Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Ufunguzi wa Afisi ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan mjini Port Sudan

Kwa msaada na muongozo wa Mwenyezi Mungu, leo, Jumapili, tarehe 7 Ramadhan 1445 H, sawia na tarehe 17 Machi, 2024, Afisi ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan imezinduliwa mjini Port Sudan (mtaa wa Al-Athmah), kusini-mashariki mwa uwanja. Itatumika kama nguzo ya kueneza fikra za Kiislamu, jukwaa la thaqafa ya Kiislamu, kitovu cha utambuzi wa kisiasa, na nukta kianzilishi cha ubebaji ulinganizi kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya utume.

Soma zaidi...

Je, Ramadhan itaweka Taqwa katika Nyoyo zenu Kusimama kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina?

Hizb ut Tahrir / Kenya kwa furaha, inawapongeza Waislamu nchini na kote duniani kwa ujumla kwa kuwasili kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Je, Ramadhan itaweka Taqwa katika Nyoyo zenu Kusimama kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina?

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Kenya kwa furaha, inawapongeza Waislamu nchini na kote duniani kwa ujumla kwa kuwasili kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Tunapoingia katika mwezi huu wa rehema, msamaha na kukombolewa na Moto wa Jahannam, tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atujaalie nguvu na afya ya kutekeleza amali adhimu ya saumu ambayo si wajibu tu bali ni moja ya nguzo tano za Uislamu.

Ramadhan hii inakuja huku ulimwengu ukishuhudia mgongano kati ya matakwa ya Umma wa Kiislamu ya kushikamana na Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na matakwa ya ukafiri wa Magharibi. Umma umeonyesha uaminifu wake kwa Uislamu na unatamani kwa dhati ushindi wa Mwenyezi Mungu. Ulimwengu unashuhudia kufilisika kiakhlaqi kwa maadili ya Magharibi huku wakiunga mkono mashambulizi ya kikatili ya ‘Israel’ huko Gaza. Dola na vyombo vya habari vya Magharibi vinaonyesha rangi zao halisi za unafiki na ubaguzi wa rangi.

Cha kusikitisha ni kwamba, unyama unaofanywa na majeshi ya Kiyahudi dhidi ya ndugu zetu wa Gaza bado haujachemsha nyoyo wala mishipa ya viongozi wa Kiislamu na majeshi yao! Enyi viongozi! Je, saumu yenu itaweka taqwa katika nyoyo zenu na kukata mahusiano na umbile la Kiyahudi? Enyi majeshi, je Ramadhan itawapeni taqwa ya kuwapuuza watawala wenu waliomfanyia khiyana Mwenyezi Mungu, Mtume wake na waumini ili muanze kuandamana kwenda Palestina na kupigana na jeshi la Mayahudi?

Katika historia yote, Ramadhan imekuwa ni mwezi wa ukombozi na ushindi. Historia hii angavu kwa hakika itahuisha ushindi katika Vita vya Badr, Qadisiyyah na Ein Jalut. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atukubalie amali zetu na aujaalie Ummah huu mlinzi na ngao Khilafah kwa njia ya Utume. Khilafah ambayo itakusanya majeshi ya Waislamu ili kuling'oa umbile uaji la Kiyahudi na kukomboa sio tu Palestina inayokaliwa kwa mabavu bali ardhi zote za Waislamu.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Kenya

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki: Amali Kubwa “Ramadhan ni Wakati wa Kuungana kwa Ajili ya Gaza!”

Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili ambayo yamekuwa yakiendelea kwa muda wa miezi mitano, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi na kujeruhiwa Waislamu zaidi ya 110,000 hadi sasa, Hizb ut Tahrir/ Wilayah ya Uturuki iliandaa amali kubwa ya halaiki kote Uturuki.

Soma zaidi...

Serikali Mpya ya Pakistan Itaisagasaga Pakistan kwa Baraka za Marekani na Vibaraka wake katika Uongozi wa Kijeshi wa Pakistan

Mnamo tarehe 4 Machi 2024, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani alisema, “Pakistan ya kidemokrasia ni muhimu kwa maslahi katika ya Marekani na Pakistan, na ushirikiano wetu na Waziri Mkuu mpya Shehbaz Sharif na serikali yake utaendelea kuzingatia kuendeleza maslahi haya ya pamoja.” Kwa hivyo, Marekani inasalia katika udhibiti kamili wa Pakistan kupitia vibaraka wake katika uongozi wa kijeshi.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu