Khilafah kwa ajili ya Ulimwengu usio na NATO
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Marais wa nchi na serikali za nchi wanachama wa NATO walikutana jijini The Hague, Uholanzi mnamo tarehe 24-25 Juni.
Marais wa nchi na serikali za nchi wanachama wa NATO walikutana jijini The Hague, Uholanzi mnamo tarehe 24-25 Juni.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hivi karibuni lilifanya kikao maalum kujadili hali ya Afghanistan. Katika mkutano huu, Roza Otunbayeva, mkuu wa Misheni ya Misaada ya Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan (UNAMA), aliwasilisha mfumo mpya wa kina unaoitwa "Mpango wa Mosaic." Alisisitiza kuwa mpango huu haulengi "kusawazisha hali nchini Afghanistan," bali unalenga kuendeleza maslahi ya kweli ya watu wa Afghanistan.
Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya ya Palestina mjini Gaza, Dkt. Munir Al-Barsh, alifichua kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaokufa kwa njaa, na kuthibitisha kwamba uvamizi "unafurahi kuwaua," huku kukiwa na mzingiro unaoendelea, kufungwa kwa vivuko, na kupuuza mfumo wa kimataifa. Katika mahojiano katika Chaneli ya Al Jazeera, Al-Barsh alisema kuwa idadi ya watoto waliouawa shahidi kutokana na utapiamlo uliokithiri imefikia 66 hadi sasa, kati yao wa hivi punde ni mtoto mchanga wa miezi mitatu Jouri Al-Masri, akibainisha kuwa makundi yaliyo hatarini zaidi, hasa miongoni mwao ni watoto, wamekuwa wahanga wakuu.
Makundi yenye silaha ya Rohingya yameanza kusajili kutoka kambi za wakimbizi za Cox's Bazar kusaidia katika mapigano dhidi ya Jeshi la Arakan huko Rakhine. Taarifa hiyo ilifichuliwa katika ripoti moja ya Shirika la Kimataifa la kutatua Migogoro yenye kichwa "Bangladesh/Myanmar: Hatari za Waasi wa Rohingya". Ripoti hiyo inabainisha kuwa, baada ya Jeshi la Arakan kupata ushindi dhidi ya jeshi la Myanmar huko Rakhine, makundi ya Rohingya yamezidi kuwa changamfu na yamekubali kufanya kazi kwa pamoja dhidi ya Jeshi la Arakan, kundi ambalo lenye Mabudha wengi wa Rakhine kuwa kambi yake. (The Business Standard, 18 Juni 2025)
Wiki hii iliyopita kumeshuhudiwa vurumai kubwa la vyombo vya habari na kisiasa kutokana na machapisho ya mitandao ya kijamii ambapo Waislamu waliwapongeza wahitimu wa mwaka huu huku pia wakiwasilisha mtazamo wa Kiislamu kuhusu kupanda malori ya kuhitimu yenye sifa ya ulevi na tabia mbaya.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan inauona utambuzi huu kama sehemu ya mchakato mpana ambao kwao utawala wa sasa utayeyushwa hatua kwa hatua ndani ya mfumo wa kimataifa wa kisekula wa dola ya kitaifa. Mfumo huu, baada ya muda, utaiweka mbali serikali hii na lengo kuu la Kiislamu la kusimamisha na kubeba Dini ya Mwenyezi Mungu (swt). Zaidi ya hayo, utambuzi huo unaweza kuigeuza Afghanistan kuwa uwanja wa vita vya kiushindani kati ya dola za kikanda na kimataifa.
Semina ya Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia kwa mnasaba wa Mwaka Mpya wa Kiislamu kwa kichwa "Hijrah... Kuzaliwa kwa Dola ambayo itaikoa Gaza."
Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh, iliandaa maandamano na matembezi leo (Ijumaa, 4 Julai 2025) baada ya swala ya Ijumaa katika misikiti mbalimbali ya Dhaka na Chittagong kupinga uhamishaji unaoendelea wa India wa Waislamu hadi Bangladesh kwa mtutu wa bunduki. Wanachama mbalimbali wa Hizb ut Tahrir walitoa hotuba katika maandamano hayo ambayo yalimalizika sambamba na matembezi.
Serikali ya Hindutva ya Modi inaendelea kuongeza kiwango cha ukandamizaji na mateso, ikiwa ni pamoja na kubomoa nyumba za Waislamu wa India na kuwapeleka uhamisho kwa nguvu usio wa haki. Kupitia hili kimsingi wanafuata nyayo za dola haramu ya Kiyahudi ‘Israel’. Hivi karibuni, hata wanawatendea Waislamu wa India kama wanyama kwa kuwaita wahamiaji haramu na kuwarudisha mamia yao nchini Bangladesh kwa mtutu wa bunduki, wakipuuza kile kinachoitwa michakato yao ya kisheria ya kitaifa na kimataifa. "Walitutendea kama wanyama," alisema mwanamke mmoja anayeitwa Rahima Khatun. "Tulipinga kwamba sisi ni Wahindi, kwa nini tuingie Bangladesh? Lakini walituelekezea bunduki na kutishia, 'Ikiwa hamtakwenda kwa huko, tutakupigeni risasi.' Baada ya kusikia milio minne ya risasi kutoka upande wa India, tuliogopa sana na haraka tukavuka mpaka kwa miguu". [Ripoti ya FP].
Sisi, katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, tunafuraha kuwaalika wanataaluma wa vyombo vya habari, wanasiasa, na wale wanaohusika na masuala ya umma kuhudhuria na kushiriki katika Kikao cha Masuala ya Ummah wa kila mwezi, ambacho mwezi huu kitakuwa na kichwa: “Hatari ya Kuyatazama Mamlaka Kama Keki Inayopaswa Kugawanywa”