Jumatatu, 17 Muharram 1444 | 2022/08/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  21 Sha'aban 1443 Na: 1443 H / 17
M.  Alhamisi, 24 Machi 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kwa kuogopa Kuondolewa Madaraka Haraka, Serikali ya Hasina Inafuata Sera Hatari ya Kuiridhisha na Marekani

 (Imetafsiriwa)

Baada ya kufuatiliwa kwa miaka mingi, Bangladesh hatimaye imepitisha rasimu ya makubaliano ya ulinzi na Marekani wakati wa mazungumzo ya nane ya ushirikiano kati ya nchi mbili hazo yaliyofanyika Dhaka, Bangladesh mnamo siku ya Jumapili (Machi 20). Makubaliano miwili yameandaliwa kuhusu ACSA (Mkataba wa Upataji na  Utoaji Huduma) na GSOMIA (Makubaliano Jumla ya Usalama wa Taarifa za Kijeshi), ambayo yanatarajiwa kuwa makubaliano hivi karibuni. Chini ya Waziri wa Masuala ya Kisiasa wa Marekani Victoria Nuland alisema mazungumzo hayo yanahusisha masuala ya kiuchumi, usalama na teknolojia, na "tunapenda kuiona Bangladesh inashiriki pakubwa ndani yake (Mkakati wa Indo-Pacific) kwani nyinyi (Dhaka) mnapenda kuhusika  ndani yake" (Times ya India, Machi 20, 2022). Inavyoonekana, huenda mkaona manufaa ya kisiasa, kiuchumi, na kiusalama katika mapatano haya ya ulinzi yanayopigiwa debe na Marekani, lakini, kiuhalisia, haya yamethibitishwa kuwa yenye madhara kwa ubwana wa Ummah.

Enyi watu, mnapaswa kujua kwamba haya yanayoitwa mazungumzo ya ushirikiano ni chombo cha wakoloni makafiri kudhibiti jeshi letu, kuwatumia kama nishati kwa maslahi yao ya kijiografia, na kudumisha utawala wao juu ya watu na Dola hii pia. Marekani itatumia jeshi letu kama mafuta ya ushindani wao wa kijiografia katika Indo-Pasifiki, kama ilivyoelezwa na Victoria Nuland. Hapo awali, walikuwa wakivamia nchi zingine moja kwa moja kuchukua udhibiti. Na leo hii utawala huo huo unadumishwa lakini chini ya pazia la aina mbalimbali za misaada, mikataba ya kijeshi na ushirikiano na watawala wa kisekula vibaraka wao katika enzi hii ya ukoloni mamboleo. Ukweli wa mambo ni kwamba serikali fisadi ya Hasina inahisi vitisho na hofu ya kuondolewa madarakani na Marekani. Kwa hivyo, inashiriki katika msururu huu wa mazungumzo ili kufuata sera hatari dhidi ya Serikali ya kuiridhisha Marekani. Lakini serikali ya Hasina inapaswa kukumbuka kuwa Marekani kamwe haionyeshi huruma kwa serikali yoyote ya kibaraka mara tu lengo lake litakapotekelezwa.

Enyi Watu, Mwenyezi Mungu (swt) ameharamisha mazungumzo na mapatano kama hayo ambayo kwa hakika yanawapa makafiri ushindi juu yetu. Yeye (swt) asema:

 [إِن يَثْقَفُوكُمْ يَكُونُوا۟ لَكُمْ أَعْدَآءًۭ وَيَبْسُطُوٓا۟ إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ وَأَلْسِنَتَهُم بِٱلسُّوٓءِ وَوَدُّوا۟ لَوْ تَكْفُرُونَ]

“Wakikuwezeni wanakuwa maadui zenu, na wanakukunjulieni mikono yao na ndimi zao kwa uovu. Na wanapenda muwe makafiri.” [Al-Mumtahinah: 2].

Enyi Watu, sikilizeni wito wetu! Msiwe chini ya imani potofu kwamba vyama vingine vya kisiasa au watu binafsi chini ya mfumo huu wa kisekula wa kidemokrasia wanaweza kukulindeni kutokana na uovu wa Wakoloni wa Makafiri. Wote ni vibaraka wa Magharibi, na mtabadilisha kibaraka mmoja kwa mwingine ikiwa humtafanya kazi kubadilisha mfumo mzima wa kidemokrasia unaoungwa mkono na Magharibi. Matakwa yenu moja pekee yanapaswa kuwa kusimamisha tena dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Vyenginevyo, mtaendelea kuteseka katika dunia hii na pia katika Akhirah kwa kuzembea kwenu kutekeleza faradhi hii kubwa. Ni lazima mshirikiane bega kwa bega na chama cha kweli Hizb ut Tahrir ili Bangladesh iwe nukta kianzilishi cha kuregea Khilafah kama mlinzi wa Ummah.

Enyi Maafisa wenye ikhlasi katika Jeshi! Nyinyi ndio wana wa Ummah mnaobeba nguvu halisi na mnaoweza kuleta zama mpya zitakazomaliza udhalilifu, kujinyenyekesha, na ukosefu wa usalama kwa Ummah. Damu muibebayo kwenye mshipa yenu ni damu ya jenerali Sa’ad bin Muadh (ra) ambaye alimnusuru Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw) kusimamisha dola ya kwanza ya Kiislamu mjini Madina. Nyinyi ni kizazi cha shujaa mtukufu Salahuddin al Ayubi (r) aliyeuhuisha Ummah huu mtukufu kwa kuikomboa Al-Aqsa kwa njia ya Jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Babu zenu kamwe hawakufeli kuchukua fursa za kubadilisha ukandamizaji na udhalilishaji kwa ‘izzah (utukufu) wa Uislamu na Waislamu. Tunakulinganieni mtekeleze dori yenu muhimu leo ambapo mumekabidhiwa ubwana na usalama wa Ummah huu. Kutafuta kazi za kidunia kama vile maprofesa wa vyuo vikuu na wataalam wa taaluma hakuwezi kuwa lengo lenu wakati Mwenyezi Mungu Azza wa Jal anataka damu yenu na kujitolea kwenu kwa ajili ya kudhihiri Uislamu na Waislamu.

Tunawaonya kwamba ni haram waziwazi kuingia katika aina yoyote ya mapatano au miungano na maadui wapiganaji ambao kamwe hawasiti kuudhuru Ummah huu mtukufu. Kwa hiyo, ondoeni minyororo ya wakoloni na tawala zao bandia kutoka shingoni mwenu na mutoe Nussrah (msaada wa kimaada) kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha tena Khilafah Rashida iliyoahidiwa. Tunawakumbusha maneno matukufu ya swahaba mtukufu wa Mtume (saw) - Abdullah bin Rawaha (ra) wakati wa bay'ah yake ya Nussrah aliyoitoa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu katika mkutano wa kihistoria huko Aqabah kabla ya kusimamishwa kwa dola ya kwanza ya Kiislamu mjini Yathrib. Alipomuuliza Mtume (saw) malipo yao yatakuwa yapi kwa ajili ya kuilinda dola ya Kiislamu na kuihami dhidi ya vitisho vyovyote. Mtume (saw) aliwafahamisha kuhusu malipo makubwa yanayowasubiri Akhirah. Aliposikia hivyo, Abdullah bin Rawaha (ra) alijibu: “Biashara yenye faida (Ribh ul-bay’)! Hatutabatilisha wala hatutaomba kubatilishwa”.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu