Jumamosi, 05 Rabi' al-awwal 1444 | 2022/10/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  21 Dhu al-Hijjah 1443 Na: 08 / 1443
M.  Jumatano, 20 Julai 2022

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Fahari ya Umma inatokana na Fahari ya Watawala Wake
(Imetafsiriwa)

Chanzo kimoja cha habari kiiliarifu "Ultra Sudan", 18/7/2022, kwamba Balozi wa Uingereza nchini Sudan, Giles Leifer, alipotembelea makaazi ya Rais wa Baraza Kuu la Mpito, Abdel Fattah Al-Burhan, wakati wa sikukuu ya Idd al-Adha huko Qandto, Jimbo la Mto Nile, alijadili kesi ya mwanamke mmoja wa Kisudan anayekabiliwa na hukumu ya kifo kwa kupigwa mawe dhidi ya tukio la uzinzi, kwa mujibu wa uamuzi uliotolewa na jaji mmoja wa mahakama katika jimbo la White Nile mwezi uliopita. Afisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza imetoa mwanga kuhusu kesi hii na ilishughulikiwa katika ngazi za juu za diplomasia ya Uingereza, kulingana na kile chanzo hicho kilichosema. Chanzo hicho kilisema kuwa balozi wa Uingereza alizungumza na Al-Burhan kuhusiana na kesi hii kwa sababu Afisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza ina wasiwasi kuihusu.

Kwa kuzingatia uingiliaji huu wa wazi wa Makafiri, maadui wa Uislamu, katika mambo ya wanawake, tunafafanua yafuatayo:

Kwanza: Ukiukaji wa makafiri dhidi ya Uislamu na hukumu zake unasababishwa na ukweli kwamba hawakupata miongoni mwa watawala mtu ambaye angetabanni hukumu hizi, kuzitabikisha, kuzihami, na kuwaadhibu vibaraka wote wanaosubutu kuwashambulia.

Pili: Udhaifu wa watawala ulizidisha ushupavu na uingiliaji wa serikali za Kimagharibi katika masuala ya Waislamu na kutafuta visingizio na uhalali wa hilo. Kwa hivyo, lengo kuu la kampeni yao dhidi ya Uislamu likawa ni kushambulia fikra msingi za Kiislamu zinazohusiana na wanawake na familia, zinazowapa Waislamu kitambulisho chao na kuwatofautisha na wengine; kwamba wao ni waja wa Mwenyezi Mungu waliojisalimisha kwa Mwenyezi Mungu (swt) peke yake.

Tatu: Fahari ya Ummah inatokana na fahari ya watawala wake. Wafalme wa Warumi na Wafursi walikuwa wakimuogopa Khalifa wa Waislamu, na walitetemeka walipojua kwamba kulikuwa na ujumbe kwao kutoka kwa Khalifa. Yule anayemsifu Khalifa Omar Ibn Al-Khattab, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, alisema kwa haki: “Kiti cha enzi cha Kisra hutikisika anapotajwa, na wafalme wa Warumi walimwogopa.”

Enyi Umma wa Uislamu mpaka lini mtawaacha wale waliovaa vazi la udhalilifu, aibu na fedheha wawatawale kwa faida ya makafiri, maadui wa Dini hii, hali Shariah imeamrisha kuondolewa mtawala ambaye uamuzi wake unaendeshwa na adui?! Basi fanyeni kazi kutoa kiapo cha utiifu kwa Khalifa anayetawala kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah ya Mtume Wake (saw) kama walivyofanya Makhalifa waliotangulia, ambaye waliozikomboa ardhi na watu kutokana na uchafu wa Makruseda; La sivyo, mkiwategemea watawala hawa na kuridhika nao, basi Farauni atawaua watoto wenu na wanawake wenu, na atawanyenyekesha, akiwasalimisha kwa maadui zenu, mtaishi chini ya utawala wake kwa udhalilifu, heshima yenu itavunjwa, hata hivyo wajibu ni kuwakataa na kuwabadilisha.

Enyi Waislamu: jueni kwamba hakuna wokovu kutokana na utawala wa makafiri, hakuna ufumbuzi wa yale mnayoteseka kutokana na kuwekewa kanuni za ukafiri juu yenu, na kutokana na utawala wa makafiri juu yenu; isipokuwa mutabanni mradi mtukufu wa Uislamu na mfuate uongozi wa kisiasa wenye utambuzi na uaminifu, kisha watu wenye nguvu na ulinzi na viongozi waadilifu na waaminifu wa jeshi watajitokeza kuunga mkono mradi wa Khilafah watakaotikisa viti vya enzi vya tawala za watumwa, zilizoundwa na ukoloni, na kusimamisha utawala wa Uislamu kupitia Dola ya Khilafah juu ya magofu yake, itakayoongozwa na Imam wa Waislamu na ngao yao aliyosema Mtume (saw) kumhusu yeye: «إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika Imam ni ngao, watu hupigana nyuma yake na hujihami kwake.” Atatabikisha hukmu za Uislamu na kuubeba Uislamu ujumbe wa uongofu na rehma kwa walimwengu, ili kueneza hukmu zake zinazoshughulikia yale ambayo dunia imetumbukia ndani yake, ya uwanja wa unyama unaozalisha maradhi ya ndui na UKIMWI.

Msemaji Rasmi wa Kike wa Kitengo cha Wanawake
cha Hizb ut Tahrir Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu