Jumatano, 18 Sha'aban 1445 | 2024/02/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  28 Jumada I 1440 Na: 1440/015
M.  Jumatatu, 04 Februari 2019

Taarifa kwa Vyombo vya Habari


Jinsi Siasa Inavyo Fanana na Zamani … Matukio Yanaendelea Kama Wanavyo Endelea Watazamaji!

(Imetafsiriwa)

Wanajeshi madhalimu wa umbile la Kiyahudi walimuua msichana kutoka Palestina kwa kummiminia risasi katika kituo cha upekuzi cha al-Za’im, mashariki mwa ardhi iliyo kaliwa Al-Quds (Jerusalem). Shahidi huyo ni mwanafunzi wa shule ya upili aliyekuwa amebeba mkoba wake wa shule wakati wa kuuwawa kwake; aliuwawa kutokana na madai ya kujaribu kutekeleza oparesheni ya kudunga kisu. Majeshi hayo vamizi yalizuia wahudumu wa ambulensi kutomfikia ili kumpa tiba. Aliachwa kuvuja damu hadi kufa.   

Uhalifu mwengine umeongezeka katika msururu wa uhalifu na mauwaji yanayo ashiria ugaidi na unyama wa umbile hilo la Kiyahudi dhidi ya watu wa Palestina, vijana wa kiume na wa kike, wazee na watoto, ambalo huhalalisha kwa madai ya kirongo na visingizio vya tayari vya kirongo, yaani jaribio la kudunga kisu. Hatukusikia wala kuona kelele wala fujo kutoka kwa watetezi wa haki za kibinadamu na wanaharakati wa haki za watoto na wanawake, wala za serikali za fedheha katika biladi za Kiislamu. Shahidi huyo, Samah Mubarak, Allah (swt) amrehemu, alikuwa chini ya umri wa miaka 16 na alikuwa amebeba tu vitabu na madaftari yake, na imani na itikadi yake moyoni mwake na katika suluki yake. Hii ilimfanya kutovua niqab usoni mwake, kitu kilichotia hofu nyoyoni mwao ambacho kilimfanya kwa mtazamo wao kustahiki kuuliwa na kuachwa kuvuja damu hadi kufa!! Hata video zilizo chapishwa zilionyesha tu msichana mwenye niqab akiingia katika kituo hicho cha upekuzi, na kisha wakampiga risasi kwa karibu, pasi na kosa wala uhalifu bali kutokana na niqab yake. Kisha wakadai kuwa alijaribu kumdunga kisu mmoja wao! Namna gani leo inavyo fanana na jana, pindi walipomuua Hadeel Al-Hashlamon, Allah amrehemu, miaka michache iliyopita kwa sababu hiyo hiyo na mandhari na tukio kama hilo!  

Uhalifu huu umesadifu kwa kutolewa taarifa na ule unaoitwa Muungano wa Dola za Kiarabu, ambao ulithibitisha usaidizi wake kamili kwa haki za Wapalestina za 1948 na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa, Umoja wa Mataifa na Baraza la Haki za Kibinadamu kubeba majukumu mabegani mwao kwa ajili yao!! Kamwe hatukusikia, shutuma, kupinga, au hata risala za rambi rambi kutoka kwa tawala za aibu na fedheha, lakini pindi mlowezi au mwanajeshi mvamizi wa Kiyahudi anapouliwa, haupumziki hadi umsalimishe yule aliyetekeleza kitendo hicho kwa Mayahudi … Ni maovu kiasi gani wanayo yafanya!

Enyi Watu wa Ardhi Tukufu (Palestina),

Mpaka lini kimya na kuvunjwa moyo kutabakia juu ya mamlaka haya, ambayo yanawatumikia Mayahudi kwa mipango yao yote ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kifikra na kithaqafa!! Mpaka lini mutabakia kimya juu ya mamlaka haya, mkusanyaji ushuru na sio msimamizi! Haya ni mamlaka kibaraka na mkono wa usalama wa Mayahudi!! Je, sasa sio wakati wa nyinyi kutafuta suluhisho sahihi, ambalo litawang’oa Mayahudi na kuikomboa ardhi hii na kuleta utukufu? Hakuna mashirika, wala makongamano, wala taarifa, wala serikali vibaraka, na watawala makhaini, waliouza uwezo na rasilimali za Ummah kwa thamani duni, watakao wanufaisha nyinyi. Ni dola yenye nguvu pekee inayotawala kwa Uislamu ndio itakayo rudisha haki kwa wenyewe na kulinda wanawake, watoto, wazee na vijana. Dola hii ni Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo itampiga kwa mkono wa chuma kila mhalifu asiye tukuza kizazi na mikataba pamoja na waumini. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

  فَسَوْفَ يَأْتِي اللهُ بِقَوْمٍ يُحِبُهُمْ وَيُحِبُونَهُ أَذِلَةً عَلَى الْمُؤمِنِينَ أَعِزَةٍ عَلَى الكَافِرينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ الله وَلا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لائِمٍ ذَلِكّ فَضْلُ اللهِ يُؤتِيهِ مَنْ يَشَاءُ وَاللهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ﴿

“… basi Mwenyezi Mungu ataleta watu anao wapenda nao wanampenda, wanyenyekevu kwa Waumini na wenye nguvu juu ya makafiri, wanapigana Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu wala hawaogopi lawama ya mwenye kulaumu. Hiyo ndiyo fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu Mwenye kujua” [Al-Ma’ida: 54]

Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu