Taasisi zote za Kikoloni, ikiwemo Tume Kuu ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu, ni Ala za kufikia Maslahi ya Marekani; Khilafah pekee kupitia kung'oa Misingi ya Taasisi zote hizi ndio itakayolinda Uislamu, Maslahi ya Watu na Ubwana wa Nchi hii
- Imepeperushwa katika Bangladesh
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Licha ya maandamano na wasi wasi wa ngazi zote za wananchi na vyama vya kisiasa, hatimaye serikali ya mpito ya Bangladesh imetia saini makubaliano ya kuanzisha afisi ya taasisi ya Kikoloni yenye ushawishi wa Marekani, Tume Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa. Uamuzi huu wa serikali umekaribishwa na mashirika ya wanawake yenye chuki dhidi ya Uislamu, ambayo yanashiriki kikamilifu katika usawa wa kijinsia wa Magharibi, utambuzi wa kijamii wa "taaluma" ya kuchukiza ya ukahaba, na kile kinachoitwa haki za binadamu za LGBTQ ikiwa ni pamoja na ushoga unaoangamiza jamii; ilhali wana utata na kukosolewa na ngazi zote za watu kwa sababu hawana sauti katika kuweka haki adilifu na utu wa wanawake, uhuru kutokana na kazi za kikatili, na uboreshaji wa hali ya maisha.



