Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  3 Safar 1444 Na: 1444 / 02
M.  Jumanne, 30 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Iraq kutoka kwa Mkwamo wa Kisiasa Hadi Hatima Isojulikana
(Imetafsiriwa)

Tangu uchaguzi wa Oktoba mwaka jana, Iraq imeingia katika mzunguko wa mvutano wa kisiasa, kutokana na mzozo wa Mashiya kwa Mashiya kuhusu aina ya serikali kati ya wengi wanaopigiwa debe na vuguvugu la Sadri, na ushirikiano unaolinganiwa na Mfumo wa Uratibu. Kisha mandhari ikwa ngumu zaidi wakati mfumo wa uratibu ulipoanzisha chaguo la tatu la kuzuia, ambalo lilizuia kuchaguliwa Rais wa Jamhuri, na kisha kuvuruga uteuzi wa Waziri Mkuu na uundaji wa serikali.

Muqtada al-Sadr hakufanya lolote ila kuwaagiza manaibu wake wa sasa kujiondoa katika mchakato wa kisiasa, kisha kuingia barabarani na kulivamia bunge la Iraq, na kukataa wito wa mazungumzo, chini ya kauli mbiu: Hakuna mazungumzo na wafisadi; na hivyo hali ya Iraq ikawa imepotea na kuchanganyikiwa.

Hadi mhubiri wa Kishiya Kazem Al-Haeri alipotangaza mnamo Jumatatu, Agosti 29, 2022, kustaafu kwake kutoka katika kazi ya maregeo, na pendekezo la kufuata maregeo ya Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Iran, akihalalisha hili kwa afya yake mbaya na umri mkubwa yanayomzuia kutekeleza majukumu ya maregeo, na akasema katika kauli yake: “Waumini wote mtiini Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Mtukufu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, kivuli chake kiwe kirefu (yaani umri mrefu), mtukufu yeye ndiye mbora na mwenye sifa za kuliongoza taifa hili na kusimamia mapambano na nguvu za dhulma na kiburi katika dhurufu hizi ambazo kwazo nguvu za ukafiri na uovu zinapigana dhidi ya Uislamu sahihi wa Muhammad.”

Hili linadhihirisha wazi shinikizo la Wairan kwa Al-Haeri kuachana na Muqtada Al-Sadr, ambaye ndiye maregeo yake, na hilo lilikuwa bayana katika kauli yake, ambapo alisema: “Watoto wa mashahidi wawili, Mwenyezi Mungu aitakase siri yao, lazima wajue kwamba mapenzi ya mashahidi wawili hayatoshi isipokuwa imani iambatane na mfikio wao kwa kazi nzuri na kushikamana kwa kweli na malengo yao ambayo walijitolea kwa ajili yake. Kudai tu au ushirikishwaji pekee hautoshi, na anayetaka kuwatenganisha watu na dhehebu kwa jina la mashahidi wawili, Mwenyezi Mungu awawie radhi, au kuuhutubia uongozi kwa jina lao hali yeye hana fiqhi au masharti mengineyo yanayohitajika kwa uongozi halali ni - kwa kweli - sio mwana Sadri, namna anavyodai au uhusiano wake naye.”

Jibu la Al-Sadr kwa uamuzi huu lilikuwa ni kutangaza kustaafu kwake kwa mwisho kutoka kwa masuala ya kisiasa katika nukuu ya tweet kwake kwenye Twitter, na alisema: "Watu wengi, ikiwemo Bw. Al-Haeri, Mungu ampe umri mrefu, wanafikiri kwamba uongozi huu ulikuja kupitia shukrani kwao au kupitia amri. Hapana, hayo yote ni kwa fadhila za Mola wangu Mlezi, na kutoka kwa baraka za babangu, aliyeitakasa siri yake, ambaye hakuitelekeza Iraq na watu wake. Ameongeza kuwa: "Najaf al-Ashraf ndio makao makuu makubwa zaidi ya mamlaka ya kidini, kama ilivyo siku zote," na akasisitiza kwamba uamuzi wa Al-Hairi haukuwa kwa hiari yake mwenyewe, kwa kuashiria wazi shinikizo la Iran.

Kutokana na kauli hizo nchi iliingia katika machafuko makubwa, huku waandamanaji wakivamia Kasri la Jamhuri, na maelfu ya waandamanaji wakatoka katika mikoa mengine, na amri ya kutotoka nje ikatangazwa nchi nzima kuanzia saa moja jioni, hadi taarifa zaidi zitakapotolewa, na Al Sharqiya TV iliripoti kwamba "Al-Kazemi inasimamia uwekaji wa usalama. Na jeshi linaloshughulikia maandamano ya kijani kibichi."

Kutokana na hayo yaliyotangulia, matukio haya ya kasi yanaipeleka nchi kwenye utata zaidi ambao hauondoi uwezekano wa mapigano, na hivi ndivyo Amerika inavyoweka kamari, ili basi icheze dori ya mwokozi kulazimisha masuluhisho yanayotumikia maslahi na miradi yeke katika kanda hii.

Enyi Waislamu nchini Iraq:

Tumeshawahi kuwaambia, na tumewaekeeni wazi mara kwa mara, kwamba dola vamizi za kigeni na wapambe wao katika dola za eneo hili na kambi za kisiasa zinazokutawaleni, hazijali kuhusu nyinyi, hazijali kuhusu shida zenu au mateso yenu, na wasiwasi wao pekee ni maslahi yao, na yale mnayoyaona leo ya wafu na waliojeruhiwa miongoni mwa safu zenu ni ushahidi bora kabisa kwamba wao hawajali ni bonde gani mtaangamia. Mandhari ya kisiasa ya Iraq si yenye kutokea kwa ghafla, bali ni kitendo changamfu, ambacho kwacho inataka kufikia maslahi yake na kutekeleza mipango yake.

Enyi Waislamu:

Kujitolea muhanga huku hakukuwa bure bilashi, kwani wengine wamekwenda, isipokuwa watambue uhalisia wa tatizo na uhalisia wa suluhisho. Uhalisia wa tatizo ni mfumo wa kisiasa na katiba yake iliyolazimishwa na mvamizi wa Kimarekani, ambazo kwazo kasumba ya madhehebu na ukabila imekita mizizi nchini humo, na mandhari hii ya kutisha itaendelea kubakia nchini humu, maadamu mfumo huu wa kidemokrasia utaendelea kuwepo. Mfisadi anayemfanya mwanadamu kuwa mtunzi wa sheria badala ya Mwenyezi Mungu ndiye anayedhibiti hatima ya watu.

Uhalisia wa tiba ni kwa Ummah kufahamu kuwa kasoro iko katika mfumo huu, kwa hiyo uasi dhidi yake na kuweka mahali pake mfumo ambao ubwana uko kwa Muumba peke yake, mfumo wa haki wa wanadamu, ambao ndani yake hakuna upendeleo kwa Mwarabu juu ya asiyekuwa Mwarabu, wala mweupe juu ya mweusi isipokuwa kwa uchamungu. Ummah unajua ulichonacho na unachodaiwa, na mtawala anajua kile ambacho Mwenyezi Mungu amemkabidhi katika kutabikisha sheria yake, na kwamba yeye ni mchungaji aliyepewa dhamana na Mwenyezi Mungu na atamuuliza juu ya kile alichomdhamini, kwa mujibu wa yale aliyoyasema (saw):

«كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ؛ فَالْأَمِيرُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ عَلَيْهِمْ وَهُوَ مَسْؤُولٌ عَنْهُمْ...»

“Nyote ni wachungaji na kila mmoja ataulizwa alichokichunga. Amiri anayewaongoza watu ni mchungaji na ataulizwa juu yao …” [Sahih].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu