Jumanne, 07 Shawwal 1445 | 2024/04/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Australia

H.  26 Rabi' I 1442 Na: 01 / 1442 H
M.  Alhamisi, 12 Novemba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ripoti ya Uhalifu wa Kivita Nchini Australia

(Imetafsiriwa)

Serikali ya Australia inatarajiwa kutoa maelezo ya madai ya uhalifu wa kivita uliofanywa na Vikosi vya Ulinzi vya Australia nchini Afghanistan.

Madai ya kudumu kwa utovu wa nidhamu wa vikosi vya Australia nchini Afghanistan yamekuwa yakiongezeka kwa miaka, ikiwemo dhidi ya wale waliopewa medali mashuhuri kwa utumishi wao nchini Afghanistan.

Serikali ya Australia, kwa upande wake, imekuwa ikiburuta miguu yake upande huu na kufanya kila jaribio la kuzika shuhuda hizi. Huku mkono wake ukilazimishwa, serikali ya Australia sasa itatoa maelezo 'yaliyo chakachuliwa" ya uchunguzi wake wa uhalifu wa kivita.

Hizb ut Tahrir / Australia inasema yafuatayo kuhusiana na hili:

1. Uharibifu wa uvamizi shirika wa Afghanistan hauhitaji kujulishwa. Australia, kama sehemu ya juhudi hii, inahusika na maangamizi jumla ya taifa zima. Ripoti, nyuma ya uchunguzi iliouweka kibinafsi, kamwe haitaiondolea Australia uhalifu uliofanywa dhidi ya watu wote wa Afghanistan.

2. Hofu maafa yanayotekelezwa nchini Afghanistan ni uhalisia unaojulikana. Usambaratishaji wa miji yote, utumiaji silaha zenye maangamivu makubwa zaidi tangu Hiroshima, kuanzishwa kwa vyumba vya mateso, kambi ya anga ya Bagram, mipango na chati za mauaji, huku wafu wakionyeshwa kama kumbukumbu za askari waliopotoka. Ulimwengu haungojei uchunguzi ili kuona maumbile au ukubwa wa kile ulichojionea wenyewe.

3. Hakuna imani kabisa kwa Australia kujichunguza yenyewe kwa madai ya uhalifu wa kivita. Kwa msingi wa usalama wa kitaifa, vitisho halisi vya mwenendo wa Australia nchini Afghanistan kamwe hautakubaliwa, kwa njia ile ile Barack Obama alizuia kutolewa kwa picha zenyekutia hatiani zaidi kutoka Abu Ghraib nchini Iraq.

4. Uchunguzi wa aina hii si zaidi ya bahashishi ya mazoezi ya kuokoa uso. Watu binafsi wanaweza kutolewa kafara, ahadi za uboreshaji kutolewa, uhakikisho wa viwango vya hali ya juu kukaririwa. Lakini uhalisia mbaya wa mashini ya vita ya Australia utaendelea bila kukoma, umefunikwa kwa fadhili nzuri na kudhibitishwa zaidi na mchakato ovyo wa mahakama.

5. Waziri Mkuu wa zamani wa Australia John Howard alitoa 'pole' kujibu janga ambalo lilikuwa ni uvamizi wa Iraq. George W Bush alikubali kuwa walipata ujasusi wa 'kimakosa'. Maneno na misemo mingi badala ya mamilioni ya maisha yalipotea na mataifa yote kuangamizwa. Hakujawahi kuwa na uwajibikaji wowote, wala hakuwezi kuwa wakati wahalifu wanapewa jukumu la kujichunguza wenyewe.

Bila shaka, Scott Morrison atapanua utamaduni huu wakati mkono wake utakapolazimishwa pia. Haishangazi, hitimisho tayari limeshanakiliwa wakati anaposema kwa kuchukua tahadhari: "Kuna mwenendo fulani wa kuchukiza hapa, lakini hatuwezi kuuchukua huo na kuutumia kwa kila mtu ambaye amevaa sare na ikiwa tutafanya hivyo, hiyo itakuwa ni dhulma kubwa sana.'

6. Uchunguzi wa uhalifu wa kivita wa Australia unaonekana kana kwamba upande mmoja kuwa ni juhudi ya kudhoofisha uwezekano wa vikosi vya Australia kushtakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC). Hii ni mahakama ile ile ambayo majaji wake Amerika imewatishia kwa kulipiza kisasi endapo kesi ya jinai itaibuliwa dhidi yao. Kwa kutegemea mfano wa Amerika, Australia imetaka kukwepa ICC pia, ikisisitiza ni Waaustralia tu wanaoweza kuchunguza mwenendo wa Australia. Huku kukiwa hakuna imani kwa ICC kama chombo, hata Australia kujifanya inashikiliwa kwa viwango vilevile kama vile kila mtu mwengine ni vigumu kuhimili.

7. Ulimwengu unahitaji mno mtindo mpya wa mwenendo. Kwa muda mrefu sana dola za kihalifu za Mashariki pamoja na Magharibi zimetenda bila kujali sheria. Mipangilio ya kimataifa iliyoanzishwa ili kudhibiti hali ya baada ya Vita vya Pili vya Dunia ilibuniwa kama upanuzi wa nguvu kama hiyo, na miongo iliyofuata ilishuhudia moja ya uhamishaji mkubwa wa utajiri na nguvu ambao haujawahi kujulikana na mwanadamu, yote juu ya migongo ya masikini na wachochole.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Australia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Australia
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu