Alhamisi, 07 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  26 Dhu al-Hijjah 1445 Na: 1445 / 49
M.  Jumanne, 02 Julai 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Bajeti ya IMF Imeleta Maafa Kwa Waislamu. Ni Hukmu za Kiislamu Pekee ndizo Zinazoweza Kutoa Ufueni, kwa Kutatua Migogoro Mikuu ya Kiuchumi

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 12 Juni 2024, Waziri wa Fedha wa Pakistan aliwasilisha bajeti ya serikali ya shirikisho kwa mwaka wa 2024-2025, ambayo ilisheheni ushuru mkubwa, na kusababisha hofu miongoni mwa watu. Bajeti hiyo ilipitishwa na bunge mnamo tarehe 28 Juni, baada ya kutoza ushuru zaidi, ambao haukuwa sehemu ya bajeti ya awali! Waziri Mkuu amekiri wazi kuwa bajeti hii imefanywa kwa uratibu na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF). Kwa hivyo, watawala walivuka mstari wa kutokuwa na aibu, wakikiri wazi kwamba wao ni vibaraka wa mfumo wa sasa wa ulimwengu wa ulimwengu, na wanafanya kazi pamoja na wakoloni.

Kwa kutenga asilimia 52 ya bajeti yote kwa malipo ya riba pekee, maslahi ya wananchi, serikali na usalama yanahujumiwa. Kwa kweli, serikali ya shirikisho haina pesa za kulipa riba hii, baada ya kulipa majimbo kutoka kwa pesa zilizokusanywa kutoka kwa ushuru. Kwa hivyo, serikali ya shirikisho italazimika kukopa ili kutumia kwa mahitaji ya umma, ulinzi, maendeleo na usalama wa kijamii. Pesa zitapatikana kwa kuchukua mikopo zaidi. Kwa hivyo, Pakistan imekwama katika hali mbaya ya kiuchumi. Khilafah ndiyo itakayomaliza nakisi ya fedha kwa kusitisha malipo ya riba mara moja. Itakusanya ushuru ulioidhinishwa na Shariah kutoka kwa wenye uwezo wa kifedha. Kamwe haitawatoza masikini na wenye deni, wanaostahiki Zaka. Itatumia mapato ya serikali kwa mahitaji ya umma, Jihad na maendeleo.

IMF ni taasisi ya kikoloni inayotokana na Mkataba wa Bretton Woods. Inafanya kazi kwa ukiritimba wa dolari ya Marekani juu ya biashara ya kimataifa. Inahakikisha utawala wa kiuchumi na kisiasa wa Marekani. Bajeti iliyoundwa kwa amri za wakoloni inahalalishwa kwa kusema kwamba ni muhimu kuepusha kushindwa kulipa madeni. Kwa kweli, IMF inahakikisha malipo ya riba kwa wakopeshaji wa mikopo kwa dolari na rupia, hata ikiwa inasababisha watu kufilisika, kujiua au watoto wao kulala njaa. Khilafah itaizamisha Titanic ya dolari, itakapotoa sarafu inayoegemezwa kwa dhahabu na fedha. Itaondoa uwezo wa serikali wa kuchapisha noti inavyopenda, ambapo hupora mifuko ya watu kupitia mfumko mbaya wa bei. Pia itamaliza suala la sasa la nakisi ya biashara ya kigeni, kwa kubadilisha biashara ya kimataifa hadi kwa dhahabu na fedha, pamoja na kumakinisha sekta ya ndani yenye nguvu.

Khilafah itakomesha sera ya ubinafsishaji iliyoamrishwa na IMF, ambayo imesababisha uharibifu wa sekta ya nishati, mafuta na gesi. Badala yake itatabikisha hukmu ya Kiislamu ya umilikaji wa umma, kuhusu nishati na madini. Ubinafsishaji umehakikisha faida kubwa kwa wamiliki binafsi, huku ukivunja mgongo wa watu. Al-Tirmidhi amesimulia kutoka kwa Abyad b. Hammal, أَنَّهُ وَفَدَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَاسْتَقْطَعَهُ الْمِلْحَ فَقَطَعَ لَهُ فَلَمَّا أَنْ وَلَّى قَالَ رَجُلٌ مِنْ الْمَجْلِسِ أَتَدْرِي مَا قَطَعْتَ لَهُ إِنَّمَا قَطَعْتَ لَهُ الْمَاءَ الْعِدَّ قَالَ فَانْتَزَعَهُ مِنْهُ Kwamba alikwenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na kumuomba amkatie kipande cha ardhi chenye madini ya chumvi. Kwa hivyo akamkatia. Aliporudi, mtu mmoja katika kikao akauliza: Je! Unajua umemkatia nini ? Umemkatia maji ya chemchemi ya kudumu. Hivyo akaichukua kutoka kwake.” Maji ya kudumu ni yale ambayo hayamaliziki, kwa maana nyengine, ikiwa umechimba madini kutoka humo, hayamaliziki. Sunnah ya Mtume imeweka hukmu ya Kiislamu kuhusu mali ya umma. Hivyo basi, Khilafah itazuia ubinafsishaji wa nishati na madini, pamoja na huduma za jamii kama vile barabara, mito, bahari, maziwa, mikondo ya umma, ghuba, bahari, misikiti, shule za serikali, mahospitali, viwanja vya michezo na malazi. Khilafah itatumia mapato ya mali ya umma kwa mahitaji ya umma, na kukomesha uzembe wa kihalifu wa mambo yao.

Khilafah itauunganisha ulimwengu wa Kiislamu katika dola moja kwa njia ya kimsingi. Itaunda soko moja miongoni mwa ardhi za Waislamu, kwa kukomesha dola ndogo zilizofeli zilizoundwa na Waingereza, Wafaransa, Warusi na Wamarekani. Kisha rasilimali za mafuta na gesi za Qatar, Saudi Arabia, Iran, Asia ya Kati na Imarati zitapatikana kwa kila mtu kutoka Indonesia hadi Morocco. Pakistan, Misri, Bangladesh, Nigeria na Sudan zitakuwa vikapu vya chakula kwa Umma mzima. Vikosi vya kijeshi vya Pakistan, Bangladesh, Indonesia, Algeria, Misri na Uturuki vitaulinda Ummah mzima. Uturuki, Iran, Misri, Pakistan, Bangladesh na Malaysia zitatoa miundombinu ya viwanda kwa Ummah. Muungano pekee ndio utakaougeuza Ummah huu kuwa uchumi mkubwa zaidi duniani.

Watawala wa Pakistan, pamoja na wale wa nchi nyingine za Kiislamu, wote ni vibaraka duni wa ukoloni, ambao barakoa zao sasa zimepomoka kabisa. Wao ni makamu wa wakoloni wanaopora makoloni, kwa kutoza ushuru mkubwa, kuitajirisha London, Washington, Paris na Beijing kupitia malipo ya riba. Ummah na majeshi yake lazima wawang'oe watawala hawa, ambao ni vibaraka wa ukoloni na wanakiuka hukmu za Kiislamu. Umma lazima uyatake majeshi yake yaipe Nusrah Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, ambayo itatokomeza nguvu dhalimu ya kikoloni.

Afisi ya Habri ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu