Uislamu uko Mbali na Mazungumzo ya Dini Mseto
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo tarehe 5 Julai 2025, jumba jipya la ibada katika Kanisa la Arise and Shine Tanzania lililopo Kawe, viungani mwa jiji la Dar es Salaam lilizinduliwa. Kanisa hilo linaongozwa na Mwinjilisti na anayejiita ‘mtume’ Boniface Mwamposa ambaye mahubiri yake mwaka 2020 yalileta msiba wa vifo vya waumini zaidi ya 20 kutokana na mkanyagano waliokuwa wakikimbia kupakwa mafuta yenye baraka.