Jumamosi, 28 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  22 Rabi' I 1447 Na: H 1447 / 010
M.  Jumapili, 14 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Enyi Waislamu: Waokoeni watu wa Gaza Kabla Hawajaangamizwa Kabisa na Jihadharini Isije Akakushukieni Ghadhabu na Adhabu ya Mwenyezi Mungu
(Imetafsiriwa)

Umbile la Kiyahudi linaendelea na vita vyake vya mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza, likilenga maeneo mbalimbali ya Ukanda huo kwa mashambulizi ya anga na mizinga mikubwa, na kusababisha makumi ya vifo na majeruhi kila siku. Kwa wiki kadhaa, limezidisha mashambulizi yake katika mji wa Gaza, eneo lenye wakaazi wengi na watu waliokimbia makaazi yao kutoka sehemu ya kaskazini ya Ukanda huo, kwa ajili ya maandalizi ya kukaliwa tena kimabavu. Linalenga shule na makaazi, linatekeleza operesheni kubwa za ubomoaji inayolenga nyumba zote za makaazi, na kuvunja magorofa ya makaazi, likiambatanisha na maonyo kuhamia sehemu ya kusini ya Ukanda huo.

Zaidi ya siku 700 zimepita tangu vita vya mauaji ya halaiki huko Gaza, ambapo umbile la Kiyahudi limefanya uhalifu wa kutisha zaidi wa mauaji, uharibifu, uhamishaji na njaa dhidi ya watu wake. Idadi ya mashahidi imezidi 60,000, na idadi ya waliojeruhiwa imezidi 100,000, kulingana na takwimu za Wizara ya Afya. Vifo kutokana na njaa na utapiamlo vimezidi visa 400, wengi wao wakiwa ni watoto. UNICEF imeonya juu ya kuongezeka kwa utapiamlo kusiko na kifani miongoni mwa watoto, na kuthibitisha kwamba majaribio ya hivi karibuni yameonyesha kuwa mtoto mmoja kati ya watano wanaugua utapiamlo mkali. Watu wa Gaza wanasifia utisho na ukatili wa yale wanayoyapatia, wakisema, “Ni mithili ya utisho wa Siku ya Kiyama,” kwa damu, miili iliyokatwakatwa, miili iliyodhoofika, na milio ya makombora na mabomu ambayo hayakomi saa zote.

Kwa zaidi ya siku 700, umbile la Kiyahudi limevuka mistari yote mekundu iliyosemwa juu yake. Hakuna kinga kwa wazee, wanawake, watoto, au hata kijusi tumboni mwa mamake. Kadhalika, hakuna ulinzi kwa hospitali, makaazi, msikiti, au kanisa. Hakuna sehemu salama mjini Gaza. Yale ambayo jeshi la Mayahudi liliyatenga kuwa maeneo salama yalipigwa kwa mabomu na mauaji yalitekelezwa. Wengi wa wale ambao walilazimika kukimbia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza na Mji wa Gaza sasa wanalala chini na kujificha chini ya anga, bila nyumba au hema la kuwahifadhi. Vile vile lilitumia vita vya njaa kuwanyenyekesha watu na kuwaua katika mitego ya vituo vya misaada vya Marekani, na kuleta pamoja nao kauli mbiu zote za haki za binadamu, haki za wanawake na haki za watoto, na aibu ya wale wanaodai kutoka kwa nchi na taasisi zao, imefichuliwa.

Enyi Waislamu: Mayahudi wamekwenda mbali zaidi katika uovu wao na wanaendelea na mipango yao ya kuua idadi kubwa zaidi ya watu wa Gaza na kuwahamisha wale waliosalia, ili kusonga mbele katika kufikia ndoto zao za kibiblia za kusimamisha dola yao kutoka Mto Nile hadi Furat, kama viongozi wao wanavyotangaza kwa ukaidi. Haya ni huku wakiegemeza migongo yao kwa Amerika na rais wake mhalifu mwenye kiburi, Trump. Kwa hakika, kiburi chao na uhalifu wao umevuka Ardhi Iliyobarikiwa hadi kufikia Syria, Lebanon, Yemen, Iran, Qatar, na nchi nyingi zaidi zinaweza kufuata. Katika jinai hii, wanategemea khiyana na ushirikiano wa watawala wenu, hasa watawala wa nchi zinazozunguka wanaowalinda, kuwakandamiza watu wa Gaza, na kuzuia harakati zozote za kuwanusuru.

Hivi kimya hiki cha watawala wasaliti na wahalifu kitaendelea hadi lini?! Je, wakati haujafika wa ulinzi wa kuwahami, ari, na uungwana kuamsha nyoyo na akili za wenye ikhlasi katika majeshi ya Waislamu?! Je, hamtawaokoa kaka na dada zenu kabla hawajaangamizwa hadi mtu wa mwisho?! Je, hamtawaokoa wao na nafsi zenu kabla ya kukushukieni ghadhabu na adhabu ya Mwenyezi Mungu kutokana na kimya na kufeli huku?! Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَإِن تَتَوَلَّوْا يَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُونُوا أَمْثَالَكُم]

“Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi.” [Muhammad: 38].

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu