Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 296
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Vichwa Vikuu vya Toleo 296
Vichwa Vikuu vya Toleo 296
Kwa hakika nyinyi ni Ummah bora miongoni mwa wengine wote, ulioletwa kwa watu, kwa sababu mnashikamana kile ambacho Mwenyezi Mungu ameamrisha na mnakataza kile ambacho Mwenyezi Mungu amekikataza na mna muamini Mwenyezi Mungu (swt).
Mauwaji ya halaiki ya Srebrenica yalikuwa ni janga la kuogofya katika historia ya wanadamu. Mauwaji hayo ya halaiki yalifanyika katika miji ambayo Baraza la Usalama liliitambua kama maeneo salama, lakini kisha likakataa kuidhinisha vikosi vya kutosha kuyalinda.
Vyombo vya habari vya Uingereza vimepata ubabaishaji mpya kutokana na hali mbaya ya uchumi wa Uingereza.
Miaka 25 imepita sasa ambapo zaidi ya wavula na wanaume wa Kiislamu 8,000 kutoka Srebrenica, mji mdogo, ulio na wakaazi wengi mno, nchini Bosnia, waliuwawa katika yale yanayo onekana sasa kuwa ndio mauwaji mabaya zaidi katika ardhi ya Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia.
Ibn Kathir ameeleza katika tafsiri yake ya aya, maana, chuki imedhihiri kwenye nyuso zao, na katika yale wanayoyatamka baadhi ya wakati, pamoja na, uadui walio nao dhidi ya Uislamu na watu wake katika vifua vyao.
Mwezi huu wa Julai unafikisha mwaka wa 25 tangu mauwaji na halaiki ya Waislamu wa Bosnia eneo la Srebrenica ambayo ni uhalifu uliotekelezwa na Jeshi la Kibosnia la Waserbia, likiongozwa na 'Mchinjaji wa Bosnia', mhalifu wa kivita Ratko Mladic.
Waziri wa Haki wa Sudan Nasruddin Abdel-Bari amefichua maelezo mapya kuhusu sheria ya mabadiliko tofauti tofauti, ambayo itachapishwa katika gazeti rasmi la serikali siku ya Jumapili 12/7/2020,
Katika kutoa heshima kwa maelfu ya Waislamu hususan wanaume na vijana waliouliwa katika mauaji ya Julai 1995 wakati wa vita vya Balkan, António Guterres aliahidi kuwa hawatosahauliwa kattu.
"Ummah Wenu ni Mtukufu: Msiudunishe!"