Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
| H. 8 Rabi' II 1448 | Na: HTS 1448 / 41 |
| M. Jumapili, 20 Septemba 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan
Ulikutana na Mkuu wa Baraza la Kabila la Dar Hamar na Kiongozi wa Kabila la Kawahlah Jijini Khartoum
(Imetafsiriwa)
Mnamo Jumamosi, tarehe 7 Rabi’ al-Akhir 1448 H, sawia na tarehe 19/9/2026 M, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Sudan—ukiongozwa na Ustadh Nasser Ridha, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan, akiandamana na wajumbe wa Baraza la Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Sudan, Ustadh Mohiuddin Bukhari na Dkt. Ahmed Abdel-Fadil, pamoja na wanachama wa hizb, Ustadh Khalid Al-Jadia’, Fadlallah Ali Suleiman, na Abdel-Wahab Muhammad Abdel-Wahab—ulifanya ziara ya kwanza kukutana na Ustadh Abdel-Hay Safiuddin Najeh, Mkuu wa Baraza la Kabila la Dar Hamar, katika makazi yake yaliyoko mtaa wa Kober, Khartoum Kaskazini.
Mwanzoni mwa mkutano huo, Ustadh Abdul-Hay alizungumzia kuhusu vita nchini Sudan, athari zake kwa dola na jamii, pamoja na uharibifu mkubwa uliosababishwa na vita hivyo. Kisha, Ustadh Nasser alizungumza na kuelezea hatari ya njama iliyopangwa: uhamasishaji na uwekaji silaha mikononi mwa makabila, pamoja na kuchochea vita ambavyo vingesambaratisha nchi. Alisisitiza kuwa suluhisho linapatikana katika kufahamu mipango ya wakoloni makafiri na kufanya kazi ya kusimamisha dola ya Kiislamu—Khilafah Rashida—kwa njia ya Utume. Ustadh Abdul-Hay alisisitiza kuwa hakuna suluhisho jengine isipokuwa kupitia Uislamu, kama itikadi na sheria (Aqeedah na Shariah), kisha akaushukuru ujumbe huo kwa ziara yao.
Katika ziara yao ya pili, ujumbe huo ulikutana na Amiri wa Kabila la Kawahlah jijini Khartoum, Ustadh Muhammad al-Zayn Fadl al-Mawla Abu Hafs, nyumbani kwake eneo la al-Thawra, Omdurman. Mwanzoni mwa mkutano huo, Amiri wa Kabila la Kawahlah alizungumzia vita nchini Sudan na uhalifu uliofanywa na Vikosi vya Msaada wa Haraka, ikiwemo uporaji wa mali, huku akihusisha hali hiyo na kushindwa kwa watu kuregea kwenye Uislamu.
Kisha Ustadh Nasser Ridha alizungumza na kusisitiza kuwa vita hivyo vilikuwa vikiendeshwa na kuratibiwa kutoka nje ya nchi. Alionya dhidi ya hatari ya kuyavuta na kuyachochea makabila kujihami kwa misingi ya kikabila, akisema kuwa hatua hiyo itatumikia malengo ya wakoloni makafiri wanaotaka kuigawanya na kuisambaratisha nchi hii. Alisisitiza kuwa suluhisho liko katika Uislamu, hasa katika kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na akamtaka Amiri huyo kuunga mkono mradi wa Khilafah. Amiri alijibu, "Mradi tu mko pamoja na Uislamu, nasi tuko pamoja nanyi," akisisitiza umuhimu wa kuendeleza mawasiliano.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |



