Jumatatu, 20 Jumada al-awwal 1447 | 2025/11/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Australia

H.  14 Jumada I 1447 Na: 05 / 1447 H
M.  Jumatano, 05 Novemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mkuu wa Ujasusi wa Australia Azindua Ulinzi wa Kipumbavu kwa Umbile la Mauaji ya Halaiki

(Imetafsiriwa)

Mkurugenzi Mkuu wa ASIO, Mike Burgess, alitumia hotuba yake ya Taasisi ya Lowy jana kupanua ulinzi wa serikali ya Australia kwa umbile la mauaji ya halaiki.

Burgess alitoa mkusanyiko mkubwa wa maneno yaliyopitwa na wakati, yaliyotolewa kutoka kwa serikali na wapigiaji debe wa mauaji ya halaiki, akionya kuhusu vitisho kwa mshikamano wa kijamii, kuongezeka kwa chuki dhidi ya Mayahudi na uhalalishaji wa vurugu za kisiasa. Burgess hata alifikia hatua ya kuonya kuhusu uwezekano wa mauaji ya kisiasa yanayotokana na nchi za kigeni nchini humu.

Katika jaribio lake ovyo la kupotosha dhana ya mwathiriwa/mvamizi, Burgess aliitaja Hizb ut Tahrir kama mfano wa chama kinachotaka kutumia vibaya malalamiko yanayozunguka Gaza. Alisema:

“Ingawa chama kama Hizb ut Tahrir kina motisha ya kidini, tabia yake ya uchochezi, matamshi ya kukera na mkakati wake wa kudhuru, ni sawa na mbinu za Mtandao wa Kijamaa wa Kizayuni. Kulaani kwa shirika hilo [Israel] na Mayahudi huvutia umakini wa vyombo vya habari na husaidia usajili wa watu. Lakini kwa makusudi huacha kukuza vitendo vya vurugu vya nje ya nchi au vitendo vya vurugu vya kisiasa. Hizb ut Tahrir inataka kujaribu na kupanua mipaka ya uhalali bila kuivunja. Kama ilivyo kwa Wanazi wapya, hii haifanyi tabia yao ikubalike. Ninaogopa matamshi yake ya kupinga [Israel] yanachochea na kuhalalisha simulizi pana za chuki dhidi ya Mayahudi.”

Hizb ut Tahrir / Australia ingependa kusema yafuatayo katika suala hili:

1. Hotuba hii inayotolewa katika Taasisi ya Lowy, iliyoanzishwa na mtetezi shupavu wa Uzayuni na mauaji ya halaiki Frank Lowy, ni ukumbusho wenye kugusa moyo wa kile serikali inachomaanisha inapozungumzia mshikamano wa kijamii. Burgess ilizungukwa na waungaji mkono wa wauaji wa watoto na wabakaji wafungwa, ambao wanaona inakubalika kuangamiza miji mizima juu ya vichwa vya wakaazi wake, na ikiwa wapo wangeokoka, hawana wasiwasi wa kuwaua kwa njaa badala yake. Mshikamano wa kijamii unamaanisha wahalifu wanaruhusiwa kuendelea na uhalifu wao huku waathiriwa wao wakitarajiwa kuteseka kwa utiifu.

2. Australia imekuwa mpigiaji upatu wa mauaji ya halaiki kila wakati. Ilikubalika wakati Uingereza ilipoikalia nchi hii mnamo 1788. Ilikubalika wakati Australia ilipohalalisha mauaji ya halaiki ya kwanza nchini Palestina mnamo 1947 na tena kwa mauaji ya halaiki yanayoendelea tangu 2023. Ukweli kwamba uhalifu huu wote ulichukuliwa kuwa ‘halali’ hufanya wasiwasi wa Burgess kuhusu kuvunja sheria za sasa kuwa wa kufedhehesha.

3. Miaka ishirini ya ‘vita dhidi ya ugaidi’ ilitufundisha urefu ambao dola za Magharibi zinaweza kwenda ili kujikinga na matokeo ya matendo yao. Badala ya kuchukua jukumu la jinai zao za zamani, ziliongeza uhalifu wao kwa kungamizi nchi nzima, wakiua mamilioni bila kubagua na kuharamisha upinzani wowote kwa vitisho hivi, hata kama ilikuwa ni kupaza sauti tu. Mkakati huo huo unatolewa ili kulitakasa umbile la mauaji ya halaiki kutokana na uhalifu wake, isipokuwa, wakati huu, ulimwengu tayari umenaswa nao muda mrefu uliopita.

4. Hisia za kupinga [Israel] ni jambo la ulimwengu wote, linaloonyeshwa na watu wote, wa imani zote na kutoka pembe zote za dunia. Ni jibu pekee kwa uhalifu wa uvamizi huo, ndiyo maana dunia imejifunza kukabiliana na mashtaka yasiyo na msingi ya chuki dhidi ya Mayahudi bila zaidi ya kupiga miayo.

5. Madai kwamba Hizb ut Tahrir inatafuta kuitumia vibaya jamii ya Waislamu kuhusu suala la Gaza yanawafanya Waislamu kuwa watoto katika kuwadharau kwao. Kana kwamba yanaashiria kuwa Waislamu hawawezi kuwa na fikra huru ya kisiasa, au hawaoni kile ambacho ulimwengu mzima unaona, na kwa hivyo wanahusika na njama za siri za watendaji waovu. Kuwafanya watoto huku, bila shaka, ndio msingi wa muamala wa serikali mtawalia kwa jamii ya Waislamu unaotumiwa ili kuhalalisha adhabu yao ya pamoja.

6. Shambulizi la Burgess dhidi ya Hizb ut Tahrir ni kampeni ya kijanja iliyoundwa kuifikia jamii ya Waislamu. Hizb ut Tahrir ni mojawapo ya sauti zenye maadili na zisizoyumba katika jamii ambazo zimekuwa zikipinga vikali uvamizi wa Palestina. Serikali na wapigiaji debe wa mauaji ya halaiki wanatumai kuinyamazisha jamii kupitia vitisho vya mara kwa mara vya ukandamizaji wa serikali, hata kama inamaanisha kuanzisha sheria za kiholela kwa ajili ya kusudi hili pekee.

7. Ulinganizi wa Hizb ut Tahrir haukufungika tu katika kuondoa ukandamizaji kutoka ardhi iliyobarikiwa ya Palestina na kuikomboa kutoka kwa wavamizi wa Kizayuni. Pia inabeba wito wa kuondoa ukandamizaji kutoka kwa watu wote wanaokandamizwa kote ulimwenguni – Waislamu na wasiokuwa Waislamu – wanaoteseka chini ya tawala za kisekula ambazo zimewachosha, kuwafukarisha, na kuwatiisha watu wao, na kuwageuza kuwa ala tu za uzalishaji kwa kipote cha mabepari walafi. Mradi wa Hizb ut Tahrir ni badali ya kihadhara kwa mfumo kinyonyaji wa kibepari – sio mfumo unaotumikia asilimia moja, kama ilivyo katika ulimwengu wa kibepari unaoongozwa na Magharibi. Kupitia mradi huu, Hizb ut Tahrir inatoa wito wa kusimamishwa kwa Khilafah ya Kiislamu kwa njia ya Utume, ambayo inahukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu – si tu kuleta usalama, amani, na haki kwa ardhi za Waislamu, bali pia kueneza haki, usalama, na utulivu ulimwenguni mzima. Hivi ndivyo Muumba alivyotuamuru kufanya, kile kinachomridhisha, na kile kitakachotuingiza Peponi.

8. Shambulizi la Burgess dhidi ya Hizb ut Tahrir ni sehemu ya kampeni pana ya chuki dhidi ya Uislamu inayoendeshwa na vyombo vya habari vya Magharibi dhidi ya Uislamu na Waislamu. Lengo ni kuwapotosha wanadamu na wenye akili timamu katika ulimwengu wa Magharibi kuhusu umbile halisi la Uislamu – ili wasiipe mgongo hadhara ya Kimagharibi iliyofilisika na kuchagua Uislamu kama hadhara badali, mfumo kamili wa maisha wenye usawa, na dini ya haki kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Burgess, katika suala hili, ni kama washirikina wajinga wa Kiquraysh waliomtukana Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ili kupotosha taswira ya Mtume na ujumbe wake – lakini je, walifanikiwa?! Jambo hili ni la wakati mmoja tu kabla ya watu kutambua uovu kutoka kwa usafi.

9. Ili kukabiliana na utata wa makusudi wa Burgess, na wakati mwingine, taarifa potofu za moja kwa moja, tungependa kukariri mtazamo wa Uislamu kuhusu suala la Palestina, unaoshikiliwa na Waislamu kote ulimwenguni:

i. Palestina ni ardhi ya Kiislamu, na Waislamu pekee ndio watakaoamua mustakabali wake.

ii. Chini ya Uislamu, Palestina ilikuwa makaazi ya Waislamu, Mayahudi na Wakristo, na kipindi hiki cha utawala wa Kiislamu bado kinasimama kama zama za dhahabu za kuishi pamoja.

iii. Palestina ilikaliwa kimabavu na Uingereza na kukabidhiwa kwa Wazayuni ili kutumikia maslahi ya kikoloni ya Uingereza (baadaye ilichukuliwa na Marekani). Uvamizi wa Waingereza, na baadaye Wazayuni, kamwe hautatambuliwa na Uislamu, na Waislamu daima watakataa jaribio lolote la kuhalalisha uwepo wa uvamizi.

iv. Palestina ilitekwa kupitia uvamizi wa kijeshi, na jibu pekee linalokubalika kwa uvamizi wa kijeshi ni kufukuzwa kijeshi.

v. Ni jukumu la majeshi ya Waislamu waliopo, ambao ni wana wa ardhi hizi, kuingilia kati kijeshi nchini Palestina sio tu kuzuia mikono ya uvamizi wa Wazayuni, bali pia kukomboa ardhi zake zote.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Australia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Australia
Address & Website
Tel: 0438 000 465
www.hizb-australia.org
E-Mail:  media@hizb-australia.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu