Alhamisi, 13 Dhu al-Qi'dah 1442 | 2021/06/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  28 Sha'aban 1442 Na: 21/1442
M.  Jumamosi, 10 Aprili 2021

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi

Hajj Zidan Abdel Fattah Masoudi (Abu Tayseer Masoudi)

﴿مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً﴾

"Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo." [Al-Ahzab: 23]

(Imetafsiriwa)

Hizb ut-Tahrir katika Wilayah ya Jordan anamuomboleza mbebaji da'wah, Hajj Zaidan Abdel Fattah Masoudi (Abu Tayseer Masoudi), ambaye alikwenda katika rehema ya Mwenyezi Mungu (swt) akiwa na umri wa miaka 84 ambao aliutumia katika kumtii Mwenyezi Mungu na kubeba ulinganizi wa kurudisha tena maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Hajj Zaidan Abdel-Fattah Masoudi, Mwenyezi Mungu amrehemu, aliubeba ulinganizi wa kuregesha tena maisha ya Kiislamu katika safu za Hizb ut Tahrir tangu miaka ya hamsini ya karne iliyopita na alikutana na aliyoyakuta katika mateso na kifungo gerezani mikononi mwa madhalimu, alifungwa jela mara nne katika njia ya faradhi hii kubwa, na dhulma yao haikumzuia kuendelea na njia hii na akabakia imara mithili ya milima Al-Rasayyat, akichunga ubebaji ulinganizi kokote aendako, wala umri wake na ukosefu wa nguvu havikumfunga juu ya hilo, akitumaini kwamba Mwenyezi Mungu amshuhudishe Khilafah, mpaka amri ya Mwenyezi Mungu ilipokuja na hali yeye yuko juu ya hilo, na roho yake ikatiririka kwenda kwa mwenye haki yake.

Tunamwomba Mwenyezi Mungu amfinike kwa rehema yake pana na amuingize katika pepe zake kubwa na amlipe kwa niaba yetu na Uislamu na Waislamu malipo bora, na hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutaregea.

Ni cha Mwenyezi Mungu kile alichotoa, na ni cha Mwenyezi Mungu kile alichokichukua, na hatusemi ila yale yanayomridhisha Mola wetu (swt), kwani hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutaregea.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Katika Wilayah ya Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu