Alhamisi, 21 Rabi' al-awwal 1443 | 2021/10/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  23 Dhu al-Qi'dah 1442 Na: 1442 / 87
M.  Jumapili, 04 Julai 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ni wazi Kutokana na Maelezo ya Usalama wa Kitaifa kwamba Serikali ya Bajwa-Imran Haina Ruwaza Nyengine Ila ya Utumwa kwa Dola za Wakoloni

(Imetafsiriwa)

Mnamo 1 Julai 2021, katika Jumba la Bunge, Jenerali Bajwa na Mkurugenzi Mkuu wa ISI, Luteni Jenerali Faiz Hameed, waliuelezea uongozi wa kisiasa juu ya hali ya usalama wa kitaifa, haswa kuhusu Afghanistan. Uangaziaji wa vyombo vya habari uliofuata wa mkutano huo wa masaa nane unaweka wazi kuwa uongozi wa kisiasa na kijeshi uko katika ukurasa mmoja wa utumwa wa wakoloni, kwa Amerika pamoja na China. Wote wanakubali kwamba uwezo mkubwa wa Pakistan unatakiwa utumiwe ili kupata ushawishi wa Amerika ndani ya Afghanistan, baada ya kushindwa kwake kwa aibu. Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan inatoa hoja zifuatazo katika suala hili:

1) Waislamu wa Pakistan na vikosi vyao vya kijeshi lazima wapinge kikamilifu unyonyaji wa uwezo mkubwa wa kijeshi, kisiasa na kidiplomasia wa Pakistan, na vilevile mafungamano ya kina ya kindugu ya Kiislamu, ili kuilinda serikali kikaragosi ya Amerika yenye kupigana vita vya kimsalaba jijini Kabul, kutokana na kusonga mbele bila ya kukoma kwa upinzani wa Afghanistan. Kushirikiana na adui kafiri mshambulizi imeharamishwa kabisa katika Uislamu na ni khiyana ya wazi kwa Mwenyezi Mungu (swt), Mtume wake (saw) na waumini. Lakini, watawala wa Pakistan hufanya kama wawezeshaji walioajiriwa kuzuia ukombozi wa Kabul, wakilazimisha upinzani wa Afghanistan kuachana na utabikishaji kamili wa Sharia ya Kiislamu, kwa jina la kugawanya mamlaka na vibaraka duni wa Amerika.

2) Waislamu wa Pakistan na vikosi vyao vya kijeshi lazima wadai kukatwa mara moja kwa laini za usambazaji za GLOC na ALOC kwa wanajeshi wa kimsalaba wa Amerika, ambazo ni muhimu kudumisha miundombinu ya Amerika katika eneo letu baada ya kujiondoa, ikipewa uwezo "juu ya upeo" ambao haingeweza kamwe kujipatia. Ushirikiano kama huo na Amerika ni kuwezesha makadirio ya nguvu ya anga, kuzuia ukombozi wa Kabul na maeneo mengine muhimu ya kimkakati kutoka kwa ushawishi wa Amerika, ikionyesha muundo ambao Amerika iliutabanni kwa Iraq.

3) Waislamu wa Pakistan na vikosi vyao vya kijeshi lazima wakatae uwekaji uzio wa mpaka kwenye Laini ya mkoloni ya Durand, ambayo ni mbinu ya ujanja ya Amerika ya kukata uhusiano wa dhati, na wa muda mrefu wa kindugu wa Kiislamu kati ya Waislamu wa Afghanistan na Pakistan, kupitia kukuza uhasama mkali wa utaifa angamivu na kuzuia matembezi huru ambayo daima yameimarisha upinzani wa pamoja dhidi ya ushawishi wa kigeni wa eneo hili. Waislamu katika nchi hizi mbili za Kiislamu wanamuamini Mwenyezi Mungu mmoja (swt), Mtume mmoja (saw) na Kitabu kimoja Kitukufu na lazima waendelee kuwa macho juu ya hatari za moto wa sera ya mkoloni ya gawanya utawale.

Enyi Waislamu wa Pakistan na Jeshi lao! Serikali ya Bajwa-Imran haina ruwaza ya kisiasa ila utumwa wetu na dola zinazopinga Uislamu kama Amerika na China. Kwa usaidizi wa kisiasa na kijeshi wa Waislamu wa Afghanistan, hapo awali mliitoa dola kuu Usovieti ya Urusi, huku sasa upinzani mtukufu wa Afghanistan ikiwa umeyashinda majeshi ya muungano wa nchi arubaini na mbili, bila chochote isipokuwa silaha za kawaida na Imani thabiti, isiyoweza kutikisika. Je! Huu sio uthibitisho tosha kwamba udhaifu wetu sio kupitia ukosefu wa rasilimali za kijeshi na uchumi, lakini kupitia kwa vibaraka wa wakoloni walioidhinishwa na Amerika, ambao hutulemea kwa ushirikiano wao wa khiyana na maadui zetu? Amerika inategemea uwezo wetu kwa ajenda yake ya kieneo, kwa hivyo ni nini kinatuzuia kutekeleza ajenda ya Uislamu ya kuunganisha Afghanistan, Asia ya Kati na Pakistan na kwengineko kama Khilafah moja? Mzikeni Raj wa mkoloni Amerika kwa mikono yenu, kwa kujitahidi kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume mahali pake. Kilimo shupavu cha Pakistan kitatupa mahitaji yetu ya chakula, akiba kubwa ya nishati ya Bahari ya Caspian itakidhi mahitaji yetu ya nishati na makaburi ya himaya, Afghanistan, itaimarishwa na nguvu ya jeshi la Pakistan na nguvu ya nyuklia, ili kulinda ardhi zetu. Kwa hivyo, Waislamu wa Jeshi la Pakistan! Jitokezeni kutoa Nusrah yenu kwa Hizb ut Tahrir ili mwishowe muongozwe na watawala wasiyemtii yeyote ila Mwenyezi Mungu (swt), kwa kumtegemea Yeye (swt) Peke Yake. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

 [وَاللَّهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]

“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.” [Surah Yusuf 12:21].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-pakistan.com/

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu