Jumamosi, 21 Muharram 1446 | 2024/07/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  16 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: 1445/25
M.  Ijumaa, 24 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mashujaa wa Utawala wa Misri Hawaelekezwi Dhidi ya Umbile la Kiyahudi Badala yake Unaendelea na Juhudi zake katika Kuzingira, Kunyima Chakula, na Kuua Watu wa Gaza!
(Imetafsiriwa)

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani iliitaka Misri mnamo siku ya Jumatano kufanya kila iwezalo kuhakikisha mtiririko wa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza. Wakati huo huo, Cairo ilieleza kuwepo kwa chama cha Kipalestina katika kivuko cha Rafah ili kupokea msaada huo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, katika kikao cha Bunge, alisema kuwa kivuko cha Rafah kinachoelekea kusini mwa ukanda huo kimefungwa tangu jeshi la Kiyahudi lilipochukua udhibiti wake tarehe 7 Mei. Aliongeza kuwa mapigano karibu na kivuko hicho yamefanya kazi ya kupeana misaada kuwa ngumu, lakini mtiririko wa misaada bado unawezekana, akimaanisha dhahiri kivuko cha Kerem Shalom karibu na Rafah. Blinken alisema, "Kwa hiyo tunahitaji kutafuta njia ya kuhakikisha kwamba msaada ambao ungepitia Rafah unaweza kupita kwa usalama, lakini tunawaomba sana washirika wetu wa Misri kufanya kila wawezalo katika mwisho wao wa mambo ili kuhakikisha kuwa msaada unapita." Uwasilishaji wa misaada kusini mwa Gaza umetatizika tangu umbile la Kiyahudi lilipozidisha operesheni zake za kijeshi huko Rafah, hatua ambayo Umoja wa Mataifa unasema imewalazimu takriban watu 900,000 kukimbia na kuzua taharuki na Misri.

Kwa upande wake, Diaa Rashwan, mwenyekiti wa Huduma ya Habari ya Serikali ya Misri, alisema katika taarifa kwa Chaneli ya Habari ya Al-Qahera kwamba Misri "inahitaji uwepo wa chama cha Palestina ili kupokea msaada katika kivuko cha Rafah na haitaamiliana na 'Israel.' kwenye kivuko hicho kwani ni dola inayokalia kimabavu." Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shoukry alisema Jumatatu iliyopita, “Uwepo wa kijeshi wa ‘Israel’ na operesheni zinazofanywa na jeshi la ‘Israel’ ni hali zinazohatarisha madereva wa malori, jambo ambalo limesababisha kusitishwa kwa misaada inayovuka mipaka.” (Al Jazeera Net, 23/5/2024).

Ni kana kwamba utawala wa Misri hatimaye umekumbuka kwamba umbile la Kiyahudi ni dola inayokalia kwa mabavu, kana kwamba haikukiuka utakatifu wa watu wetu wa Gaza, mipaka ya bandia, na hata makubaliano ya khiyana yaliyotiwa saini na utawala huo, na ilikaribia kudhibiti kikamilifu ukanda wa Salah al-Din sambamba na Ukanda wa Gaza! Haya yote yalikiukwa na umbile la Kiyahudi, lakini utawala wa Misri, kama tawala zote za vibaraka, unaendelea kutangaza na kubaki na haki ya kujibu, kana kwamba damu inayomwagika si damu ya Umma ambayo lazima ihifadhiwe, kana kwamba ardhi iliyonyakuliwa si ardhi ya Umma ambayo ni lazima ikombolewe, na kana kwamba matukufu yanayokiukwa na kunajisiwa sio matukufu ya Umma ambayo yanapaswa kuregeshwa na kutakaswa kutokana na unajisi ya Mayahudi!

Jibu kwa umbile la Kiyahudi sio kukata misaada kwa watu wenye njaa na wasio na silaha bali ni kutoa kauli kama ya Harun al-Rashid kwa Nikephoros: Kutoka kwa mtawala wa Waislamu na kiongozi wao hadi kwa mbwa wa Mayahudi na walio nyuma yake na wanaomuunga mkono. Mnachokiona ni kidogo kuliko mnachokisikia, na kwa jina la Mwenyezi Mungu nitakuleteeni majeshi mengi kama chembe za mchanga, na nitawang'oa nyinyi na umbile lenu ovu kutoka kwenye mizizi yenu, na nitawaletea ushindi watu wa ardhi iliyobarikiwa, ushindi unaotukuza Uislamu na watu wake. Hivi ndivyo inavyopaswa kuwa jawabu, lakini ni wapi hili, na yuko wapi yule anayeitikia wito wa Ummah na vilio vya wanawake wake huru, akisema, "Hapa niko kwa ajili yake, niko hapa kwa ajili yake," na kubeba bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kwa haki na kung'oa tawala hizi zinazolinda umbile ovu, na kuregesha dola ya Kiislamu inayoyapeleka majeshi yake kwenye ardhi iliyobarikiwa, kama msaidizi na mkombozi, dola ya Kiislamu; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume?

Kilichotokea na kinachoendelea kutokea kutoka kwa umbile la Kiyahudi kinalazimu uhamasishaji wa haraka wa majeshi chini ya mfumo wowote na sheria zozote. Je, itakuwaje zaidi pale Dini na Aqida yetu zinapotuamrisha kukusanya majeshi ili kuwapa nusrah (msaada) watu wetu wanaodhulumiwa huko na kukomboa kabisa ardhi yao?! Ardhi ya Palestina ni ya Ummah wote, na ukombozi wake ni wajibu kwa Ummah wote, hasa wajibu kwa Misri na jeshi lake, kwa kuwa liko karibu zaidi, lenye nguvu zaidi, na uwezo zaidi. Kamwe haijuzu kwao kuwatelekeza au kufeli kuwanusuru.

Enyi Wanajeshi wa Kinana, askari bora: Kheri yenu imefungamanishwa na nusra yenu kwa ajili ya Dini hii, watu wake, na matukufu yake. Ikipotea, hakuna kheri kwenu wala miongoni mwenu. Regesheni kheri yenu na mustahiki hilo kwa haki, kama ngao ya Ummah dhidi ya mashambulizi ya Magharibi na wafuasi wake, muikomboe na ardhi yake kutoka kwa tawala zinazotii amri zake, na kuwanusuru wale wanaofanya kazi ya kuutabikisha Uislamu ndani ya dola yake, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo inaunganisha Ummah pamoja nanyi na kukupelekeni kwenye kuikomboa ardhi ya Uislamu na kuwanusuru wanaodhulumiwa.

Basi bebeni Rayah (bendera) ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kwa haki, na muwang’oe watawala hawa wanaosimama kati yenu na heshima ya dunia hii na Akhera, na kuweni Maanswari (wanaonusuru) wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, ili Mwenyezi Mungu akukubalieni na akupeni nusra, na mpate ushindi mkubwa.

[وَلَيَنْصُرَنَّ اللَّهُ مَنْ يَنْصُرُهُ إِنَّ اللَّهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ * الَّذِينَ إِنْ مَكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ أَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ وَأَمَرُوا بِالْمَعْرُوفِ وَنَهَوْا عَنِ الْمُنْكَرِ وَلِلَّهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ]

“Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu. (40) Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi husimamisha Sala, na wakatoa Zaka, na wakaamrisha mema, na wakakataza mabaya. Na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya mambo yote.” [Al-Hajj:40-1].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu