Inatosha Inatosha, Hali Haivumiliki Tena Baada ya Mauaji ya Mahema, Ni Kipi chengine Kitausukuma Ummah na Majeshi yake?!
- Imepeperushwa katika Kitengo cha Wanawake Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo siku ya Jumatatu, tarehe 27/5/2024, Wizara ya Afya huko Gaza ilitangaza kwamba idadi ya waliouawa kutokana na mauaji yaliyofanywa na vikosi vya uvamizi dhidi ya waliokimbia makaazi yao katika kambi ya mji wa Rafah imeongezeka hadi 45, wakiwemo wanawake 23, watoto na wazee, na waliojeruhiwa kufikia 249.