Kuongezeka kwa Misimamo Mikali ya Hindutva ni Matokeo ya Moja kwa Moja ya Sera ya Kisekula ya Kigeni ya Pakistan! Khilafah Itapitisha Sera ya Kigeni, iliyojengwa juu ya Msingi wa Kubeba Ujumbe wa Kiislamu wa Tawhid kwa Ulimwengu Mzima
- Imepeperushwa katika Pakistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo tarehe 22 Januari 2024, Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, alizindua Ram Mandir maarufu, kwa shangwe na sherehe nyingi. Likiwa katika mji wa Ayodhya, hekalu hilo la Kibaniani lilijengwa juu ya magofu ya Msikiti wa Babri, nembo kuu ya utawala wa Waislamu juu ya bara hilo dogo, ambao ulivunjwa na makundi ya Mabaniani mwaka wa 1992.