Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
H. 23 Dhu al-Hijjah 1446 | Na: H 1446 / 48 |
M. Alhamisi, 19 Juni 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mkataba wa Yunus-Tarique wa London ni Jaribio la Kudumisha Utawala wa Marekani na Mfumo wao Kandamizi wa Kisekula wa Kibepari
(Imetafsiriwa)
Mnmo tarehe 13 Juni 2025, mkuu wa serikali ya mpito Dkt. Yunus, akiwa amkeketi jijini London, amewakatisha tamaa wananchi kwa kufanya maridhiano ya kisiasa na Tarique Rahman, kaimu mwenyekiti wa BNP (Bangladesh Nationalist Party) kwa sababu watu wa nchi hii hawajasahau historia ya utawala mbaya na ufisadi wa matabaka tawala ya BNP. Kwa hakika, maridhiano haya ya kisiasa ya Yunus-Tarique na kugawanya madaraka ni sehemu ya mpango wa Marekani, ambao kupitia kwao wataweza kutekeleza miradi ya kikoloni. Mumeshuhudia kwamba waliokuwa mabalozi wa Marekani Dan Mozena, Bernicat na Peter Hass, wote wamekaribisha maridhiano haya na kuonesha kuridhika, na kwa mujibu wa taarifa za habari, BNP pia imependekeza kumfanya Dkt. Yunus kuwa rais. Kupitia kuanguka kwa dhalimu Hasina, watu wa nchi hii walionyesha nia yao ya kutaka kuwa huru kutokana na mfumo dhalimu wa kibepari na kutawaliwa na Wakoloni makafiri wa Magharibi. Aina hii ya maridhiano si lolote bali ni usaliti kwa watu wa nchi hii.
Sisi, kwa niaba ya Hizb ut Tahrir, tunataka kuitahadharisha serikali ya mpito na jukwaa la kisiasa kwamba watu wa nchi hii kamwe hawatavumilia njama zozote za kuanzisha utawala wa dola za Kikafiri-Kishirikina katika ardhi hii ya Kiislamu. Wanapaswa kujifunza somo kutokana na kuanguka kwa mtawala Hasina aliyechukiwa. Mwenyezi Mungu (swt) asema,
[الَّذِينَ يَتَّخِذُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِنْ دُونِ الْمُؤْمِنِينَ أَيَبْتَغُونَ عِنْدَهُمُ الْعِزَّةَ فَإِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا]
“Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je! Wanataka wapate kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.” [Surah An-Nisa: 139]. Kwa hiyo, serikali ya mpito inapaswa kutengeneza mazingira sahihi ya kisiasa ili kufikia mwafaka wa kisiasa unaoegemezwa juu ya Uislamu, maslahi ya watu na kulinda ubwana wa nchi, ili matumaini na matarajio ya wananchi yaonekane na kutimizwa kikweli. Mwenyezi Mungu (swt) asema,
[إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ وَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ]
“Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemewe.” [Surah Al-Hujurat: 10]. Kwa hiyo tunapaswa kuwaunganisha watu kwa kusahau tofauti zetu, na kuwakataa makafiri na washirikina.
Enyi watu, baada ya miaka kumi na tano ya harakati, mapambano na mihanga mingi, mumemshusha dhalimu Hasina, matunda ya mfumo wa Kisekula wa Kibepari. Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (ra) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema «لَا يُلْدَغُ الْمُؤْمِنُ مِنْ جُحْرٍ مَرَّتَينِ» “Muumini hang’atwi mara mbili kutoka tundu moja” [Sahih Bukhari na Muslim]. Kwa hivyo, hampaswi kung’atwa tena kutoka tundu lile lile la mfumo wa kibepari wa kisekula kupitia maridhiano ya kisiasa na kugawanya madaraka miongoni mwa matabaka tawala tiifu kwa Magharibi, hasa Amerika. Ni lazima tukatae sarakasi ya kile kinachojulikana kama mageuzi ya serikali na kuwa wachangamfu katika mabadiliko ya kina ya serikali. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «... ثم تكون ملكًا جبرية فتكون ما شاء اللّه أن تكون، ثم يرفعها إذا شاء أن يرفعها، ثم تكون خلافة على منهاج نبوة. ثم سكت» “kisha utakuwepo utawala wa dhulma, utakuwepo kwa muda atakao Mwenyezi Mungu uwepo kisha atauondoa apendapo kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume” [Musnad Ahmad]. Kwa lengo la kutekeleza bishara njema hii ya Mtume (saw), ni lazima tusimamishe umoja wa kisiasa ili kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Ni kwa kusimamisha Khilafah pekee, Uislamu, maslahi ya Umma wa Kiislamu, na ubwana wa ardhi za Kiislamu yatalindwa, Insha'Allah.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.”[Surah Al-Anfal: 24].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Bangladesh |
Address & Website Tel: +88 01798 367 640 www.ht-bangladesh.info |
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd |