Jumapili, 10 Dhu al-Hijjah 1445 | 2024/06/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  9 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: H.T.L 1445 / 17
M.  Ijumaa, 17 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon Kikao
“Waliohamishwa Ni Ndugu Zetu”
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon iliandaa kikao kikubwa katika mji wa Tripoli Ash-Sham, kuanzia Msikiti Mkuu wa Al-Mansouri. Hii ilikuwa ni kueleza mshikamano wao pamoja na waliohamishwa na wakimbizi kutoka Syria, ambao walikimbia ukandamizaji wa utawala wa mhalifu Assad na kutafuta hifadhi kwa ndugu zao nchini Lebanon kutafuta usalama na makaazi hadi wapate fursa ya kuregea kwa heshima na usalama katika nchi yao ambako walilelewa na kukulia. Wakati wa kikao hicho, kulikuwa na hotuba za Sheikh Dkt. Mohammad Ibrahim, Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon, na Ndugu Ahmad Al-Shamali, Mwanachama wa Hizb ut Tahrir. Hotuba hizo zilizungumzia nukta zifuatazo:

*Hali yetu na hali ya ndugu zetu waliohamishwa, na uhusiano wetu nao, unaweza kufupishwa kwa maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[وَالَّذِينَ تَبَوَّؤُوا الدَّارَ وَالْإِيمَانَ مِن قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ وَلَا يَجِدُونَ فِي صُدُورِهِمْ حَاجَةً مِّمَّا أُوتُوا وَيُؤْثِرُونَ عَلَى أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ]

“Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.” [Al-Hashr:9].

*Wabaguzi wa rangi wamegawanyika katika makundi mawili: kundi moja ni la wale wenye ubaguzi mbaya wa rangi, ambao wanaamini kuwa ardhi hii ni yao na kusahau kwamba wengi wao walikuja katika ardhi hii kama wageni wa dola ya Kiislamu kwa jumla, na watu wa Al-Sham hasa. Kundi jengine ni la wale ambao wamesahau jinsi walivyofika katika ardhi hii, na ambao bado, hadi leo, hawazungumzi Kiarabu kwa ufasaha na wana pasipoti kadhaa ili kukimbia kutoka nchi hii ikiwa chochote kitatokea! Makundi haya mawili, wabaguzi wa rangi wenye chuki na wasahaulifu, tukiyapita kijuu juu bila ya kuwataja majina na kuwasifia, ni kwa sababu tunajua ubaguzi wao wa rangi wa kuchukiza na chuki yao dhidi ya Uislamu na watu wake! Haishangazi kwamba wanauuma mkono walionyooshewa!

*Ama baadhi ya wale “walio” Waislamu, wanawaona wale wanaoharakisha kuwa pamoja na wabaguzi wa rangi, wakitafuta mapenzi yao, na kuwapa cheti cha kutokuwa na hatia kwa matendo yao, na wanajitwika lawama juu yao, na kuwapa njia ya kuokoa maisha. Hali yao iko hivyo kwa sababu hawaishi hali ya Waislamu kama Umma mmoja ulioungana; badala yake, wanaishi hali ya Lebanon pamoja na madhehebu yake ya kuchukiza, madhehebu yenye kuchukiza, na ubaguzi mbaya wa rangi. Hali yao ni kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[فَتَرَى الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يُسَارِعُونَ فِيهِمْ يَقُولُونَ نَخْشَى أَن تُصِيبَنَا دَآئِرَةٌ فَعَسَى اللهُ أَن يَأْتِيَ بِالْفَتْحِ أَوْ أَمْرٍ مِّنْ عِندِهِ فَيُصْبِحُواْ عَلَى مَا أَسَرُّواْ فِي أَنْفُسِهِمْ نَادِمِينَ]

“Utawaona wale wenye maradhi nyoyoni mwao wanakimbilia kwao wakisema: Tunakhofu yasitusibu mabadiliko. Huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi au jambo jingine litokalo kwake wakawa wenye kujuta kwa waliyo yaficha katika nafsi zao.” [Al-Ma’ida:52].

Na kwa wanasiasa hawa miongoni mwa Waislamu, hasa wale wa Tripoli, hususan Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani, pia tunasema: Kwa nini mumejifungamanisha na wabaguzi hawa wa rangi, na dhidi ya nani? Dhidi ya Waislamu wa Lebanon wanaokataa mwelekeo huu! Na hii hapa ndio sauti yao, ambayo mumeisikia kwa uwazi, ikitabanni njia ya waliohamishwa, ikithibitisha kuwa wao ni watu wetu, na sisi ni miongoni mwao, na wao ni miongoni mwetu.

* Tunafahamu kwamba munatafuta njia ya kuhalalisha mahusiano na utawala mhalifu wa Bashar Assad, ambao yeye na babake wametekeleza ukatili nchini Syria na Lebanon. Na hawa hapa, wanaanza kuwasiliana na utawala wa Syria kando kando ya Mkutano wa Waarabu nchini Bahrain! Mawasiliano haya hayatangazwi rasmi na serikali bali yanapitishwa kwa siri kupitia vyombo vya habari kwa kisingizio cha suala la watu waliohamishwa! Mawasiliano haya hayatangazwi rasmi na serikali bali yanapitishwa kwa siri kupitia vyombo vya habari kwa kisingizio cha suala la watu waliohamishwa!

* Tunafahamu jinsi Marekani inavyosimamia eneo hili na kudhibiti masuala yake kwa manufaa yake yenyewe! Lakini tunakuonyeni musijaribu kuwatumia waliohamishwa kama kichocheo cha njama zenu na utiifu wenu kwa bwana wenu Marekani! Pia tunawatahadharisha wabaguzi wa rangi wa kimadhehebu dhidi ya kucheza na moto kwa kuzua masuala ili kuchochea fitna! Waislamu leo sio sawa na walivyokuwa zama za vita vyenu, hivyo msipite njia hii!

* Ama kuhusu kupanga mambo ya watu wetu waliohamishwa, hilo hatupingi, bali ni lazima ifanywe bila dhulma, mapendeleo, au kuvuka mipaka!

* Kuhusu ndugu zetu ambao wanazuiliwa kiholela katika magereza ya Lebanon bila kesi miongoni mwa watu wetu waliohamishwa, tutapinga kuhangaishwa kwao kwa kila njia. Tunatoa wito kwa mawakili wa Kiislamu na wataalamu wa sheria kusimama kidete katika suala hili, na tunayawajibisha mashirika ya haki za binadamu na ya misaada ya kibinadamu kwa yale yanayoweza kutokea kwa ndugu zetu waliowekwa kizuizini kwa maoni yao! Hasa kwa vile munajua kwamba utawala wa kihalifu nchini Syria utafanya kazi ya kuwamaliza, kama ulivyofanya kwa wengine hapo awali!

Na ujumbe kwa Waislamu kwa jumla:

Waliohamishwa ni ndugu zenu; walikimbiza nafsi zao, Dini yao na watoto wao kwenu, basi msiwasalimishe mwa adui zenu na wao. Zingatieni maneno ya Mtume (saw):

«الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ لَا يَظْلِمُهُ وَلَا يُسْلِمُهُ، وَمَنْ كَانَ فِي حَاجَةِ أَخِيهِ كَانَ اللهُ فِي حَاجَتِهِ، وَمَنْ فَرَّجَ عَنْ مُسْلِمٍ كُرْبَةً فَرَّجَ اللهُ عَنْهُ كُرْبَةً مِنْ كُرُبَاتِ يَوْمِ الْقِيَامَةِ وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِماً سَتَرَهُ اللهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ»

“Muislamu ni ndugu ya Muislamu, hamdhulumu na wala hamsalimishi katika maangamivu, na anayejishughulisha na haja ya ndugu yake, basi Mwenyezi Mungu atajishughulisha na haja zake, na anayempa faraja Muislamu kutokana na shida yake, Mwenyezi Mungu atamfariji shida miongoni mwa shida za Siku ya Kiyama na anayesitiri (aibu) ya Muislamu, Mwenyezi Mungu atamsitiri (aibu zake) Siku ya Kiyama.” [Sahih]

Na kwa hakika, wajibu wa Sharia unaamrisha kuwachukulia Waislamu kuwa ni Ummah mmoja, sio watu, mataifa na dola zilizotenganishwa kwa kile kinachoitwa mipaka ya kitaifa inayousambaratisha Ummah na kutengeneza kizuizi cha kulinda mifumo iliyoundwa na kafiri mkoloni ili kuutumikia maslahi yake ya kikoloni. Hairuhusiwi kwetu, wala si halali, kuutambua uhalisia huu uliowekwa na ukoloni, achilia mbali kujitahidi kuuwekea taasisi na kuhalalisha hali ulizoziunda.

* Ummah wa Kiislamu ni Ummah wa kipekee tofauti na wengine, wenye uhusiano wake kati yao wenyewe kwa wenyewe kupitia mafungamano ya Aqidah ya Kiislamu na fahamu za Uislamu na Sharia yake.

* Ujumbe wa mwamko ulitolewa na Sheikh Nabil Rahim, ambapo aliashiria udugu wa Kiislamu na utakatifu wa kuwalinda waliohamishwa na kusisitiza kwamba wananchi wa Lebanon wanapaswa kukataa mwelekeo wa ubaguzi wa rangi na kusisitiza kwamba mgogoro wa kiuchumi ni mgogoro wa wezi na wafisadi, si mgogoro wa watu waliohamishwa.

Kwa kuhitimisha, Hizb ut Tahrir/Wilayah Lebanon inathibitisha kujitolea kwake kwa jambo hili mpaka ukweli uthibitike na uwongo ubatilike, hata kama wabaguzi wa rangi, wachongezi na wanafiki watachukia. Tutaendelea na misimamo ya haki, maneno ya ukweli, na mapambano ya kifikra dhidi ya mfumo wowote mgeni na Uislamu, na mapambano ya kisiasa dhidi ya tawala potovu katika ardhi za Kiislamu hadi kusimamishwa Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Chini ya kivuli chake, Waislamu na wasiokuwa Waislamu huishi, na inawahifadhi wale wanaokimbilia humo, wakitafuta usalama na ulinzi bila kujali dini zao.

[وَإِنْ أَحَدٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّى يَسْمَعَ كَلاَمَ اللّهِ ثُمَّ أَبْلِغْهُ مَأْمَنَهُ ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لاَّ يَعْلَمُونَ]

“Na ikiwa mmoja wapo katika washirikina akikuomba ulinzi, basi mpe ulinzi apate kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu. Kisha mfikishe pahala pake pa amani. Haya ni kwa kuwa hao ni watu wasiojua kitu.” [At-Tawba:6]. Hili linakaribia kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hali katika eneo hili - mara kwa mara - ziko kwenye ukingo wa mabadiliko makubwa, kwa hivyo simameni katika safu za Uislamu na watu wake.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu