Ukosoaji wa Trump wa India ... Maslahi ya Amerika, Sio Urafiki na Pakistan
- Imepeperushwa katika Pakistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo 30 Julai 2025, Rais wa Marekani, Donald Trump alitangaza msururu wa ushuru wa kulipiza kisasi dhidi ya India, akiikosoa kwa kuwa na “vizuizi vizito na visivyo vumilika vya biashara visivyo vya ushuru” na kutoza ushuru wa forodha wa 25% pamoja na faini. Huku Trump alkikiri “urafiki” na India, aliikosoa vikali kwa kununua vifaa vya kijeshi vya Urusi na mafuta ya bei nafuu wakati Marekani ilikuwa ikiishinikiza Urusi kumaliza vita nchini Ukraine. Katika karipio la hadharani lisilo la kawaida, Trump aliusifu uchumi wa Urusi na India kuwa “umekufa” na akamuonya Rais wa zamani wa Urusi Medvedev “kuchunga mdomo wake.”



