Jumanne, 09 Ramadan 1445 | 2024/03/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  1 Rajab 1444 Na: 1444 H / 18
M.  Jumatatu, 23 Januari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali Inataka Kuudhuru Ulinganizi wa Khilafah kwa Kutumia Somoy TV Kuikashifu Hizb ut Tahrir kwa Habari za Uzushi

(Imetafsiriwa)

Ripoti ya habari ya Januari 17 katika Somoy News TV ya Bangladesh, ambayo mara kwa mara huwa kama msemaji wa serikali, ilidai kuwa Hizb ut Tahrir ina kile kinachoitwa uhusiano na mtu katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ambaye pia ana uhusiano wa karibu na balozi za nchi za Magharibi. Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilayah Bangladesh inalaani vikali 'uovu huo wa uandishi habari' wa kueneza uwongo wa kashfa kuhusu hizb ambayo haina rekodi ya kudumisha uhusiano wowote na balozi zozote, misheni za kidiplomasia au maafisa wao sio nchini Bangladesh wala katika sehemu yoyote ya ulimwengu ambako inafanya kazi, achilia mbali kupokea msaada wowote kutoka kwao. Tayari ni ukweli uliothibitishwa kwamba tangu kuanzishwa kwake mwaka 1953, Hizb ut Tahrir imekuwa ikiendesha mivutano ya kifikra na kisiasa ili kuzikomboa ardhi za Kiislamu ikiwemo Bangladesh kutoka mikononi mwa wakoloni wa Makafiri na kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kupitia kusimamisha tena Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hizb siku zote imekuwa ikifichua uingiliaji na njama za wazi za dola za kikoloni hususan Marekani na Uingereza katika nyanja zote zikiwemo siasa na uchumi wa nchi. Imekuwa ikiwaongoza watu mara kwa mara kuhusiana na njia za kufikia uhuru wa kweli na ukombozi kutoka kwa minyororo ya ukoloni mamboleo. Licha ya kukabiliwa na dhulma zisizo kifani, kukamatwa, kuhukumiwa, propaganda n.k. kutoka kwa mabeberu wa Kikafiri na watawala vibaraka wao kwa takriban miaka 70 ya mapambano yake ya kisiasa, Hizb ut Tahrir haijawahi kamwe kufanya maridhiano yoyote na dola yoyote ya kigeni au watawala wao vibaraka popote pale duniani. Hizb haikubali mfumo wa ulimwengu wa Magharibi na haiamini katika kubadilisha mamlaka kupitia uingiliaji kati wa balozi za kigeni au misheni za kidiplomasia. Bali, kando na kuunda rai jumla kwa ajili ya mfumo wa utawala wa Khilafah, inawataka maafisa wanyoofu wa kijeshi kuiondoa serikali inayotawala, na kutafuta nusrah (msaada wa kinguvu) kutoka kwao kusimamisha Khilafah ili kuondoa udhibiti wa kikoloni na utawala kutoka kwa ardhi za Kiislamu. Hizb ilikuwa tayari imeweka wazi msimamo wake wa kupinga ukoloni kwa wananchi na maafisa wa kijeshi wenye ikhlasi kama chama cha kisiasa chenye utaratibu, ikhlasi na ukweli. Lakini bado tunaona kutapatapa kwa serikali ya Hasina kuzuia da'wah ya Hizb ut Tahrir. Safari hii tumeona jaribio jengine la kutumia vyombo vya habari kuchafua sura ya Hizb ut Tahrir kwa kashfa zilizochochewa kisiasa baada ya kushindwa kujaribu kukihusisha chama hiki na misimamo mikali na uanamgambo siku chache zilizopita. Utawala huu dhalimu hauviruhusu vyombo vya habari kusimama na ukweli mbele ya taifa, bali unavilazimisha viwe kama mdomo wake ili viweze kudhuru ulinganizi wa Khilafah na kuchelewesha utabikishaji wa Shariah.

Enyi Waandishi wa Habari, je, si ujinga kweli kweli kubuni hadithi kuhusu kile kinachoitwa uhusiano wowote wa Hizb ut Tahrir na balozi za Magharibi wakati hizb imekuwa ikifichua ajenda za wakoloni wa Magharibi bila kuchoka! Munadai kuwa sehemu ya jamii yenye ufahamu zaidi, kwa hivyo munapaswa kujua vizuri zaidi njia ya Hizb ut Tahrir na ajenda ya kisiasa. Hizb ut Tahrir ni chama ambacho kinafanya kazi ndani na watu na kwa ajili ya watu. Kwa hivyo, jaribio lolote la kuichafua harakati hii yenye ikhlasi, ambayo ni sauti ya Ummah, litakuwa ni tendo lisilokomaa ambalo litaharibu kukubalika kwenu na kuaminiwa miongoni mwa watu. Kumbukeni, waongo wamelaaniwa na Mwenyezi Mungu (swt),

[إِنَّمَا يَفْتَرِي الْكَذِبَ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِ اللَّهِ وَأُولَئِكَ هُمُ الْكَاذِبُونَ]

Wanao zua uwongo ni wale tu wasio ziamini Ishara za MwenyeziMungu. Na hao ndio waongo.” [An-Nahl: 105]. Munapodai kuwa nyinyi ni kielelezo cha jamii, matakwa ya jamii yanapaswa kuonyeshwa katika habari zenu - kwamba watu katika taifa hili wanataka kuondokana na utawala dhalimu wa Hasina unaoungwa mkono na wakoloni wa Magharibi. Munapaswa kufichua mara kwa mara njama za kisiasa za kieneo za Magharibi ikiwa ni pamoja na kuingilia kwao nchini Bangladesh na ushirikiano wa wanasiasa wa kisekula wa nchi hii katika uhalifu huu.

Enyi Waandishi wa Habari! Nyinyi sio adui yetu. Nyinyi ni ndugu zetu. Wanaharakati wa Hizb ut Tahrir pia wanatoka katika jamii ile ile mliyomo, na mapambano yetu ya kisiasa yanapaswa kuelekezwa tu dhidi ya adui yetu wa pamoja - Wakoloni Makafiri. Kwa hivyo, tunatoa wito kwenu muchukue msimamo wa kijasiri na wa dhati dhidi ya utawala huu wa kikhiyana na kidhalimu. Jizuieni kutangaza uwongo wao ulioamriwa na kuwa kama vinywa vyao. Ikiwa hamuwezi kuwa mshiriki changamfu katika kazi ya kusimamisha Khilafah, basi angalau jiepusheni na kauli za uongo dhidi yake kwa amri ya serikali.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu