Unyanyasaji wa Kimpangilio wa Kijinsia Dhidi ya Wanawake wa Sudan Hautoi Jibu lolote kwa Kukosekana kwa Dola Inayojali Heshima ya Mwanamke Mwislamu
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo Alhamisi tarehe 11 Disemba, shirika, ‘The Strategic Initiative for Women in the Horn of Africa’, liliripoti kuwa limerekodi karibu matukio 1300 ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake katika majimbo 14 nchini Sudan tangu vita vianze nchini humo mnamo Aprili 2023, huku Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vikilaumiwa kwa 87% ya visa hivi. Lilielezea unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake ukitumika kama silaha ya kimfumo katika mzozo huo, likisema “umeenea, unarudiwa rudiwa, unakusudiwa na mara nyingi unalenga”. Ubakaji ulichangia robo tatu ya matukio yaliyorekodiwa, huku visa 225 vikihusisha watoto, baadhi wakiwa na umri wa miaka 4. Matukio yalitokea majumbani, maeneo ya umma na pia yalijumuisha kizuizini cha muda mrefu cha wanawake ambao waliteswa, kubakwa na genge na ndoa za kulazimishwa. Mnamo Jumapili tarehe 7 Disemba, vikundi vya matibabu vya Sudan viliripoti kwamba watoto na wanawake kadhaa walinyanyaswa kingono na kubakwa walipokuwa wakikimbia kukamatwa kwa El Fasher huko Darfur na RSF Oktoba hii.



