Jumapili, 17 Dhu al-Hijjah 1445 | 2024/06/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  4 Shawwal 1445 Na: 1445 / 44
M.  Jumapili, 05 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tangu tarehe 11 Mei 2012, Naveed Butt, Msemaji wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan Alisalia katika Kupotezwa kwa Kulazimishwa kwa Sababu Anaitetea Khilafah Rashida

(Imetafsiriwa)

Kutekwa nyara kwa Naveed Butt tangu tarehe 11 Mei 2012, ni dhambi kubwa na ukiukaji wa wazi wa haki za binadamu. Hakuna kesi ya ugaidi, uasi au uhaini iliyosajiliwa dhidi ya Naveed Butt. Zaidi ya hayo, hakuna kesi hata ya kumdhuru nzi, au kung'oa jani kutoka kwa mti, ya Naveed Butt mwenye huruma na mkarimu. Uongozi kadhaa wa kijeshi na kisiasa umebadilika tangu kutekwa nyara kwake, hata hivyo, Naveed bado hana uhuru wa kuilingania Khilafah Rashida. Kwa nini?! Huku uongozi huu wa kijeshi na kisiasa ukija na kuondoka, bwana wao wote, Marekani, amebakia. Wito wa kuunganishwa kwa Ulimwengu wa Kiislamu kama dola moja uko nje ya dira finyo, duni ya uongozi wa kisiasa na kijeshi wa kitumwa. Hata hivyo, ni wito unaotoa tahadhari katika Ikulu ya White House, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na Pentagon. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «وَمَنْ عَادَى أَوْلِيَاءَ اللَّهِ فَقَدْ بَارَزَ اللَّهَ بِالْمُحَارَبَةِ» “Na yeyote atakayeonyesha uadui kwa Awliya (walio waliokaribu na Mwenyezi Mungu) ametangaza vita na Mwenyezi Mungu.” [Hakim amesimulia kuwa ni Sahih kutoka kwa Mu'aadh bin Jabal] Ilhali, watawala wa Pakistan hawazingatii hili!

Naveed Butt ni kiongozi mwenye uwezo wa Umma wa Kiislamu, katika wakati ambapo kuna mgogoro wa uongozi. Naveed Butt ni mwana mwenye kipaji na mahiri wa Ummah, mhandisi mwenye shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Illinois. Yeye ni msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan. Hizb ut Tahrir chama kikubwa zaidi cha kisiasa cha Kiislamu katika ulimwengu wa Kiislamu. Wito wake wa kusimamishwa Khilafah unatazamwa kwa heshima kote Pakistan. Licha ya kupotezwa kwake kwa nguvu mnamo tarehe 11 Mei 2012, hadi leo, watu wanasambaza makala, mahojiano na vipande vya video zake kuhusu suala la Khilafah kwenye mitandao ya kijamii. Kazi yake juu ya utawala wa Kiislamu, uchumi, mahakama, mambo ya nje, elimu na uundaji wa familia katika jamii, zimeendeleza wito wa Khilafah kutoka katika kauli mbiu isiyoeleweka, hadi kwenye ruwaza iliyo wazi na ya kina. Ilhali, wao wenyewe wameshindwa kuwaongoza Waislamu ipasavyo, watawala wa Pakistan wanamweka Naveed kwenye korokoro zao. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[إِنَّ الَّذِينَ يُحَادُّونَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ أُوْلَئِكَ فِي الأَذَلِّينَ]

“Hakika wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hao ndio miongoni mwa madhalili wa mwisho.” [Surah Al-Mujadilah 58:20]. Ilhali watawala wa Pakistan hawajisalimishi kwa unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu (swt)!

Naveed Butt amepotezwa kwa nguvu tangu tarehe 11 Mei 2012, kwa sababu alinyanyua neno la haki dhidi ya watawala madhalimu. Je, sio wakati sasa wa kumwachilia huru Naveed wakati Tume ya Uchunguzi ya Pakistan kuhusu Upotezwaji kwa Nguvu imetoa agizo la kutolewa, mnamo tarehe 4 Januari 2018, kwa nambari ya marejeleo ColoED ID No. 860-P? Lakini, watawala wa Pakistan hawatii, kwa sababu hawasubutu kuinua kidole bila ya idhini ya Marekani. Hata hivyo, kusema ukweli mbele ya watawala madhalimu sio kosa. Badala yake, ni wajibu muhimu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«أَلَا لَا يَمْنَعَنَّ أَحَدَكُمْ رَهْبَةُ النَّاسِ أَنْ يَقُولَ بِحَقٍّ إِذَا رَآهُ أَوْ شَهِدَهُ فَإِنَّهُ لَا يُقَرِّبُ مِنْ أَجَلٍ وَلَا يُبَاعِدُ مِنْ رِزْقٍ»

“Jueni hofu ya watu isimzuie mmoja wenu kusema neno la ukweli pindi anapoliona au kulisikia, kwani kufanya hivyo hakufupishi ajal (uhai) wala hakuongezi riziki” [Ahmad] Ni Naveed Butt ndiye bila ya uoga aliwahisabu watawala juu ya kuwezesha kwao shambulizi la Marekani dhidi ya Abbottabad. Ni Naveed ndiye ambaye alipinga kwa ujasiri usaliti wao kwa Kashmir na Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, pamoja na uharibifu wao wa uchumi kupitia kujisalimisha kwao kiupofu kwa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF).

Utekaji nyara kwa nguvu wa Naveed Butt tangu tarehe 11 Mei 2012 unafichua uongo wa Demokrasia na uhuru wa kujieleza. Watoto wa Naveed Butt wamekua bila ya ulezi wa baba yao, huruma na upendo, kwa sababu tu Naveed alipaza sauti yake kwa ajili ya Dini ya Mwenyezi Mungu (swt) ifuatwe katika ngazi ya serikali, jamii na maisha jumla. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَمَنْ لَمْ يَحْكُمْ بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الظَّالِمُونَ]

“Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhaalimu.” [Surah Al-Maida 5:45]. Ni katika sheria gani ya mbinguni, au duniani, ambapo usemi huo wa kisiasa na kidini ni uhalifu? Hakika, kesi ya Naveed Butt inathibitisha kwamba Demokrasia ni utawala dhalimu, ambao unalinda tu maslahi ya wakoloni na vibaraka wao. Je, sio wakati sasa wa waandishi wa habari, wanaharakati wa haki za binadamu, wanasheria na maulamaa kupaza sauti zao kutaka Naveed Butt aachiliwe huru mara moja? Je, wakati haujawadia sasa kwamba wote washiriki katika ujira wa kuregesha utawala kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt) ambapo ni faradhi kubwa iliyofaradhishwa na Mwenyezi Mungu (swt)?

Enyi Waislamu wa Jeshi la Pakistan! Naveed Butt imepoteza kwa lazima tangu tarehe 11 Mei 2012, kwa sababu bado hamjatimiza wajibu wenu. Naveed Butt alitaka kwamba mutoe Nusrah yenu kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah Rashida. Anaheshimu wajibu wake kwa Mwenyezi Mungu (swt) hadi leo, huku nyinyi mmebakia katika mapuuza yenu. Je, mutakubali kubaki katika dhambi hadi lini? Mnaweza kukaa kimya katika dhambi na hali Mwenyezi Mungu (swt) ameitayarisha dunia kwa ajili ya kuregea Khilafah Rashida? Upinzani mkali wa Waislamu wa Gaza umefichua udhaifu wa umbile la Kiyahudi na ufisadi wa mfumo wa kilimwengu wa Marekani. Watawala wa Waislamu wote wamefichuliwa kupitia kuzuia kwao majeshi ya Waislamu na nia yao ya kusalimisha sehemu kubwa ya Palestina kwa umbile la Kiyahudi, kupitia suluhisho la dola mbili la Marekani. Watu wenye uadilifu wa fikra wa Mashariki na Magharibi wamehofishwa na mauaji ya halaiki ya Gaza na hawatatoa machozi kwa kumalizika dhulma. Zaidi ya yote, Mwenyezi Mungu (swt), An-Naseer, Atakuleteeni Nasr Yake, ikiwa mutahamasika katika kumtii. Komesheni Fitnah, wakamateni madhalimu, sahisheni makosa mupate radhi za Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[وَاتَّقُوا فِتْنَةً لاَ تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْكُمْ خَاصَّةً وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ]

“Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu walio dhulumu peke yao kati yenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” [Surah Al-Anfaal 8: 25].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu