Jumatatu, 28 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Denmark

H.  25 Rabi' II 1447 Na: 03 / 1447 H
M.  Ijumaa, 17 Oktoba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Usaidizi kwa Mauaji ya Halaiki ndio Jinai – Sio Wito wa Ukombozi

(Imetafsiriwa)

Leo, Ijumaa, Oktoba 17, 2025, nimeachiliwa huru na Mahakama ya Kitaifa kufuatia kutiwa hatiani katika Mahakama ya Jiji kwa kutoa wito wa ukombozi wa Palestina.

Hotuba yangu katika maandamano ya Mei 2021 mbele ya ubalozi wa Misri, ambapo nilitoa wito kwa majeshi ya Waislamu kuja kuwaokoa wanaume, wanawake na watoto wanaodhulumiwa mjini Gaza, ilikuwa, kwa mujibu wa hukumu ya Mahakama ya Jiji la Copenhagen kuanzia Juni 2024, ilikuwa ya kihalifu.

Ilithibitishwa katika Mahakama ya Jiji pamoja na Mahakama Kuu kwamba hotuba hiyo haikuelekezwa kwa Mayahudi, bali ilitoa wito wa kuondolewa kwa umbile haramu la Kizayuni liitwalo “Israel” kupitia mapambano ya silaha.

Uamuzi wa Mahakama ya Jiji kwa hivyo uliufanya wito wa ukombozi wa Palestina kuwa wa kihalifu moja kwa moja, huku madai ya upande wa mashtaka yaliyochakaa ya chuki dhidi ya Mayahudi yakiporomoka haraka.

Hukumu hiyo ilibatilishwa leo kwa sababu haikuwa na hoja na haina msingi wa kisheria. Hata hivyo, ilikuwa ni sehemu ya mkondo wa kisiasa wa hukumu za ghafla dhidi ya wapinzani wa uvamizi wa Kizayuni wa Palestina.

Ni fedheha kwa mfumo wa mahakama wa Denmark kwamba kesi hii ilifikia hata Mahakama Kuu kabla ya kutupiliwa mbali, na kwamba mahakama imepotoshwa kwa kiwango kama hicho cha juu sana ili kulinda umbile la mauaji ya halaiki la Mazayuni na uungaji mkono usio na masharti wa dola ya Denmark kwa ajili yake.

Jaji katika Mahakama Kuu kwa hali hii alikataa kusalitiwa na shinikizo kubwa lililotolewa na serikali, ambayo imewahimiza hadharani polisi na upande wa mashtaka kumfungulia mashtaka mtu yeyote anayetoa wito wa ukombozi wa Palestina.

Ingawa hivi sasa nimeachiliwa huru, haiwezi kupuuzwa kwamba kumekuwa na msururu mrefu wa hukumu za kisiasa dhidi ya raia ambao wametoa wito wa – au kuidhinisha – upinzani wa silaha dhidi ya uvamizi wa Kizayuni. Katika kesi moja, hata ilisababisha kufutwa kwa uraia!

Utiaji uhalifuni huu na kufunguliwa mashtaka kwa watu kwa misimamo yao ya kisiasa dhidi ya uvamizi wa kijeshi unaofanya mauaji ya halaiki kwa kutumia vyombo vya silaha vya Denmark si lolote ila majaribio ya vitisho yasiyokubalika. Lakini hatua hiyo imepita mkondo wake. Kesi za kisiasa au la – wito wa ukombozi wa kweli wa Palestina hauwezi kuzuiwa. Ni wazi zaidi leo kuliko wakati mwengine wowote kwamba saratani ya uvamizi kijeshi wa Wazayuni, ugaidi wa kiserikali, mauaji ya watu wengi, mateso, wizi wa ardhi, na mauaji ya kikabila lazima yakomeshwe kupitia ukombozi wa kijeshi – mtazamo ambao unapata uungwaji mkono kote duniani kama suluhisho pekee la kweli.

Sisi, katika Hizb ut Tahrir/Denmark, tunatoa wito kwa kila mtu aliye na adabu thabiti kuendeleza upinzani dhidi ya uungaji mkono wa serikali ya Denmark kwa koloni ya walowezi ya Kizayuni na mipango yake inayoendelea ya kuwaangamiza Wapalestina.

Tunatoa wito makhsusi kwa ndugu na dada zetu Waislamu kufanya kazi kwa azma na subira kubwa zaidi kwa ajili ya kutokomeza kabisa uvamizi na ukombozi wa Palestina kupitia majeshi ya ulimwengu wa Kiislamu.

Wito wa ukombozi wa Palestina si uhalifu, bali ni wajibu na heshima. Serikali ya Denmark ndiyo inayotenda kwa uhalifu katika kuunga mkono koloni ya walowezi wa mauaji ya halaiki.

Elias Lamrabet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Denmark

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Denmark
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu