Kuanguka kwa Khilafah Kunaashiria Wito wa Kuhuishwa Kwake
- Imepeperushwa katika Pakistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo tarehe 3 Machi 1924, sawia na 28 Rajab 1342 H, kikundi kidogo cha wasaliti wa Kituruki, wakiongozwa na Mustafa Kemal, walivunja urithi wa zaidi ya karne 13 za umoja wa Waislamu. Kuanzia wakati huo na kuendelea, Waislamu walipoteza paa lao juu ya vichwa vyao na wakawa mayatima. Leo, miaka 104 ya hijria imepita tangu tukio hili la kusikitisha. Baada ya kuanguka kwa Khilafah, makafiri waligawanya ulimwengu wa Kiislamu katika maeneo madogo yaliyojitenga. Waliweka vikwazo vya usafiri kati ya maeneo haya, yakihitaji pasipoti na visa, na kuharibu majeshi yetu, silaha, rasilimali, ardhi, uwezo wa binadamu, na teknolojia-kila kitu.



