Jumamosi, 21 Muharram 1446 | 2024/07/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  2 Sha'aban 1445 Na: 1445/19
M.  Jumatatu, 12 Februari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ni Nani Atakayefuta Aibu Yenu, Enyi Wanajeshi wa Kinana?!
(Imetafsiriwa)

Baada ya mkuu wa ujasusi wa Misri kuwaonya Hamas juu ya ulazima wa kukubali makubaliano ya kubadilishana wafungwa yaliyoandaliwa chini ya mwavuli wa Marekani ndani ya wiki mbili, na kisha tangazo la redio ya jeshi la umbile la Kiyahudi kwamba Misri ingekubali kuivamia Rafah kwa masharti ya kuhakikisha kuwa Wapalestina hawafurushwi hadi Sinai, pia mnamo Jumapili asubuhi, tarehe 11/2/2024, redio hiyo ilinukuu maafisa wa Misri wakiufahamisha upande wa 'Israel' wa kutoupinga uvamizi wa kijeshi wa Rafah katika mji wa Rafah kwa sharti la kuepuka majeruhi ya raia wa Palestina. (Euronews).

Kisha ukatokea upigaji makombora wa Rafah, ambayo iko tu umbali mfupi kutoka kwa walinzi wa mpaka wa Misri, baada ya usiku wa manane, na kuwaamsha watu kwa milio ya ndege na sauti ya milipuko, mbele ya macho na masikio, kwa ukimya na kutelekezwa kutoka kwa Ummah wote na majeshi yake, lakini kwa ushiriki na baraka kutoka kwa watawala wake na serikali zinazounga mkono umbile la Kiyahudi katika kuhudumia Marekani na Magharibi.

Wakati jeshi la Kiyahudi likiushambulia kwa mabomu mji wa Rafah ulioko kusini mwa Ukanda wa Gaza, ambao umezingirwa na utawala wa Misri, na kuwanasa watu wake mbele ya moto wa jeshi hilo linaloikalia kwa mabavu, watu wanawaita askari waheshimiwa wa Kinana, wakiisihi fahari na mabaki ya Uislamu ndani ya nafsi zao, wakiwaomba kwa ajili ya Mwenyezi Mungu wawaokoe; wawaokoe watu hawa wanaodhulumiwa na kuteswa.

Yaliyotokea na yanayowatokea kwa watu wetu katika Ardhi Iliyobarikiwa ni fedheha ambayo haitafutika isipokuwa kwa damu, ni fedheha juu ya Ummah mzima kwa jumla, na fedheha kubwa zaidi inaangukia majeshi yake, na fedheha kubwa zaidi inawapata wanajeshi wa Kinana. Vipi mnaweza kuwapiga mabomu na kuwaua watu wetu nchini Palestina mbele ya macho na masikio kutoka kwenu?! Je damu haichemki kwenye mishipa yenu?! Au hakuna damu kwenye mishipa yenu?! Tujibuni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, vipi mutamkabili Mwenyezi Mungu na damu ya watu wa Palestina mikononi mwenu?! Na mtasimamaje mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na hali wanasema mumetutelekeza na mumewatia nguvu maadui zenu juu yetu?!

Enyi Wanajeshi wa Kinana: Ukombozi wa Palestina ni wajibu wenu hata kabla ya vita hivi na kabla ya shambulizi hili la mabomu, na sasa ni wajibu wa haraka kuwanusuru wadhulumiwa hawa na kuwaondolea dhulma. Munafanya nini?! Wallahi, hawa watawala hawatakufaeni, wala hawatakukingeni na hata cheche moja ya Moto Siku ya Kiyama, basi msiwasikilize na wala msiwatii katika kumuasi Mwenyezi Mungu. Ni dhambi gani kubwa kuliko kuwatelekeza ndugu zenu katika ardhi iliyobarikiwa?! Je! haikukufikieni kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)?:

«مَا مِنِ امْرِئٍ يَخْذُلُ امْرَأً مُسْلِمًا فِي مَوْضِعٍ تُنْتَهَكُ فِيهِ حُرْمَتُهُ وَيُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ إِلاَّ خَذَلَهُ اللَّهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ وَمَا مِنِ امْرِئٍ يَنْصُرُ مُسْلِمًا فِي مَوْضِعٍ يُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ وَيُنْتَهَكُ فِيهِ مِنْ حُرْمَتِهِ إِلاَّ نَصَرَهُ اللَّهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ نُصْرَتَهُ»‏

Hakuna mtu (Muislamu) atakayemtelekeza Muislamu mwengine katika mahali ambapo utukufu wake unakiukwa na heshima yake inadunishwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atamtelekeza katika mahali ambapo angependa msaada wake; na hakuna mtu (Muislamu) ambaye atamsaidia Muislamu mahali ambapo heshima yake inadunishwa na utukufu wake unakiukwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atamsaidia mahali anapotaka msaada wake.” Uko wapi msimamo wenu kuhusu kilio cha mayatima, wazee na wanachuoni?!”

Na uko wapi msimamo wenu kwa vilio mayatima, wazee, na wanazuoni?! Na kuko wapi kushikamana kwenu na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ambaye alitangaza uhamasishaji wa jumla na akaingia Makkah kwa ushindi, na kutangaza ushindi kwa Khazaa'ah na kusema:

«نُصِرْتَ يَا عَمْرُو بْنَ سَالِمٍ» “Nimenusuriwa, Ewe Amr ibn Salim.” na akasema: «لَا نَصَرَنِي اللَّهُ إِنْ لَمْ أَنْصُرْ بَنِي كعب» “Mwenyezi Mungu asininusuru iwapo sitawanusuru Bani Ka'b.”

Na nyinyi muko wapi na Al-Muutasim, ambaye mwanamke mmoja aliomba msaada kutoka kwake, na akakimbilia kumsaidia na kuifungua 'Amuriyyah ili amsaidie?! Muko wapi katika maelfu ya wanawake wanaokuombeni msaada, na wazee wanaokuombeni msaada, na watoto wanaokuiteni nyuma ya nyua na kuta (kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, enyi Wamisri)?! Vilio vya watu hawa vimeamsha huruma kwa watu wenye nia njema kote duniani, vikipita karibu yenu kana kwamba hamkuwasikia, ilhali ni ndugu zenu na watu wenu! Basi uko wapi uungwana wenu, na iko wapi Aqidah yenu, na Uislamu wenu, na uko wapi wema wenu munaojifakhirisha nao?! Wallahi, leo hamuna udhuru, na aibu yenu haitafutika isipokuwa kwa damu.

Enyi Wanajeshi wa Kinana, Enyi Wanajeshi Bora: Uungwana sio beji, bali ni amana ambayo kwayo mtaulizwa. Unastahiki tu wale wanaobeba bendera ya Rayah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kwa haki, kama wapiganaji katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wasaidizi wa waliodhulumiwa, watiifu kwa Mwenyezi Mungu, Mtume wake na Dini yake, wasio na utiifu. kwa yeyote juu ya utiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na kutowatii watawala wanaotii amri za Magharibi, kutekeleza mifumo yao, kutekeleza miradi yao ya kikoloni, na kusimama katika njia ya kukomboa matukufu ya Ummah na kuwanusuru wanaodhulumiwa miongoni mwao. Hawa ndio wanaostahiki wema, basi je nyinyi ni miongoni mwao? Jijibuni nafsi zenu kabla ya Mwenyezi Mungu kuulizeni, na simameni kumnusuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Dini yake. Ling’oeni umbile hili fisadi kutoka kwenye mizizi yake na yeyote anayesimama baina yenu nalo, akikuzuia kuling'oa, wakiwemo watawala wa uovu na khiyana.

Ni amana ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), basi ilindeni na muwe watu wake, ngao ya Ummah huu, walinzi wake, na wasaidizi wa wanaodhulumiwa ndani yake, wenye msimamo juu ya Dini yake na mambo ya dunia. Kwani msipotenda na kukiuka matukufu ya Ummah na kuyanajisi matukufu yake kama inavyotokea sasa, basi hamna kheri kwenu wala hamna heshima kwenu. Muonyesheni Mwenyezi Mungu kutokana na nafsi zenu yale anayoyapenda, na muonyesheni kwamba mnastahiki wema huu kwa kubeba rayah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kwa haki na kuwanusuru waliodhulumiwa kama alivyofanya, kuikomboa ardhi ya Uislamu waliyoipora Mayahudi, na kuwasaidia watu wa Nchi Iliyobarikiwa ambao matukufu yao yamekiukwa. Jueni kwamba wajibu wenu ni kuondosha kila kinachokuzuieni kutimiza yale ambayo Mwenyezi Mungu amewajibisha juu yenu kwa sababu 'chochote kinachohitajika kutekeleza wajibu ni wajibu pia.'

Kwa hiyo, uondoeni mfumo huu unaokutieni madoa kwa fedheha na kushirikiana na kuwalinda maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu. Simamisheni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Dola inayo kusanya majeshi kwa ajili ya haki na msaada wa watu wake; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Basi hebu hasira zenu na zithibitike, enyi Wanajeshi wa Kinana, na hebu hasira zenu ziwe ni dalili inayothibitisha ukweli kwa maneno ya Mwenyezi Mungu na kuzikata njia za wahalifu.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal:24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu