Jumatatu, 17 Muharram 1444 | 2022/08/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  17 Sha'aban 1443 Na: 1443 H / 15
M.  Jumapili, 20 Machi 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mahakama Kuu ya Kisekula ya Karnataka Inasubutuje kutoa "Fatwa" kuhusiana na kile ambacho Mwenyezi Mungu (swt) Amewafaradhisha Waislamu!

Enyi Waislamu! Ni nani Mwengine Isipokuwa Khilafah Atalinda Haki na Heshima za Dada zetu?

(Imetafsiriwa)

Kwa kushikilia marufuku ya hijab kwa wasichana wa shule na walimu wa Kiislamu katika taasisi za elimu chini ya serikali ya Jimbo hili inayoendeshwa na chama chenye misimamo mikali cha Hindutva Bharatiya Janata (BJP), Mahakama Kuu ya Karnataka ilitoa uamuzi kwamba kuvaa hijab sio kitendo muhimu cha kidini cha Uislamu! Kwa hakika, hii itatoa utangulizi wa kisheria kuwatesa Waislamu wa Majimbo mengine zaidi; kana kwamba, amri hii ya mahakama ilitolewa kuwaadhibu Waislamu jasiri mithili ya Dada yetu Muskan aliyeonyesha ushujaa mbele ya kundi la watu wenye jeuri wa Hindutva kwa kutamka “Allahu Akbar”, akionyesha ujasiri wake katika itikadi ya Kiislamu.

Enyi Watu! Ingawa kila Muislamu anajua kwamba kuvaa hijab ni wajibu katika Uislamu, vipi Ritu Raj, Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Karnataka, Baniani Msekula, anaweza kusubutu kufafanua iwapo uvaaji hijab ni kitengo muhimu katika Uislamu? Hapo awali, watawala wa kisekula, wasomi na vyombo vya habari kote ulimwenguni kwa unafiki waliunga mkono msimamo wa dada yetu shujaa, Mushkan, kukamata rai maarufu kwa msingi wa kile kinachoitwa kauli mbiu ya kinafiki ya "uhuru", lakini wakafichua unafiki wao waliposhindwa kukosoa amri ya mahakama ambayo hata haiendani na kile kinachoitwa "uhuru wa kidini". Kwa hakika, wako macho sana katika kutukuza uhuru wa ukaaji uchi, lakini wakafungia macho haki ya mwanamke ya kujifinika wakati ni faradhi ya Mola wa Ulimwengu.

Enyi Watu! Hijab ni ishara ya heshima ya dada zetu na ni kadhia ya uhai na kifo kwa Waislamu. Mnajua kwamba wakati mwanamke mmoja tu Muislamu alipovuliwa hijab yake kwa nguvu na mwanamume kutoka kabila la Kiyahudi la Banu Qaynuqa, Mtume wetu kipenzi (saw) mara moja alituma jeshi dhidi yao na kulifukuza kabila zima kutoka Madina. "Fatwa" ya Mahakama Kuu ya Karnataka ya kupiga marufuku vazi la Hijab ni sehemu ya njama zinazoendelea za serikali za kibaraka wa mabeberu za kisekula za kufuta kwa mpangilio kitambulisho cha Uislamu na Waislamu kutoka kwa bara hilo. Tabaka la watawala wa kisekula na wasomi wa nchi hii pia wanahusika katika njama hiyo hiyo. Mnajua kuwa dada zetu katika nchi hii wanakabiliwa na dhulma na kejeli kama hizo kutoka kwa mamlaka ya kisekula ndani ya serikali na taasisi zengine, pamoja na vyombo vya habari.

Enyi Waislamu wa Bangladesh na Bara hili! Ijapokuwa Wakoloni makafiri wa Magharibi walizigawanya ardhi zetu kwa nguvu kwa kutumia watawala wao vibaraka, walishindwa kuondoa mshikamano wenye nguvu wa udugu miongoni mwetu. Wakoloni wa kikafiri na vibaraka wao, watawala wa kisekula wa bara hili, wanakula njama dhidi ya Uislamu na Waislamu kwa sababu Bara zima la India ni ardhi ya Waislamu na Waislamu wametawala bara hili kwa muda wa miaka elfu moja. Waislamu wa bara hili wamefungwa imara na Uislamu, damu na historia ya pamoja. Kwa mujibu wa bishara njema za Mtume (saw), Hindustan itakuja tena chini ya utawala wa Kiislamu.

Ulinzi wa Uislamu na Waislamu haupaswi kutarajiwa kutoka kwa tabaka la sasa la watawala wa kisekula, ambao ni kibaraka wa Makafiri. Ni Khalifa pekee ndiye mlinzi wa Waislamu na Dola ya Khilafah itaulinda Uislamu na Waislamu. Mtume (saw) amesema,  «وَإِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»“Hakika Imam ni ngao watu hupigana nyuma yake na hujihami kwayo” (Sahih, Bukhari). Hivyo basi, ni faradhi kufanya kazi ya kuisimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume ili kuwanusuru dada zetu wanaopigania haki na heshima zao.

Enyi Vizazi vya Muhammad bin Qasim! Enyi Maafisa Wanyofu ndani ya Jeshi la Bangladesh! Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[وَإِنْ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمْ النَّصْرُ]

“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia” [Al-Anfal: 72]. Ikiwa msichana wa kawaida wa Kiislamu kama Muskan anaweza kuonyesha ujasiri kama huo katika kuutetea Uislamu, haifai kwenu kukaa kimya licha ya uwezo wenu. Hupaswi kusahau kwamba Khalifah Umawiyya Al-Waleed bin Abd al-Malik alikusanya jeshi la kutisha kutoka Iraq chini ya uongozi wa jenerali shupavu wa kijeshi Muhammad bin Qasim al-Thaqafi juu ya vilio vya wanawake wa Kiislamu, ambao walikandamizwa na dhalimu Raja Dahir huko Sindh, na kuumaliza utawala wa Raja Dahir Sen. Hivyo basi, toeni nussrah (msaada wa kimada) kwa chama chenye ukweli cha Hizb ut Tahrir ambacho kitaregesha Dola ya Khilafah kurudisha usalama kwa Ummah huu kwa mara nyingine tena na kutovumilia unyanyasaji wa mwanamke hata mmoja wa Kiislamu mikononi mwa maadui wa Uislamu. Khilafah ijayo itakuwezesheni kumfukuza Raja Dahir mpya, Hindutva Norendra Modi, na kuiregesha India chini ya kivuli cha Khilafah kupia kuiondoa mipaka hii bandia.

Abu Hurayra (ra) narrated, «وَعَدَنَا رَسُولُ اللَّهِ ﷺ غَزْوَةَ الْهِنْدِ فَإِنْ أَدْرَكْتُهَا أُنْفِقْ فِيهَا نَفْسِي وَمَالِي فَإِنْ أُقْتَلْ كُنْتُ مِنْ أَفْضَلِ الشُّهَدَاءِ وَإِنْ أَرْجِعْ فَأَنَا أَبُو هُرَيْرَةَ الْمُحَرَّرُ» “Mtume (saw) ametuahidi ufunguzi wa India. Basi iwapo nitaushuhudia nitatumia nafsi yangu na mali yangu. Iwapo nitauwawa nitakuwa miongoni mwa mashahidi bora na iwapo nitarudi nikiwa hai nitakuwa Abu Huraira aliyehuru (kutokana na madhambi)” [Ahmad, An-Nisa’i, Al-Hakim].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu