Afisi ya Habari
Wilayah Misri
H. 17 Dhu al-Hijjah 1446 | Na: 1446/36 |
M. Ijumaa, 13 Juni 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Utelekezaji wa Serikali ya Misri wa Gaza:
Kuanzia Kuzuia Nusra, Hata wa Maneno, hadi Kushiriki kwa Kizuizi!
(Imetafsiriwa)
Katika mandhari inayojirudia rudia, kwa kila maafa yanayowakumba watu waliozingirwa wa Gaza, tawala za Kiarabu - zinazoongozwa na utawala wa Misri - zinathibitisha kwamba sio tu hazipo katika wajibu wao wa kunusuru, lakini pia ziko katika nafasi ya ulaji njama na usaliti, na hata kushiriki kikamilifu katika mzingiro, kulinda vivuko na kuzuia mradi wowote wakilishi au maarufu kwa lengo la kukandamiza Waislamu.
Mnamo 11 Juni 2025, utawala wa Misri uliwafukuza wanaharakati 12 wa Morocco ambao walikuwa wamefika kihalali katika Uwanja wa Ndege wa Cairo kushiriki katika "Maandamano ya Kimataifa hadi Gaza," msafara wa wakilishi ulioitishwa na wanaharakati kutoka kote ulimwenguni, Waarabu na wasio Waarabu, kuangazia mzingiro, njaa na mauaji yanayoendelea katika Ukanda wa Gaza kwa miezi kadhaa. Badala ya Misri, lango pekee lililo wazi la Gaza, kuwakaribisha kwa misaada na usaidizi, wakifungua njia yao kuelekea Rafah kushuhudia dhuluma wanayoipata, jibu lilikuwa ni muamala wa kudhalilisha kutoka kwa usalama na kufukuzwa mara moja.
Hawakuwa wamebeba silaha, wala hawakuitisha milipuko ya mabomu au hujuma. Bali, walikuja na nyoyo zilizojaa matumaini kwamba wangechukua msimamo wa kiwakilishi katika mshikamano na watu Waislamu wanaochinjwa mchana na usiku. Hata hivyo, walizingirwa ndani ya uwanja wa ndege, wakahojiwa kwa maswali ya kudhalilisha, na kupewa chaguo kati ya kuwekwa kizuizini au kufukuzwa, kana kwamba mshikamano na Gaza ni uhalifu chini ya utawala huu!
Ni jambo lisilofikirika kuwa tukio hili lilikuwa la bahati mbaya, au lilihusiana na udhibiti wa mpaka tu, kama Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri ilivyodai. Inajulikana kuwa kivuko cha Rafah kiko chini ya udhibiti wa Misri na kiko wazi kwa utawala wa Misri kwa khiyari yake. Hakika, inaweza kuruhusu mtu yeyote inayetaka kuingia na kuzuia mtu yeyote inayetaka kuingia. Hata hivyo, mamlaka haya juu ya kuvuka kamwe hayajawahi kutumika kunusuru watu wa Gaza. Badala yake, imebakia kuwa njia ya shinikizo na mzingiro inayotekelezwa kwa jina la ubwana, ikiigeuza kuwa chombo cha kutumikia usalama wa umbile la Kiyahudi.
Wale wanaofunga kwa imara kivuko kwa msaada, kuzuia misafara wakilishi, kukandamiza maandamano ya mshikamano, na kuainisha hisia za hasira kama tishio la usalama hawawezi kupewa udhuru wa ujinga au uzembe. Badala yake, wanahusika katika uhalifu.
Waislamu mjini Gaza, au kwengineko, lazima wasiachwe peke yao wakabiliane na mauaji, kuzingirwa, njaa, na uharibifu bila ya kunusuriwa na Umma, hasa wale wenye uwezo wa kuwapatia misaada. Utawala wa Misri, pamoja na jeshi lake, vifaa, na uwezo, ni miongoni mwa wenye uwezo zaidi. Hauna udhuru kwa kukaa kimya; bali ni dhambi kwa kupuuza wajibu wake. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
[وَإِنِ اسْتَنْصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]
“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia” [Al-Anfal 8:72]. Iwapo utafutaji tu msaada unawajibisha msaada, inakuwaje wakati watu wa Gaza wamelia mara kwa mara kuomba msaada, na Umma wa Kiislamu kila mahali umeonyesha utayari wake wa kusimama pamoja nao? Je, msimamo wa serikali ulikuwa ni upi? Haikuwanusuru wala hata kumruhusu yeyote aliyetaka kuwafariji. Kinachoshangaza zaidi ni kwamba utawala huu umehama kutoka kwenye msimamo wa kushiriki na kwenda kwenye ule wa kuzuia kila mpango, hata ule ambao hautishii mamlaka yake, kana kwamba kuelezea tu mshikamano wake na Gaza kumekuwa, kwa maoni yake, "tishio la usalama." Hili linaonyesha kuwa imefanya uamuzi wa wazi wa kuegemea upande wa adui wa Umma huu, na kwamba inaiona kadhia ya Palestina kuwa si chochote zaidi ya mzigo ambao uchochezi wake lazima unyamazishwe.
Jeshi la Misri, na utawala unaoshikilia mamlaka ya kisiasa na kijeshi, lazima uelekeze vikosi vyao sio kuzuia misafara au kufunga vivuko, bali kwa kufungua kivuko kwa nguvu, kuvunja mzingiro wa Gaza, kushambulia ngome za Mayahudi, na kuikomboa Palestina yote. Hawapaswi kusimama kwenye magofu ya kivuko cha Rafah, wakisubiri ruhusa kutoka kwa Amerika au idhini kutoka Tel Aviv.
Ardhi ya Palestina ni ardhi ya Kiislamu inayokaliwa kwa mabavu. Ukombozi wake ni wajibu wa Waislamu wote, na kwanza kabisa wa majeshi. Huu ni wajibu kamili wa kidini ambao hauwezi kuachwa kwa kupita kwa wakati au kwa kutumia mikataba ya kimataifa au mikataba ya khiyana. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «فُكُّوا الْعَانِي» “mkomboeni mateka”. Kwa hivyo wako wapi majeshi na kutoka kuwakomboa maelfu ya wafungwa katika jela za Mayahudi? Kwa hakika, wako wapi na kuwakomboa wafungwa waliozingirwa ndani ya Ukanda wa Gaza? Mipaka imebadilishwa kuwa gereza kubwa, lililofungwa imara kwa jina la "ubwana." Ubwana una hatia katika Uislamu ikiwa unawazuia Waislamu kuwanusuru ndugu zao.
Walichofanya wanaharakati, licha ya maumbile yake ya kiwakilishi na kutokuwa na uwezo wa kuwasaidia watu wa Gaza, kinaonyesha mwamko wa hali ya juu ndani ya Umma, ambao haujafa, wala kusahau wajibu wake. Hata hivyo, tatizo haliko kwa watu, bali ni tawala zinazolinda umbile la Kiyahudi, kuhalalisha mahusiano nalo kwa dhahiri au kwa siri, na kuupiga vita umma juu ya dini, imani na misimamo yake.
Utawala wa Misri leo haujasimama pasi na uchukuaji hatua; badala yake, ni upande changamfu katika mlinganyo wa kuinyonga Gaza. Hakika, ushiriki wake katika kizuizi aghlabu huzidi uhalifu wa Mayahudi, kwani huzuia hata hewa ya huruma kufikia Ukanda huo. Inawapiga wanaharakati, inawatesa waandishi wa habari, inawafukuza wale wanaoonyesha mshikamano, na kunyamazisha sauti, kwa sababu inatambua kwamba sauti yoyote huru ni tishio kwa utawala wake na utiifu wake, wa kitumwa.
Mojawapo ya maafa makubwa yaliyoendelezwa na tawala za baada ya Sykes-Picot ni kupandikizwa kwa fahamu ya "ubwana wa kitaifa," ambapo Waislamu wa Morocco wakawa wageni nchini Misri, Waislamu wa Misri wakawa wageni nchini Syria, na Waislamu wa Jordan wakawa wavamizi nchini Palestina.
Hii inagongana na Uislamu, ambao uliunda Ummah mmoja, bila kutambua mipaka, pasipoti, au visa. Je, Muislamu wa Morocco anahitaji visa ili kufika Palestina? Je, ahojiwe kuhusu nia yake ya kuonyesha mshikamano? Au msaada umekuwa uhalifu, na usaliti ni heshima, machoni pa serikali vibaraka?
Kilichotokea Uwanja wa Ndege wa Cairo halikuwa tukio la kupita! Bali ni dalili ya ugonjwa wa kudumu unaosibu serikali inayotawala: usaliti wake kwa umma na imani yake, na ushiriki wake katika mradi wa Mamarekani na Wazayuni wa kufilisi kadhia ya Palestina.
Utawala huu hauwezi kurekebishwa kwa kuuweka viraka au kuurembesha. Bali, unaweza tu kusahihishwa kwa kuung’oa na kuweka mahala pake mfumo wa Kiislamu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo itakusanya majeshi kuikomboa Al-Aqsa na kuinua bendera ya Uislamu. Kile ambacho Ummah, hasa vijana wake, lazima utambue ni kwamba njia ya kwenda Palestina haipitii kuziombea dua tawala, wala kupitia misafara ya wakilishi, licha ya uwakilishi wao wa maana. Bali, inapitia mabadiliko makubwa katika ardhi za Kiislamu, kupitia kusimamishwa kwa dola ya Kiislamu ambayo haijui chochote isipokuwa ushindi au kifo cha kishahidi.
Enyi Wanajeshi wa Kinana: Ukombozi wa Palestina ni wajibu juu yenu, na hakuna jambo la faradhi zaidi baada ya imani kuliko kuutekeleza. Kuufukuza uwepo wa kijeshi wa makafiri katika ardhi za Kiislamu ni wajibu juu yenu kabla ya mtu mwengine yeyote. Linapotokea shambulizi katika ardhi za Waislamu, au inapojulikana kuwa adui anajiandaa kuvamia ardhi za Waislamu, jihad ni faradhi kumfukuza adui mpaka kila mtu katika ardhi hiyo atosheke. Adui akipata udhibiti juu yake, wajibu wa jihad huhama kutoka kwenye ardhi hiyo kwenda kwa wale walio karibu nao. Ikiwa hawataweza kufanya hivyo, basi ni juu ya wale walio karibu nao, na kadhalika mpaka faradhi iwafikie Waislamu wote. Adui akipata udhibiti juu ya ardhi maalum, jihad inakuwa ya khiyari kwa watu wa ardhi hiyo inayokaliwa, kwani wanakuwa wafungwa. Hata hivyo, inabakia kuwa ni faradhi kwa wale wanaoweza kufanya hivyo miongoni mwa Waislamu katika ardhi zinazozunguka eneo hilo linalokaliwa kwa mabavu. Kwa kuwa serikali inayokutawaleni inaharamisha jihad kukomboa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, na “chochote kinachohitajika kwa ajili ya kutekeleza wajib chenyewe ni wajib,” kuuondoa utawala huu ni wajib ili kuregesha jihad na kukomboa ardhi ya Uislamu na matukufu yake, na kabla ya hapo, taji la faradhi. Kuhukumu kwa Uislamu ndani ya dola yake, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.
Enyi Wanajeshi wa Kinana: Mumekuwa na mnaendelea kuwa ngao ya Ummah; silaha mkononi mwake. Regesheni uhuru wenu, simameni pamoja na Ummah wenu, na mukate minyororo ya watawala wanaokuzungukeni. Tupeni marupurupu yao, vyeo, na mishahara. Shikanisheni mikono yenu pamoja na mikono ya wale watakaokuingiza kwenye Pepo ambayo upana wake ni kama mbingu na ardhi, kwani hiyo ina manufaa zaidi kwenu na ni yenye kudumu zaidi kwa Mwenyezi Mungu. Bebeni pamoja nao hamu ya Ummah wenu na muregeshe mamlaka yake chini ya mwavuli wa Uislamu na dola yake, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.
[وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ]
“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na Watoto” [An-Nisa 4:75]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Misri |
Address & Website Tel: http://hizb.net/ |
E-Mail: info@hizb.net |