali ya hizb. Ndani yake, alihutubia Ummah wa Kiislamu kwa jumla, akiukumbusha jinsi wakoloni makafiri walivyoweza kuivunja Khilafah mnamo 1924 M kupitia njama iliyoongozwa na Uingereza kwa msaada wa wasaliti kutoka kwa Waarabu na Waturuki. Kisha akahakiki hali ya ardhi za Waislamu baada ya kuvunjwa kwa Khilafah chini ya watawala Ruwaibidha (watepetevu duni): jinsi jana walivyoiharibu ardhi iliyobarikiwa ya Palestina kwa mara ya kwanza, na jinsi leo wanavyotafuta kuiharibu kwa mara ya pili kwa kukimbilia kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi chini ya uongozi wa Rais wa Amerika, Trump, ambaye anajitahidi mbele ya macho na masikio yao kuinyakua Gaza kwa ajili yake mwenyewe ili yeye na Mayahudi waweze kuisimamia wanavyotaka. Kisha akahakiki hali ya ardhi za Waislamu leo chini ya watawala Ruwaibidha, na jinsi bado zinavyokabiliwa na njama za ugawanywaji wa kikoloni na ukandamizaji wa kijinai nchini Sudan, Libya, Yemen, Syria, Kashmir, Chechnya, Timor Mashariki, Cyprus, Myanmar, na Turkistan Mashariki. Kisha akawahutubia wanajeshi katika majeshi ya Waislamu na kuwakumbusha wasifu wa wale waliowatangulia kuanzia wanajeshi wa Uislamu na makamanda wao mujahidina, Harun al-Rashid, Salah al-Din, Muhammad al-Fatih, Selim III, na Abdul Hamid, ambao utukufu wao umebakia kuchongwa imara katika kumbukumbu ya historia. Aliwataka wafuate haki na kuwaiga kwa kuikomboa Palestina kupitia jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, kisha kuregesha kila shubiri ya ardhi ya Waislamu iliyonyakuliwa na makafiri, ambapo ndani yake kuna heshima kwao na kwa Waislamu. Kisha akawakumbusha, Mwenyezi Mungu amhifadhi, jinsi Hizb ut Tahrir inavyoongoza ulinganizi wa kusimamisha tena Khilafah kote ulimwenguni, na jinsi ulinganizi huu umekuja kuvuruga usingizi wa Wakoloni makafiri wa Magharibi, kwa hivyo vipi basi ikiwa wanajeshi katika majeshi ya Waislamu wangeisimamisha? Aliwasilisha jinsi hali ya Uislamu na Waislamu itakuwa lau Khilafah yao ingesimamishwa leo: kuanzia kufurushwa kwa ushawishi wa kikoloni kutoka katika ardhi zetu, hadi heshima ya Uislamu na Waislamu, hadi kuwaandama wakoloni makafiri ndani kabisa ya ardhi zao wenye. Alithibitisha kwamba ushindi huu na ulinzi ni ahadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kutoka kwa Mtume Wake (saw), kwamba Mwenyezi Mungu ataipa ushindi Khilafah endapo Waislamu wataisimamisha. Kisha akathibitisha kwamba ulinganizi wa Hizb ut Tahrir wa kusimamisha Khilafah ni ulinganizi wa heshima na nguvu, kwani unahifadhi dini na maisha ya kidunia, na kwamba ndio kile ambacho Maswahaba walianzisha baada ya kifo cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kabla hata hawajaendelea kumzika, licha ya umuhimu na uzito wa mazishi na hivyo umuhimu wake na ukubwa wa kuyafanyia kazi kiasi kwamba walichelewesha mazishi yake (saw). Amiri wa Hizb ut Tahrir alihitimisha hotuba yake kwa kuthibitisha kwamba Khilafah ni kadhia ya uwepo wa Ummah wa Kiislamu, na kwamba tunahakikishiwa kurudi kwake kwa ahadi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), lakini kwamba hili halitatokea isipokuwa kupitia kazi nzito na ya dhati. Aliwataka Waislamu na watu wenye nguvu na ushawishi kuharakisha kujiunga na ulinganizi huu na kutoa nusra.
Kisha zikafuata amali za mwamko za wanaume na wanawake wa Hizb ut Tahrir kote ulimwenguni, ambazo zilijumuisha hotuba zilizorekodiwa, makala, na maoni, pamoja na kufanya visimamo kadhaa na kufanya makongamano katika miji kadhaa kote duniani, moja ikiwa ni kongamano la kimataifa lililofanywa na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwenye Chaneli ya Al-Waqiyah TV. Al-Waqiyah TV pia ilitoa msururu wa vipindi maalum kwa ajili ya mnasaba huu, pamoja na maingiliano muhimu ya wanaume na wanawake wa Hizb ut Tahrir kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii mtandaoni. Amali hizi zilichapishwa na majukwaa mbalimbali ya hizb katika lugha nane.
Vile vile, sisi katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir tunawaomba wafanyikazi wote waaminifu katika uwanja wa vyombo vya habari kuchangia katika kusambaza amali za kampeni hii, tukitumai kwamba Mwenyezi Mungu atatupa sisi na wao mafanikio katika kufanikisha uzinduzi wa pili wa Ummah wa Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.
Mhandisi Salah Eddin Adadah
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |



