Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Jordan kwenda kwa vitivo vya Sharia na Waandaaji wa Kongamano la "Uhalisia wa Maji Nchini Jordan"
- Imepeperushwa katika Jordan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Chini ya uangalizi wa Waziri wa Wakfu na Masuala ya Matukufu ya Kiislamu, Dkt Muhammad Al-Khalayleh, vitivo vya Sharia katika vyuo vikuu vya Jordan, kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ), watafanya kongamano la kwanza kwa wanafunzi wa vitivo vya Sharia katika vyuo vikuu vya Jordan chini ya anwani: "Uhalisia wa maji nchini Jordan ... Changamoto na Masuluhisho kutoka kwa Mtazamo wa Kiisilamu." Ambalo litafanyika kwa kutumia programu ya Zoom mnamo Jumamosi tarehe 12/12/2020.