Alhamisi, 28 Jumada al-thani 1447 | 2025/12/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari

H.  1 Muharram 1360 Na:
M.  Jumanne, 18 Novemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

‘Mkataba wa Mageuzi ya Julai: Udanganyifu Mkubwa’:
Hizb ut Tahrir Yalaani Mkataba huo, na Kuhimiza Badali Msingi ya Kisiasa kwa Demokrasia Iliyofeli

(Imetafsiriwa)

Katika kujibu hotuba ya hivi karibuni ya Mshauri Mkuu Profesa Yunus kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Kitaifa wa Julai na kura ya maoni kuhusu mapendekezo ya mageuzi ya katiba katika Mkataba huo, Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh inatoa onyo kali kwamba mapendekezo ya mageuzi na mchakato wake wa utekelezaji si kitu zaidi ya hatua ya juu juu ambayo inashindwa kushughulikia sababu za msingi za mgogoro wa kisiasa wa Bangladesh. Inatoa udanganyifu wa mabadiliko ili kuhifadhi dhati ya mfumo wa kidemokrasia uliofeli. Mkataba huo, ambao unaahidi mipaka ya muda, taasisi zilizoimarishwa, na uangalizi na uwajibikaji, unawasilishwa kama suluhisho kwa miongo kadhaa ya utawala wa kimabavu. Hata hivyo, mfumo huu unaendeleza tu mfumo ule ule wa kidemokrasia uliofeli chini ya kivuli kipya. Unasema kwamba kubadilisha muundo ambao umewaruhusu kipote cha wanaoungwa mkono na Magharibi kudumisha madaraka – chini ya BAKSAL, utawala wa kijeshi, na kinachoitwa serikali za kidemokrasia – ni kama kupanga upya viti vya deki kwenye Titaniki.

Mkataba wa Julai, pamoja na mipango yake tata ya uangalizi na uwajibikaji na nguvu ya kusawazisha kati ya rais na waziri mkuu, inafichua kasoro ya asili ya mfumo wa kidemokrasia wenyewe. Kwa mfano, majaji wasiochaguliwa, ambao nguvu zao zinatokana na sheria zilizotungwa na wanasiasa waliochaguliwa, wanawezaje kuwawajibisha wanasiasa hao kikweli? Ni utani wa mviringo. Na ikiwa rais na bunge wote watachaguliwa, mgongano wao usioepukika wa maslahi husababisha mgongano na kufungwa tunakoona katika mfano tunaoambiwa kuiga: Marekani.

Hivyo, Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh inahimiza kwa nguvu makundi ya kisiasa yenye ikhlasi ya Bangladesh kujitenga na utumwa huu wa kifikra na kwa ujasiri kutafuta njia badali ya kweli. Lazima wapate ujasiri wa kuhoji uhalali wa mfumo ambao umetuangusha kila mara. Mabadiliko ya kweli hayatatokana na katiba mpya ndani ya mfumo ule ule uliovunjika, bali kutokana na kufikiria upya kimsingi utaratibu wa kisiasa unaowahudumia watu kweli, huru kutokana na minyororo ya udanganyifu ya fikra ya kati na kati ya kidemokrasia. Watu walitaka mabadiliko ya kweli baada ya kuanguka kwa Hasina, lakini suluhisho linalotolewa ni kurudi kwenye mfumo ule ule wa kidemokrasia wenye dosari uliowaangusha. Wanasiasa na wasomi lazima wajiulize: baada ya kujitolea sana, kwa nini kutafuta majibu katika mfumo ambao umetusaliti kila mara? Kwa nini hofu ya kuwapinga Wamagharibi, dola zile zile zilizounga mkono udhalimu wa Hasina? Hawakutusaidia wakati huo; kwa nini mufuate mpango wao sasa? Kwa kuufunga mjadala kwenye mfumo huu uliovunjika, wanasaliti damu na jasho la wale waliopigania mabadiliko ya kweli. Ni wakati sasa wa kujadili mfumo wa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Huu si muundo wa kiromantiki, bali ni suluhisho la kivitendo na lililo tayari. Hizb ut Tahrir inatangaza kwamba imejiandaa kikamilifu na katiba kamili na ya kina kwa mfumo wa Khilafah unaoegemea Hukm Shariah. Mfumo huu hutoa sera kamili kwa nyanja zote za utawala, ikiwemo uchumi, haki, ustawi wa jamii, usalama wa kitaifa, na mahusiano ya kigeni. Hebu na tungane pamoja kuleta mabadiliko ya kweli chini ya Khilafah Rashida, tukitimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw), na kupinga mfumo wa kilimwengu wa Kimagharibi wenye utata ambao umetuletea tu ukandamizaji na mateso.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu