Jumamosi, 11 Shawwal 1445 | 2024/04/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  14 Sha'aban 1445 Na: 1445 H / 025
M.  Jumamosi, 24 Februari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mateso ya Wanawake wa Gaza Waliodhulumiwa, je wana Mlipizaji Kisasi? na je Umma wa Kiislamu Umepoteza Mu’tasem wake?!
(Imetafsiriwa)

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ilifichua mnamo Jumatatu kwamba idadi kadhaa ya wanawake na wasichana katika Ukanda wa Gaza wamebakwa na jeshi la Kiyahudi linalokalia kwa mabavu. Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema leo kuwa wataalamu wake wana wasiwasi kuhusu ripoti zinazoonyesha kuwa wanawake na wasichana wa Kipalestina wanaoshikiliwa mateka wamekuwa wakifanyiwa vitendo mbalimbali vya unyanyasaji wa kingono. Umoja wa Mataifa ulisema kwamba kuna ripoti zilizo nakiliwa za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ambao wanawake na wasichana wa Kipalestina wanaendelea kukabiliana nao huko Gaza na Ukingo wa Magharibi. (Mtandao wa Quds, 19/02/2024)

Ni jambo la aibu kwamba habari hizi zinafichua kwamba wataalamu kutoka Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa "wakionyesha wasiwasi" na Kamishna huyo anahisi "kusikitishwa hasa" na ripoti zinazoonyesha kuwa wanawake na wasichana wa Kipalestina wanaoshikiliwa na vikosi vya uvamizi wamekuwa wakivuliwa nguo na kupekuliwa na maafisa wa jeshi la uvamizi.

Ni fedheha juu ya Umma wa Kiislamu kwamba mashirika haya ya kimataifa, yaliyotokana na uzao wa mfumo wa kibepari, yana wasiwasi na huzuni juu ya ripoti hizi wakati Umma wa Kiislamu ukiwa katika usingizi mzito, uliozoea matukio haya ya kuogofya na vilio vikali bila ya kuchochea hatua!

Ni jambo la kufedhehesha kwamba mashirika haya ya kimataifa kwa mara nyengine tena yanatumia wasiwasi na huzuni zao - zile ambazo zimeacha vita huko Gaza na kufichua unafiki wa kauli mbiu zao na vyeo vyao vya kifahari wanavyoviinua - huku wanawake wa Kiislamu wakidhulumiwa na kukanyagwa utu wao bila ya damu kuchemka katika mishipa ya wanaume wa Ummah huu!

Inatia uchungu kwamba Umma wa Kiislamu umepoteza mwelekeo kwa haya yanayotokea, na inasikitisha kwamba umezoea kushuhudia maafa na mauaji ya halaiki ya watoto wake bila ya kuitisha hatua kutoka kwa watawala wake... Bali inasikitisha kwamba umbile hili nyakuzi linaendelea kuwadhalilisha watu wa Gaza kwa kuwaua kwa njaa, kuwadhulumu, kuwabomolea nyumba zao, kuwahamisha na leo hii, kusubutu kuwavunjia heshima wanawake...

Enyi Umma wa Kiislamu: hawa ni dada zenu wanaotaka msaada wenu, basi mwitiko wenu wa wito wao uko wapi? Wanaume wako wapi, na kwa nini kimya hiki cha kuchukiza? Ikiwa hamkasiriki kwa heshima yenu na utu wa binti zenu na wanawake unaovunjwa na wahalifu hawa, basi ni lini mutakasirika?! Ikiwa vilio na maombi yao hayakutingisini, basi lini mutatingiswa?!

Enyi Umma wa Kiislamu: Gaza inaangamizwa, kila siku inashuhudia mauaji mabaya zaidi kuliko yale yaliyotangulia, huku watu wa Ummah wamekaa bila kuchukua hatua! Laiti damu yao ingetiririka tena katika mishipa yao, ili waweze kufufuka, kutoa na kutetea kwa ukali utu wao!

Simameni, enyi Umma wa Kiislamu, na muelekee kwa wale watawala wasaliti ambao ni kivuli cha umbile hili halifu, lilifinikwa na kivuli chao na kulindwa nao. Bomoeni viti vyao vya enzi, kwani pindi kivuli kinapoondoka, vilevile umbile hili la ovu litaondoka. linganieni dola itakayowakusanya watu wenu waliotawanyika na kuunganisha sauti yenu!

Na Enyi Wanazuoni wa Umma wa Kiislamu, Enyi Warithi wa Mitume: mko wapi kuhusiana na yanayowasibu wanawake wa Gaza?! Wallahi mtahisabiwa kwa kunyamaza kwenu na uzembe wenu... Mtakabiliana kutoka kwa Mwenyezi Mungu na yale mnayostahiki kwa kushindwa kwenu kuuongoza Umma wa Mtume wenu kwenye njia ya wokovu kutokana na udhalilifu na udhaifu unaoruhusu viumbe wanaochukiza zaidi kusubutu kuwakiuka wanawake wake! Semeni neno lenu, wala musiogope kulaumiwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na fuateni mfano wa wanazuoni watukufu na wenye ikhlasi wa Ummah huu, ambao majina yao hayafi, na waliopata utukufu, daraja ya juu, na radhi za Mwenyezi Mungu wao na Jannat (pepo).

Enyi Wanachuoni: Vita vya Gaza ni vita vya Aqida, vita vya msalaba dhidi ya Uislamu, basi ni kipi mlichotoa kwa ajili ya Dini yenu? Je, bado humjainusuru?

Vita hivi vimeonyesha kuwa taifa la ukafiri limeungana na kukimbilia kusimama pamoja na umbile hili nyakuzi, ambalo limepandikizwa katika moyo wa Umma ili kuzuia umoja wake na kuzuia mkusanyiko wake chini ya Raya moja inayotawaliwa na Imam mmoja anayeitekeleza Sheria ya Mola wake Mlezi... Ni vita ambavyo adui kafiri ametayarisha majeshi kwa ajili ya  ushindi wa jeshi la Mayahudi ambalo lilisemekana kuwa ni "jeshi lisiloshindika," lakini Operesheni Kimbunga cha Al-Aqsa ililifichua kama jeshi la katuni linalolikejeli na uwezo wake...

Taifa la ukafiri linataka kuhifadhi fahari ya umbile hili "lililooza", hivyo limetayarisha vifaa na nguvukazi kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa watu wasio na hatia wa Gaza. Hapa kuna Marekani, kwa mfano, ikipuuza vita vyake na Urusi na China, ikituma mabomu na makombora yake kwa umbile hili kuwaua na kuwaangamiza watu wa Gaza. Taifa la ukafiri, ambalo linafanya kazi ya kurefusha maisha ya hadhara yake ya Kimagharibi, linakimbilia kulisaidia umbile hili ili kuhakikisha kuwa linabakia hai na kuzuia kutokea kwa chombo kinachotishia uwepo kwake.

Basi muko wapi Umma wa imani?! Yako wapi majeshi ya Waislamu yatakayotetea ndugu zao na kulinda utu wa dada zao?! Je! hivi sivyo munavyopaswa kuwa munafanya? Je, hamupaswi kuamsha ari za wenye ikhlasi miongoni mwao waanzishe juhudi za pamoja zitakazolionyesha taifa la ukafiri yale ambayo hawajayasikia kuhusu Waislamu kutetea heshima ya dada zao?!

Jeshi la uvamizi limenasa picha za wafungwa katika mazingira ya kudhalilisha na kuziweka kwenye mtandao ili kuwadhalilisha zaidi watu wa Gaza na Waislamu kwa jumla... Taasisi ya Euro-Mediterranean Observatory for Human Rights imeeleza kuwa ushahidi hatari zaidi iliopokea ni kuhusu wafungwa kudhalilishwa kingono moja kwa moja, huku baadhi ya wafungwa wakiripoti kuwa "askari ('Waisraeli') waliwanyanyasa, ikiwa ni pamoja na kuwashika viungo vyao nyeti, kuwalazimisha kuvua nguo, na kuvua hijab zao."

Basi mko wapi enyi watu wa Umma wa Kiislamu? Je, mumepigwa na ugumba?! Je, fahari na ulinzi wa utu wenu umekufa ndani yenu?!

Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja ya Mamlaka ya Wafungwa na Masuala ya Ukombozi, yenye uhusiano na Shirika la Ukombozi wa Palestina, na Klabu ya Wafungwa, miongoni mwa wafungwa hao ni "watoto wachanga na wanawake wazee." Muko wapi mbele ya yale ambayo binti zenu, dada zenu na mama zenu wanavumilia, wanyonge na wanaodhulumiwa?!

Sisi, katika Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, hatuna shaka juu ya ikhlasi ya wanaume wa Ummah wa Kiislamu kwa Dini yao, ulinzi wao kwayo, hamu yao ya kuinusuru, na kuinua bendera yake...

Tuna hakika kwamba miongoni mwao wapo ambao damu yao inachemka wanaposikia habari kuhusu Gaza na watoto wake na wanawake wake. Msisite, enyi watu, Ummah bora kabisa ulioletwa kwa ajili ya wanadamu, kutimiza dori yenu ya kufikia moja ya heshima mbili: ushindi au Shahada (kuuawa kishahidi).

Tangazeni hilo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Dini yake, na Mwenyezi Mungu atawanusuru wale wanaonusuru njia yake, na atakufanyeni makhalifa kama alivyo wafanya walio kuwa kabla yenu, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uwezo, Mwenye nguvu.

Enyi Wanazuoni wa Waislamu: vueni vazi la hofu na fedheha na semeni haki, muongoze Ummah na wenye nguvu kwenye njia ya wokovu, na mukae mahala penu kama warithi wa Mitume, muwaangazie njia yao na muwaongoze kwenye haki na njia ya ushindi.

Na enyi Majeshi ya Waislamu: je hakuna miongoni mwenu atakaye vua vazi la uoga, na kujikomboa kutoka katika minyororo ya watawala wake, na kutangaza uasi ulio safi ambao kwao atashinda kwa ajili ya wanawake wa Gaza, Palestina na nchi zote za Kiislamu?!

Tunamuomba Mwenyezi Mungu kwamba wito wetu upate masikio yenye kuitikia, yanayoitikia wito huu na hivyo kumridhisha Mola wa ardhi na mbingu.

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu