Alhamisi, 28 Jumada al-thani 1447 | 2025/12/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  10 Jumada II 1447 Na: BN/S 1447 / 10
M.  Jumatatu, 01 Disemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Moyo wa Hebron na Msikiti wa Ibrahimi Wafanywa Kuwa wa Kiyahudi kwa Kufuata Hatua Zile Zile kama Ulivyofanywa kuwa wa Kiyahudi Msikiti wa Al-Aqsa
(Imetafsiriwa)

Baada ya umbile la Kiyahudi kuamua kuhamisha mamlaka ya kiidara ya Msikiti wa Ibrahimi kutoka Manispaa ya Hebron hadi “Baraza la Kidini la Kiyahudi huko Kiryat Arba,” na baada ya umbile hilo kukataa pingamizi iliyowasilishwa na Manispaa ya Hebron kuhusu uamuzi huu, pamoja na uamuzi uliofuata wa kugeuza ua wa ndani wa Msikiti wa Ibrahimi kuwa uwanja wa umma, na pamoja na vyama vya Kiyahudi vinavyofanya kazi ya kununua nyumba katika mji wa Hebron (al-Khalil) - moyo wa Mji wa Hebron, huku Msikiti wa Ibrahimi ukiwa kiini chake, unafanywa kuwa wa Kiyahudi waziwazi mbele ya ulimwengu na mbele ya Umma wa Kiislamu, kama vile eneo la Safari ya Usiku ya Mtume wake (saw) na viunga vyake linavyofanywa kuwa la Kiyahudi.

Kuchukuliwa kwa Msikiti wa Ibrahimi kulifanyika baada ya Makubaliano ya Oslo, haswa kufuatia mauaji yake mwaka wa 1994, baada ya hapo umbile hilo lilianzisha “Tume ya Shamgar,” ambayo iligawanya msikiti baina ya waabudu wake Waislamu na Mayahudi wanyang'anyi, ikiwapa Waislamu theluthi moja na Mayahudi theluthi mbili, kama zawadi kwa mauaji waliyoyafanya msikitini. Kisha, mnamo 1997, Shirika la Ukombozi wa Palestina (PLO) liliidhinisha Itifaki ya Hebron, upanuzi wa Makubaliano ya Oslo yenye hila, ikigawanya mji katika Maeneo H1 na H2. Hii iliwezesha udhibiti wa Mayahudi juu ya sehemu ya kusini ya Mji wa Hebron, Mji wa Kale, na Msikiti wa Ibrahimi.

Inashangaza kwamba Itifaki ya Hebron yenye sifa mbaya haishambuliwi wala kulaaniwa, licha ya kuwa makubaliano yenyewe yaliyotoa uhuru kwa uvamizi katikati ya Mji wa Hebron na juu ya Msikiti wa Ibrahimi, huku lengo likiwa ni kushambulia mahakama za uvamizi ambazo kwazo haki inatafutwa! na kuelekeza maombi kwa Umoja wa Mataifa, ambao umefumbia macho uhalifu wote wa umbile hilo halifu, isipokuwa mara kwa mara kuelezea “wasiwasi,” lakini Baraza lake la Usalama hivi karibuni lilitoa uamuzi unaoweka Gaza chini ya udhamini wa Marekani na kuwapa Mayahudi mamlaka kamili ya kufanya chochote wanachotaka.

Hakika, inashangaza kwamba taasisi zinamgeukia muuaji mwenyewe zikidai haki, kuregeshwa kwa misikiti na matukufu yetu, bila kupaza sauti zao kwa wale waliosaini Makubaliano ya Oslo na kisha Itifaki ya Hebron, mzizi wa janga hili lililoanza na makubaliano hayo ya hila ya kuachilia ardhi ya Uislamu na Waislamu. Kinachohitajika kidogo zaidi, ingawa hakiwezi kamwe kuondoa uhalifu wa kupeana ardhi ya Palestina na kutelekeza matukufu ya Waislamu, ni kutangaza kukataliwa kwa Makubaliano ya Oslo na kupinga dhambi zote zilizofuata na zilizojengwa juu yake, makubaliano ambayo yanakubali sehemu kubwa ya ardhi iliyobarikiwa ya Palestina na ambayo uvamizi huo hutumia kujihalalisha, kuyaweka kando chini ya miguu yake kila yanapokinzana na mipango yake.

Enyi Waislamu: Msikiti wa Ibrahimi umekuwa sinagogi la Kiyahudi ambapo hufanya ibada zao za batili. Kukabiliana na hatua zao hakufikiwi tu kwa kuwaita Waislamu kuswali huko, bali kwa kukemea uhalifu wa Mamlaka ya Palestina, ambao ni uhalifu wa “Oslo” na kudai kufutwa kwake pamoja na matokeo yake yote, ili suala hilo lirudi kwenye msingi wake wa asili: “kwamba hii ni ardhi inayokaliwa kimabavu ambayo umbile hilo halina uhalali wake, na kwamba Umma wa Kiislamu lazima utetee matukufu yake. Msikiti wa Ibrahimi, mithili ya Msikiti wa Al-Aqsa, ni mojawapo ya matukufu ya Kiislamu sio urithi wa Palestina’ bali ni urithi wa umma ambao ni wa Bwana wa Viumbe, Muhammad (saw). Umma huu ndio unaomiliki kadhia hiyo, na ndio mwakilishi halali wa wito wa kutimiza wajibu wake sio vyombo vya kimataifa vilivyoanzisha umbile hilo na kulinda jinai zake kwa karne moja, wala mahakama za umbile hilo zenyewe.”

Kila jaribio la kutatua kadhia ya Palestina nje ya muundo wa Uislamu na bila mikono ya Waislamu si chochote ila ni kupoteza kadhia hiyo, kumhalalisha mnyang'anyi, na usaliti unaowapa wahalifu wake aibu ya milele katika ulimwengu huu na udhalilifu kesho Akhera. Ama kuhusu hatua zote zilizochukuliwa na Mayahudi, hazingekuwa na uwepo au athari yoyote hata kama ulimwengu wote ungezikubali lau kama Ummah na majeshi yake hawangechelewa kutimiza wajibu wao kwa matukufu yao: Msikiti wa Al-Aqsa, Msikiti wa Ibrahimi, na Ardhi yote iliyobarikiwa; na kama hawangesita kulinda heshima na damu ya watu wake. Lakini kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kuchelewa huku hakutaendelea kwa muda mrefu. Hakika, Ummah leo unaonekana uko tayari kuelekea Palestina, ukiendeshwa zaidi na kile unachokiona kila siku cha Mayahudi kutojali zaidi dhidi ya ardhi na watu wake. Mapinduzi ya Ummah dhidi ya wale walioisaliti na kuitelekeza yanakuja hivi karibuni, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu - kufuta umbile hilo na kuling'oa, kusafisha misikiti na ardhi kutokana na uchafu wake, na kutakasa Ummah kutokana na wasaliti waliomsaliti Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن مَّنَعَ مَسَاجِدَ اللَّهِ أَن يُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ وَسَعَىٰ فِي خَرَابِهَا أُولَٰئِكَ مَا كَانَ لَهُمْ أَن يَدْخُلُوهَا إِلَّا خَائِفِينَ لَهُمْ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ]

“Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye zuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kutajwa ndani yake jina lake na akajitahidi kuiharibu? Watu hao haitawafalia kuingia humo ila nao wanaogopa. Duniani watapata hizaya na Akhera watapata adhabu kubwa.” [Al-Baqarah: 114].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 0598819100
www.pal-tahrir.info
E-Mail: info@pal-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu